Nashukuru
kwa kupata nafasi hii ya kushirikishana nanyi kwa sehemu historia ya maisha
yangu mpaka nilipofika sasa.Nimshukuru kipekee admin na rafiki yangu pia
Yunus Joas kwa kuandaa jukwaa hili adhimu ili tuweze kupeana hamasa na kupiga
hatua katika Nyanja mbali mbali chanya za kimaendeleo.
Pia
nikushukuru wewe kijana uliyeacha shughuli zako ili uweze kufuatana nami katika
simulizi hii itakayopelekea kujifunza kwetu sote na kusaidiana pia kiushauri
kwa namna moja ama nyingine.Ninafanya kazi na Mpango Mkakati Technologies kama
CEO.
Lakini
pia ni mhamasishaji wa mambo chanya katika jamii.Pia katika suala zima la
kuhamasisha mimi huendesha more campaign kila mwaka ambayo ipo chini ya
mpangomkakati kwa sasa.Kampeni hii ilianzishwa na mimi mwenyewe mwaka 2014
ikiwa na jina la 2014more na kauli mbiu isemayo ishi zaidi ya 2013 katika 2014.Ikiwa
na dhumuni kuu moja kuwahamasisha watu kutafuta kupiga hatua zaidi mbele na
kukataa kutorudi nyuma au chini ya pale walipokuwa.Lakini madhumuni
madogomadogo ya kampeni hii yalikuwa matatu:
- Suluhisho la ajira kwa vijana kupitia vijana wao wenyewe (Youth Centred solution to unemployment)
- Matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na miundombinu ya internet
- Nafasi ya kijana katika maendeleo ya nchi yake
Basi
nisiende sana huko maana badaye nitawaelezea vizuri na namna tunavyoifanya
kampeniIla kwa ufupi kampeni inaendelea mwaka huu ni 2016more "live beyond
2015 in 2016"Yenye kauli mbiu isemayo "INAWEZEKANA".

Nirudi
kwa upande wangu binafsi na maisha yangu tangu nazaliwa mpaka nilipo sasaMimi
ni mzaliwa wa pili kati ya watoto watano katika familia ya Bw. na Bi. Amos T.
Hulilo Baba yangu ni MchungajiMnano tarehe 28. 09. 1988 nilizaliwa.Nimekulia
kijiji cha Kamanga wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza mahali ambapo niliishi miaka
kumi ya kwanza ya maisha yangu kabla ya familia yetu yote kuhamia mjini kwa
majukum ya kikazi ya mzee wangu.
Nakumbuka
nikiwa nilisifika kwa kumbukumbu ya kuwakalili wageni waliokuwa wakija
nyumbani.Lakini pia nilitamani sana kuwa kondakta wa malori makubwa na kila
mara nilipanga mawe na kujenga mfano wa gari na kuingia ndani yake na
kuliendesha.
Lakini
mara kadhaa pia nilisikika nikisema kwamba nataka kuwa mchungaji baada ya
kupata hamasa kutoka kwa mchungaji mmoja aliyetokea wilaya ya Sengerema kuja kijijini
kwetu aliyekuwa akiendesha Pikipiki. Nikikumbuka hadithi hizi hunifanya nipate
nguvu ya kwenda mbele bila kukata tamaa.
Siku
moja alikuja jamaa mmoja anayefanya biashara ya kusukuma torori akiwa na viatu
vizuri nikamuuliza umepata wapi akaniambia nimesukuma torori nikanunua,
nikawaza kama torori ndio njia hata mi naweza nikatoroka nyumbani kwenda
gengeni nikasukume torori nipate Pesa za kununua tafu buti lakini sikufanikiwa
kufika nilizuiliwa njiani na ndipo mzee wangu alininunulia viatu hivyo.
Mzee
wangu alianza kunionesha umuhimu wa elimu tangu mapema.Alikuwa akitoka kwenye
biashara zake za samaki mchana alituketisha mimi na kaka yangu na kuanza
kutufundisha namna ya kuandika namba kwenye kibao maalumu alichokinunua pamoja
na chaki. Tulifirahia sana kujifunza.
Mwaka
1994 kwa mara ya kwanza nilipelekwa shule ya awali pamoja na kaka yangu hapo
kijijini. Nakumbuka tulikalia mawe na tuliandika chini. Enzi zile za kuzungusha
mkono juu ya kichwa na uguse sikio ndio uandikishwe darasa la kwanza .Mimi
nilihudhuria siku chache kisha nikaacha na kukaa nyumbani.Kaka yangu aliendelea
na mwaka uliofuata alijiunga na darasa la kwanza.
Mimi
nikiwa nyumbani na harakati zangu za kutimiza ndoto ya kuwa kondakta au
Mchungaji.
