Nilianza
kushawishika na kujisikia kugombea nafasi ya uongozi kuwawakilisha mwaka wa
kwanza kama mbunge waoNilichukua fomu huku nikiwa na uoga na kitojiamini ila
nilijitahidi kutokuonyesha kwa hali ya nje.Sikutoa
taarifa kwa wazazi wangu kwamba nimeamua kugombea uongozi maana wangenizuia kwa
sababu miaka hiyo migomo ilikuwa mingi na watu walifukuzwa chuo Baada ya
mchakato mzima kufanyika sikupita kwenye mchujo.

Niliiongoza
kwa mafanikio makubwa sana ndani ya mwaka mmoja tu na tukapewa kuwa idara
Katika
uongozi wangu tulifanikiwa kununua vifaa vingi ikiwa ni pamoja na kuongeza
ujuzi na mipaka ya kazi hadi nje ya chuo Tulitengeneza na kuprint kadi za
harusi.Kutengeneza DVD za Matukio mbali mbali Hapa ndipo nilipoanza kuingiwa na
element na moyo wa kufanya biashara Kwa bidii Hapo kabla nikiwa mwaka wa kwanza
nilifanya lakini haikuwa kama mwaka wa pili Nakumbuka mwaka wa kwanza
nilijiunga na wenzangu watatu tukajiita TRUST COMPANY.
Hapa
tulifanya biashara ya kuuza DVD empty pamoja na CD empty ikiwa ni pamoja na
kufanya vomputer maintainance and repair Wakati nikiwa mwaka wa pili kasi yangu
ya kutaka kuajiliwa ilipungua. Matendo yangu yaliashiria kwamba nilipenda
siasa.
Na
nilifuatilia kwa karibu sana siasa za chuo na hata za kitaifa Wakati huu migomo
ilikuwa Mingi na ilinigusa sana ila sikuwa msitari wa mbele sana Nakumbuka
nilitokea kupenda sana mambo ya uongozi Katika maktaba yangu ndogo ya vitabu
ambavyo sikuwahi hata kuvisoma maana sikuweza na sikuwa na kingereza
kilichonyooka nilikuwa na kitabu cha John C. Maxwell chenye kichwa kisemacho
"21 irrefutable laws of leadership ".
Kulingana
na kiu yangu ya uongozi nilianza kukisoma bila kujali naelewa vizuri au la Hapo
ndipo tabia ya kusoma vitabu ilipozaliwa kwangu Nilikisoma kila nilipopata muda
hata kama dakika moja tu Nilikisoma nikiwa kwenye daladala hata ofisi za watu
Nilikisoma darasani pia nikisuburi mwalimu aingie Nilianza kununua vitabu
vingine Na kuvisoma pia.
Baada ya
muda tabia hiyo ikawa sehemu ya maisha yangu japo ilinichukua muda kusoma na
kumaliza kitabu kimoja Nakumbuka siku moja nikiwa na test nilishindwa kujizuia
nikajikuta nasoma kwanza kitabu cha Maxwell ili kiishe ndio nisomee mtihani.Nashukuru
Mungu nilipata Uwezo wa kumudu yote Mwaka huo ulitokea mgomo na viongozi
wengi sana walifukuzwa na wengine kusimamishwa chuo Mimi pia nilihofu sana
kufukuzwa maana kuna wakati nilikuwa na kundi la wanafunzi wenzangu pale
utawala nikapanda juu ya kiti kuhamasisha na kuwatoa uoga maana tunadai haki zetu
hii iliitwa kutoa modality.
Nashukuru
Mungu Nilipona katika hili Darasani nilijitahidi kujenga mahusiano mazuri na
kila mwalimu aliyenifundisha Nilifuta ubao kila mara na nikisaidia kufunga
projector na kuitoa katika kila kipindi Na watu walinifahamu kwa hilo .Baadhi
hawakuipenda sana tabia hiyo japo haikuwapunguzia chochote ..Na baadhi
walidhani nafanya hivyo nikiandaa mazingira ya kushinda uongozi kwa kipindi
ambacho kilikuwa mbele Lakini mimi sikujali.
Nilifanya
kila kilicho chema machoni pangu hata kama watu hawakuniunga mkonoNilitamani
sana wanafunzi tuwe na maisha yatakayotoa mchango kwa jamii hata tungali shule.Nikiwa
mwaka wa pili yaliyokea mafuriko hapa Dsm na watu waliachwa bila makazi
Niliguswa sana na jambo hilo nikaamua kutoa wazo na kuhamasisha wanafunzi
wenzangu tuchange tulichonacho ili tuwasaidie.
Kweli
tulikusanya michango japo kulikuwa na changamoto za mwitukio wa watu.
Hivyo
tulipata kiasi cha fedha na kisha mimi na mbunge wangu kwa wakati ule Bahati
Kamwela tulipeleka msaada wa vitu mbali mbali vilivyonunuliwa kwa kutumia fedha
iliyokusanywa.Haya yote
yalizidi kunifanya nipende mambo ya uongozi na yalinifundisha kuwa kiongozi
maana yake nini hata kama hauna cheo Fulani.