Maisha
yalikuwa mazuri maana nilicheza na watoto wenzangu nikitikisa miti kama gari
huku nikichuma Pesa zisizoisha juu ya miti yaani matawi ya miti .Siku moja
asubuhi saa mida ya saa tatu katika harakati za kuendelea kucheza na jamaa
zangu wavulana na wasichana. Niliruka toka juu ya jiwe kubwa hadi chini kwenye
shamba la mahindi.
Nilivyotua
chini pembeni yangu niliona nyoka mkubwa sana aliyejikunja nane, sifahamu kama
alikuwa amelala au ametega mtego na mimi yawezekana nilikuwa
nimepatikana.Haraka haraka nikaingiwa na ukimya na ujasiri wa kutopiga kelele
wa kulia wa kukimbia isipokuwa kutembea taratibu kwa kunyata ili mshikaji
asishtuke kwamba mi nipo ili anifanyie yake.Huwa nikiifikiria hii sehemu nawiwa
kusema sikustahili ila niliachwa kwa sababu Fulani .
Nikafanya
kazi ya kusomba mawe jamaa wakampiga na baadaye wakampiga na jembe kama leki
lakini Lenye meno marefu na bado akawa na nguvu za kuvutia upande wakeLakini
mwishoni tulimwua yule nyoka.
Mnamo
mwaka 1996 kwa hiari yangu na kupenda kwangu mwenyewe na kwa maamuzi ambayo
mpaka Leo nashangaa niliamua kurudi shule.Kaka yangu aliagizwa udongo mfinyanzi
ili atengeneze Sanaa ya shule kwa somo la stadi za kazi nafikiri, mimi pia
nikaenda naye kutafuta udongo mfinyanzi na nikatangaza kwenda shule siku
iliyofuatia.Asubuhi kulivyokucha kaka yangu alivyoamka na kujiandaa na mimi
nilifanya hivyo.
Alipoanza
kuondoka nilimfuata nyuma tukaongozana.Nilipofika maeneo ya shule ya awali
ambapo zamani ilikuwa stoo ya pamba niliamua kutupa udongo mfinyanzi na
kuelekea darasani huku nikimuacha kaka yangu akiendelea kwenda shule ya msingi
maana ilikuwa mbele kidogo zaidi ya shule yetu ya vidudu.
Niliingia
darasani, Mwalimu alivyouliza wanafunzi wapya na mimi nikaenda kujiandikisha
upya, huyu Mwalimu alikuwa mzee sana alifahamika kwa jina la Malele.Mwanzo wa
shule haukuwa mwepesi, nilianza hatua ile ile ya kuandika chini na nikiwa sijui
kitu.Nakumbuka siku moja nikiwa sijui nifanye nini maana siwezi dada mmoja
anaitwa Ester alinitia moyo kwa kuniambia maneno haya, " usihofu utajua
tu", haya maneno huwa nayakumbuka hadi Leo na picha ya yale maongezi ipo
kichwani mwangu mpaka kesho kutwa.
Yawezekana
sikuyaelewa yale maneno lakini naamini yamechangia sana mimi kuwa jinsi nilivyo
Leo maana yalinipa moyo wa kutokata tamaa na kuniongezea nguvu ya kwenda mbele
zaidi .Usiache kumtia moyo mtu kwa kumwambia maneno mazuri, maneno yana nguvu
sana.
Kweli
nikaendelea kwa bidii. Kuna wakati nilikosa hesabu zote niliporudi nyumbani
nikamsimulia mama, kisha akanifundisha namna ya kujumlisha na kutoa kwa
kuhesabu vidole vya mikono tangu siku hiyo kufeli hesabu kwangu ilikuwa
historia, hii nayo sitaisahau ASANTE SANA MAMA.Usiishie kuwaandikisha watoto
wako shule tu waweza kuwa Mwalimu wao pia.
Mwisho
wa mwaka yaliyo mwa majina ya wanafunzi wanaojiunga na darasa la kwanza Shule
ya Msingi Kamanga, na mimi nilifurahi kusikia jina langu likitajwa katika
nafasi ya 37.Mwaka 1997 nilianza darasa la kwanza chini ya Mwalimu yule yule
huku nikiwa sijui kusoma na kuandika nisichoweza kukisoma ila mkali wa kuhesabu
namba na kujumlisha na kutoa.Nikiwa darasa la kwanza nikifanya juhudi nijue
kusoma na nikafanikiwa.
Nilitumia
kitabu cha hadithi ya chombo kilichovunjika kama kitabu changu cha kujifunzia
kila nilipopata muda wakati wa mapumziko shule chini ya mti wa mzambarau na
niliweza kusoma hata vitabu vingine pia na stori ya dagaa bila kukwama nadhani
mnaikumbuka.Nilifanya vizuri darasa la kwanza na kushika nafasi ya sita.Mwaka
1998 Januari nilihamishiwa shule ya Msingi Kirumba jijini Mwanza.
Nilipofika
tu mitihani yangu ya kufunga mhula wa kwanza nilikuwa mtu wa 128.Baba
hakufurahishwa na hali hiyo ingawaje nilikuwa nimepata alama za juu tu.Mhula
uliofuata nilianza utoro na kuchelewa shule nikiwa kundi moja na kaka yangu
pamoja na rafiki yangu Paschal.Siku moja nilikimbizwa sana na nikaamua
kujipeleka kwa Mwalimu kwa hiari na nikachapwa viboko visivyozidi vitatu
ambavyo hata sikusikia maumivu yake sana kiasi cha kulia na tangu siku hiyo
nikasema utoro basi Niliendelea vizuri na darasa la Tatu hali yangu yakitaaluma
ilianza kubadikikaNikashika nafasi ya nne.
Darasa
la nne tukafungana wawili nafasi ya Tatu mhula wa kwanza na mtihani wa taifa
nikang'ara kwa kushika nafasi ya kwanza shuleni kwetu.Darasa la tano nikawa wa
tatu la sita nikawa wa pili na darasa la saba nikawa namba moja na kushika
nafasi ya nne mtihani wa mock wilaya ya mwanza, hii ilikuwa 2003.Nakumbuka
darasa la nne na kuendelea ndipo nilipojifunza kuomba Mungu kwa kuelekezwa na
mama yanguIkiwa ni pamoja na kufunga kwa mahitaji yangu ya kimasomo.
Hivyo
siwezi kusema neno au mimi ni wa tofauti sana lakini Mungu alihusika na bado
anahusika kwa kiwango kikubwa na maisha yangu.Baada ya kumaliza darasa la saba
sikujiunga na preform one.Nikiwa na rafiki yangu Mandela tuliamua kuanzisha
biashara ya genge.Kweli tulipata kisehemu nyumbani kwao tukajenga kipanda na
tukawa tunaleta vitu kutoka soko la Kirumba na kuuzaBaada ya kufanya biashara
hivyo kwa muda niliondoka kwenda Musoma kwa Mjomba wangu ambapo nilipata fursa
ya kusoma preform one mpaka matokeo yangu yalipotoka na nikachaguliwa kujiunga
shule ya ufundi Mazengo Iliyopo Dodoma ambayo kwa sasa ndiyo chuo cha mtakatifu
Yohana (St. John university).
Hapa nilikuwa miongoni mwa formone wadogo kuliko wote
Na siku ya kwanza kuachwa shule mzee alivyonipeleka nililia machoziLakini
niliamua kukomaa na sikusumbuliwa na wadogo tulilindwa sanaMaana form two
walikuwa wasumbufu sana Basi hapa ufahamu wangu uliongezeka na nikakutana na
mazingira mapya na watu wapya na ambayo yalinipa fursa ya kuishi kwenye mfumo
mpya wa maisha ambao ulikuwa na Uhuru zaidi wa kujitegemea na kuamua japokuwa
nilikuwa nimebanwa na sheria za shuleNilijisikia vizuri na fahari sana kuwa
mmoja wapo wa wanafunzi wa shule hii japo chakula hakikuwa kizuri
sana.Nilipomaliza form two tuliambiwa tuchague shule zingine maana Mazengo
itakuwa chuo kikuu.
Mimi
nilijaza Moshi Technical na nilipelekwa huko Nikasoma form three na form
fourKisha nikafaulu kwa daraja la kwanza point 11 na nikachaguliwa kujiunga na
shule ya sekondari Ilboru combination ya PCMWakati nikiwa form two baba
alinitia moyo niwe daktari wa binadamu lakini nilikataa.
Nikiwa
form 3 nikiacha somo la Baolojia na kusoma jiografia Huku nikiendelea
kushikilia wazo la kuwa mhandisi wa talakilishi na kuwa mchumi ukiwa mpango
kando wanguNilipomaliza kidato cha nne na baada ya kuwa na matokeo mazuri
nilirudi kutamani sana kuwa Dk. Kwa sababu fulani fulani ambazo badaye
niligundua si za msingi.
Niliwaza
sana mpaka nikaugua mwishowe nikamwambia baba.Alichofanya alinishauri na kisha
akanipeleka kwa daktari baada ya hapo nikawa vizuri na maisha yakaendelea
Maisha Ilboru yalikuwa mazuriNilisoma kwa bidii sana .Huku nikiahirisha kwenda
nyumbani na kubaki Arusha ili Pesa yangu ya nauli ninunu vitabu na kusoma
masomo ya ziada maana vitabu vilikuwa ghari kidogo tofauti ni vya o level .