Muda
ulipofika nilichukua fomu ya kugombea ngazi ya ukatibu wa college (COICT)
Hapa
nilipita mchujo na kugombea lakini kura hazikutosha Ila nilikuwa mbunge wa
kuteuliwa ikiwa tiketi ya kuwa mjumbe wa kamati kuu ya college kama mwakilishi
wa taaluma.
Nilifanya
kazi kwa bidii kushughulikia matatizo ya wanafunzi wenzangu Pia niliteuliwa
kuwa naibu waziri wa mawasiliano na Habari katika serikali ya wanafunzi .Wakati
huo nilifanya bidii kunoa kingereza changu japo hakukuwa na wengi wa kuongea
nao hivyo ilibidi niongee peke yangu au nilisikilize speech a kuzirudia.
Nilipakuwa
video za watu wengi mashuhuri kutoka youtube na kuzidikiliza nikiwa na lengo la
kujifunza .Kabla nilisumbuliwa sana na muonekano wangu Hususa ni mpangilio wa
meno yangu ya mbele hayakuota kwa mpangilio mzuri Hili lilinisumbua siku nyingi
na bado liliendelea.
Pia
nilichukua hatua ya kujifunza zaidi kupitia historia za watu wengine kama
Martin Luther King Jr., Malcom X, Cheguavara, Mwl. Nyerere, Patrick Lumumba,
Mobutu, Nkwame na wengine wengi
Historia
za watu hawa na yale waliyoyafanya yalinipa kujifunza na sababu zaidi ya
kulitafuta kusudi la kuishi kwangu.
Walinipa
sababu ya kutokata tamaa hata kama mazingira ni magumu na watu hawaniungi mkono
Lakini
kila mara nilijitahidi kuishi kile nilichokismini Mara suala la kuajiliwa
likafutika nikaanza kuwaza zaidi kumiliki kampuni na kusaidia watu kujitambua
Sikutamani tena maisha ya kwenda ofisi moja hadi nyingine kuomba kazi Nakumbuka
siku moja baba nilienda kumtembelea baba hapa Nairobi nchi jirani ya Kenya Kwa
kipindi hicho na yeye alikuwa masomoni huko.
Alinitaka
nimweleze ni nachoweza juu ya maisha ya mbele na mipango niliyonayo Tuliongea
mengi na nikamwambia jinsi ninavyoguswa na maisha duni ya watu na ambavyo
ningependa kuwasaidia wajikwamue kwa kadili nitakavyoweza. Na nikamwambia sina
mpango wa kuajiliwa Ila niko radhi nianze na kitu chochote hata kama ni kidogo.
Alipenda
mawazo yangu na moyo nilioonyesha wa kutaka kuwasaidia watu, lakini akanishauri
na kunisihi niajiliwe walau kwa miaka mitano kisha ndio nianze shughuli zangu
Nilikubali ushauri wake kwa wakati ule na kuahidi kuufanyia kazi ili hali ndani
bado nilikuwa na maamuzi yale yale huku nikiwaza namna ya kumshawishi
akubaliane na maamuzi yangu ili nimwondoe wasi wasi.
Nikiwa
mwaka wa pili mwisho mimi pamoja na Rafiki zangu watatu waliokuwa wamehitimu
masomo mwaka huo tulianzisha kampuni ya IT and Media lakini haikifanikiwa kukua
na ilikufa pole pole na kusambaratika.
Nikiwa
mwaka wa Tatu 2013 niliendelea kusoma vitabu na hapa nilikuwa nimejitoa IT
Bench na kuwa mwanachama wa kawaida Niligombea uongozi tena nafasi ya
Mwenyekiti wa college niliyokuwa nikisoma na nikapita bila kupingwa.Hii
ilinifundisha kutokata tamaa na kutoyaangalia sana madhaifu uliyonayo lakini
kuangalia na kutumia nguvu au uimara wako katika maeneo Fulani.
Nikiwa
mwaka wa tatu zilitoka nafasi za kujiunga na kozi fupi ya uongozi iliyoitwa
chini ya East African Uongozi school ambayo ikijumuisha wanafunzi wa vyuo mchanganyiko
Afrika Mashariki.Nilituma
maombi yangu na nikaitwa kwenye usaili Baada ya usaili mimi sikuchaguliwa
kujiunga Niliumia sana kuikosa nafasi ile muhimu kwangu.
Baada ya
kukosa na kuumia nikatulia na kukubali kwamba nimekosa ile nafasi Maana
hata baba nilishamwambia na faida zake pia .Baada ya kukubaliana kuwa nimekosa
na kukiri wazi mbele yangu kwamba waliopata wameonekana kuwa na vigezo kuliko
mimi Nikijiuliza tena sababu za mimi kutaka ile kozi kwa shauku kubwa ilikuwa
ni nini?Je ni malipo ya dola za kimarekani 15 kwa siku?Au
nilitaka sana kujifunza mambo ya uongozi ?Jibu langu likawa dola 15 ndio lakini
zaidi sana kujifunza Basi nikampigia simu Mwalimu alinifanyia usaili nikamuomba
nipate nafasi ya kusoma bila kulipwa chochote na nikamuahidi sitakuwa na Madai
yoyote.Akaniambia haina tabu we siku ya kuanza njoo.