Niliendelea kutamani na kumwomba Mungu anipe nafasi ya
kujiunga chuo kikuu cha Dsm kwa masomo ya uhandisi wa talakilishi Hapa kidogo
nilianza kuhisi mwanga kwa mbali wa badiliko la maisha yangu Juu ya nilivyowaza
na nilivyoyaona maisha yangu .Sikuwahi kujiunga na club yoyote lakini kwa mara
ya kwanza nilijiunga na English Club Mi sikujua kitu kingine zaidi ya kusoma tu
na kusali pamoja na michezoNilipoanza kwenda debate club ndipo Nilipoona kitu
cha ziada kwa wenzangu.Waowalikuwa na uwezo wa kujenga hoja kwa lugha ya
kingereza tena kwa kujiamini hata kwenye uwepo watoto wa kike na mimi sikuweza
japo nilijaribu mara kadhaa huku nikipiga mweleka kwa vigugumizi vingi na
kujiumauma Nilijiona duni sana.Nulijiona mimi si bora sana.
Pia nikakumbuka jinsi nilivyo na meno ambayo
hayajapangika vizuri ikanisumbua sanaNilipomaliza kidato cha sita ndugu zangu walinitaka
nibaki Arusha wanitafutie shule ya kufundisha kwa muda Ila nilikuwa na
mpango wa kwenda kuanzisha tuition centre.
Kwa
hiyo Nilirudi nyumbani mwezi wa Tatu 2010.Nikiwa na rafiki yangu Hamis ambaye
ni daktari kwa sasa tulitafuta centre tukaanza Hatukuwa na wanafunzi wengi
sanaLakini baada ya siku chache niliitwa na mwalimu wangu aliyenifundisha
masomo ya ziada nikiwa kidato cha tano alinisihi na kunibembeleza niende
nikafundishe advanced physics na mamlaka yote yatakuwa juu yangu na hata fedha
nitakazotoza zitakuwa zangu.
Kwa
mara ya kwanza milikabidhiwa darasa Lenye wanafunzi zaidi ya hamsini na
nikaanza kufundisha huku nikijipatia Pesa nyingi kwa wakati huo.Nilifanya kazi
hiyo mpaka matokeo yangu yalipotoka Wanafunzi walinikubali sana Na hata matokeo
hayakuniangusha pia Matokeo yangu yalipotoka nilifaulu kwa daraja la kwanza
tena point 5 Nikaomba kujiunga Chuo kikuu cha Dar es salaam kwa masomo ya
shahada ya kwanza ya uhandisi wa Tarakirishi na Teknolojia ya Habari (BSc. in
Computer Engineering and IT).Nikijisikia furaha sana kutimiza sehemu ya malengo
yangu ya kusomea kitu nikichokitaka.
Nilimshukuru Mungu sana kwa hatua hiyo Binafsi
changamoto ambayo ilinisumbua kwa muda mrefu ni kitojiamini na kujiona mnyonge
japo kikawaida usingeweza kunigundu Basi mnamo mwezi oktoba 8. 2010
nilijiunga rasimi na chuo kikuu cha Dar es salaam Hapa malengo yangu yalikuwa
kusoma kwa bidii na kufaulu kwa alama za juu kama kawaida nikiwa na ndoto za
kufanya kazi na makampuni makubwa kama Tigo, Vodacom, TTCL au kubaki kuwa
mkufunzi wa chuo Hiyo ndiyo picha niliyoingia nayo chuo kikuu.
Na
kila usiku mmoja niliyoenda kulala nililala kwa amani nikiitazamia haja hiyo ya
moyo wangu, lakini vile vile niliamka asubuhi kwa shauku kubwa nikijituma
kulifikia hiloNikiendesha mjadala mkubwa sana nikiwa semester ya kwanzaNa
semester ya pili Na nikifaulu kwa GPA nzuri sana Niliwiwa na kujiskia kweli
nastahili kuwa Mwalimu Na wengi waliniambia hivy Na kunisifia kuwa ningefaa
kuwa mhadhiri wa chuo kikuu.
Kipindi hicho chote nilikuwa na mitazamo ile ile
niliyotoka nayo huku chini Natumai tupo pamoja, naomba kuishia hapo na kesho
nitaendelea maana sehemu inayofuatia ndiyo chanzo cha mimi kuamua kuwa
mjasiriamali na mhamasishaji pia.
Asanteni
kwa kunisikiliza
ITAENDELEA
………