Nikafurahi
sana Siku wanafungua mafunzo kwa sherehe sikuweza kuhudhuria nilikuwa safarini
kwa mahafari ya baba yangu alikuwa anapata shahada yake ya kwanza Bahati nzuri
siku hiyo usiku ndiyo nilifika dar kutoka Nairobi.Kesho yake
asubuhi mapema kabla darasa lianze nilienda kwa mwalimu akaniambia watu wamejaa
na yeye Hana mamlaka ya kuongeza huku akisahau kuwa aliniambia nije siku ya
kuanza Nilijisikia kuishiwa nguvu maana nakosa kozi hivyo.
Lakini
katika maneno yake aliniambia VC ndiye mwenye mamlaka Na huyu hakuwa mwingine
alikuwa Prof. Rwekaza Mkandala ambaye bado ni VC hadi sasa Nikamfuata ofisini
na kujitambulisha na kumweleza kila kitu na kwamba ninachohitaji ni kusoma tu
na si vinginevyo.Naye pia
akaniambia itakuwa ngumu maana kuna gharama ambazo wenzangu wanalipiwa sasa.
Nikamwambia
nikizijua hizo kama zipo ndani ya Uwezo wangu nitalipa tu Akakaa kimya kwa muda
kisha nikamuaga naondoka wakati nanyanyuka kwenye kiti niondoke maana
imeshakuwa nongwa akaniambia we nenda coordinator akwambie hizo gharama kisha
utaamua kujiunga au kuacha.Hilo jibu
likanipa furaha maana nikajua nishajiunga japo mfukoni sikuwa na hata senti
moja ya kulipa.
Nikaenda
nikamwambia coordinator VC amekubali nijiunge ila ameniambia nikuone unijulishe
gharama ili nilipe.Coordinator
akasema sawa haina tatizo nione wakati wa mapumziko baada ya kipindi Kweli
baada ya hapo nilienda kumwona na akaniambia gharama zote ni dola za kimarekani
180 sawa na tsh. 290,700/= maana exchange rate kwa wakati huo ilikuwa sh
1615/=Nikaona ni nyingi kwangu maana sikuwa na kitu wakati huo na nilibaki chuo
kushughulikia masuala ya wanafunzi wenzangu ila nikamwambia haina tatizo
nitalipa kwa awamu.
Basi
maisha yakaendelea wakati wa kozi nilitokea kupendwa na watu wote darasani hata
walimu pia.Pia kama kawaida mimi ndiye niliyepewa jukumu la kufunga na kuondoa
projector wakati wa session, hapo nikaanza kuona umuhimu wa kihelehele changu
kuwafungia walimu projector na kufuta ubao Kule darasani bila kudai chochote
wala bila kutumwa na mtu.
Nilijitahidi
kutokuonyesha kwamba mimi silipwiNa nilifanya hivyo. Nilijitahidi kutoa maoni
ya namna ambavyo tungeweza kujifunza zaidi na ilinipa fursa ya kushinda nafasi
ya ukatibu mkuu katika uongozi wa wanafunzi huku nikipita kwa kura nyingi sana
kuliko mpinzani wangu.
Nilifanikiwa
kusoma na kumaliza kozi vizuri.changamoto nilizokutana nazo wakati wa kujiunga
na masomo niliyojifunza pamoja na watu niliokutana nao, nikajikuta nimekuwa
tofauti na mwenye mawazo chanya zaidi.Kwa kweli nikiwa uongozi school
nilijifunza mengi.
Nilikuwa
najua kutengeneza connectionLakini hapa nilijifunza zaidiBaada ya hapo nilipata
fursa kuhudhuria debate ya wanafunzi wa vyuo vikuu wa yumuiya ya Afrika
Mashariki Ilifanyika pale JB Belmont Hotel Posta .Kiukweli nilikuwa
nimeyumba kiuchumiIla nilikuwa na suti ambayo mzee alikuwa ameninunulia Kwa
hiyo nikawa nahudhuria kila siku, hapo nipo smart sana but kwa mfuko sina kitu
Ila uzuri tulipata lunch na nilikuwa na Pesa kidogo ya kunisaidia kurudi chuo
kwa daladala
Nilijitahidi
kujenga mahusiano na watu wapya.
Interview
ya kwanza tulifanya na East Africa Radio. Na hii ilichukua dakika kumi na tano
hewani.Sio Siri
hii kwangu ilikuwa ni hatua kubwa sana na nillizidi kuhamasika na kupenda
masuala ya diplomasia na siasa kwa ujumla.Tulivyotoka nje tulikutana na
Constantine Mihambo wa capital radio naye akaomba tufanye naye interview Hii ya
sasa ilikuwa recorded ambayo ingeruka kesho yake kwenye kipindi cha morning jam
ambacho yeye ndiye mtangazaji Niliwataarifu watu wasikilize na nilipata
positive feedback nyingi.
ITAENDELEA
……….