Jana nilikuwa kwa kaka yangu mmoja Bwana Tobias Nahumu anayeishi na familia yake, mke na watoto 2 maeneo ya Sinza Makaburini.Miongoni mwa vitu tulivyoongolea ni kuhusu familia yake na maisha kwa ujumla ikiwemo shughuli zake za kila siku za kutafuta kodi ya nyumba, chakula na nguo za mke na watoto.
Nilijisikia vibaya sana, baada ya kaka yangu Tobi kulalamika juu ya maisha yake. Anadai maisha ni magumu sana, hata kazi anazofanya ni ngumu, aliongea vitu vingi sana ambavyo siwezi hata ku-share hapa kwa sababu huyu ni sehemu ya familia pia haiwezi kuleta picha nzuri na sio heshima.
Ambacho siwezi kuficha tu ni kwamba Tobi "amekata tamaa". Hana matumaini tena ya kupata mafanikio makubwa ya kipesa, kiimani na furaha kwa ujumla.Baada ya kurudi gheto kwangu, nikajikuta na msongo wa mawazo na viulizo vingi kichwani mwangu. Inakuwaje kijana anakata tamaa?
Nilichokifanya nikaamua kumpigia simu rafiki yangu, Damian ambaye anaishi Arusha, nikamuuliza kwanini vijana wengi wanakata tamaa mapema hasa hapa kwetu Tanzania? Nilifanya hivyo kwa sababu siamini kijana wa miaka 29 kukata tamaa ya maisha au kulalamika.Damian ni mtafiti wa maendeleo ya vijana, baada ya kupiga nae story kwa muda wa nusu saa, akanipa takwimu ambazo zimenishtua kidogo, na hicho ndo kilichonipelekea kuandaa haya makala!
Damian anadai kuwa, "watu 3 kati ya 20 ndio hawajakata tamaa ya maisha ila 17 hawana matumaini ya kufikia malengo yao".
Ni ukweli usiopingika kwamba, "mambo yote huharibika tu pale unapokata tamaa". Kukata tamaa ni kupoteza matumaini juu ya kitu fulani. Ukikata tamaa basi umefukuza mafankio nyumbani kwako.
Hivi na wewe unajihisi kukata tamaa?, leo nimekuandalia sababu kuu 4 kwanini hutakiwi kukata tamaa!!
1.BADO UKO HAI.
Sababu ya wewe kutokupoteza imani na matumaini ni wewe kuwa hai muda huu. Hata kama upo mahututi muda huu, bado hujafa, uko hai. Jipe matumaini kila kitu kitakaa sawa. Fursa zipo nyingi sana, unaishi kwa sababu fulani, kuna kitu unatakiwa kukifanya kabla ya kuondoka hapa duniani.
2.BADO UNA NAFASI YA KUFANIKIWA.
Nafasi ni ya kila mmoja, acha woga pambana, ulizaliwa kufanya vitu vikubwa. Jikubali.
3.CHANGAMOTO NI SEHEMU YA MAISHA!.
Ukiona wewe hupitii katika magumu basi hudhaniwi kufanikiwa kabisa. Vikwazo na changamoto ndio chachu ya mafanikio. Changamoto ni msukumo wa wewe kupambana. Nelson Mandela, Abraham Lincoln, Barack Obama, Bill Gates, Nkwameh Nkrumah, walipitia changamoto nyingi sana. Ukubwa wa changamoto huendana na ukubwa wa mafanikio. "Hakuna njia rahisi ya mafanikio sehemu yoyote, na wengi wetu tunapaswa kupitia mfereji wenye giza(wa kifo) tena na tena kabla ya kufika kwenye kilele cha matamanio yetu".
4.MAFANIKIO NI MAAMUZI.
"Umaskini hauji kwa bahati mbaya, hutokana na matendo ya kila siku ya mwanadamu". Kila mtu anahitaji maendeleo, lakini si kila mtu yuko tayari kuchukua hatua, kushika wajibu na majukumu ya kumpeleka kwenye hayo maendeleo na mafanikio anayoyahitaji. Amua leo kuwa tajiri au maskini.
Jamani kila kitu kinawezekana, tatizo la sisi watanzania au waafrika kwa ujumla hatupendi kujifunza hatupendi kujaribu, unapoacha kujifunza huna tofauti na maiti au mfu anayetembea.
Muda mwingi sisi lalamika tu, kutafuta "taarifa na maarifa juu ya ndoto & malengo yetu hatutaki". Afu tunasema maisha magumu, maisha sio magumu, vichwa vyetu ndo vigumu.
Wewe una malengo gani?, Unapenda kufanya nini? Unapenda kuwa nani?
Ifuatayo ni list ya "vitabu" vyenye "taarifa, maarifa, ujuzi & siri za mafanikio na maisha mwanadamu"
1.JINSI YA KUANZISHA BIASHARA NA UENDESHAJI WAKE.
2.MBINU 39 ZA KUPATA UTAJIRI
3.INUKA TOKA KWENYE KABURI LA UMASKINI.
4.KWANINI UFELI
5.MBINU 40 ZA KUFAULU MTIHANI
6.HATUA MUHIMU ZA KUBADILI HISTORIA YA MAISHA YAKO.
7.MAMBO 20 YATAKAYOKUFANYA UFURAHIE MAISHA YAKO.
8.SABABU 12 KWANINI NDOA NYINGI LEO ZIMEJAA MIGOGORO.
9.KANUNI YA MAISHA KAMILI
10.HEKIMA CHUMVI YA MAISHA.
11.NJIA IENDAYO UZIMANI
12.INUKA
13.NGUZO TATU ZA MAISHA
14. SIRI SABA ZA KUWA HAI LEO
NB; Vitabu hivi vimeandikwa na waandishi vijana walio bobea katika masuala ya uongozi, imani, ujasiria mali, biashara, elimu, michezo, uhamasishaji, ushauri, mahusiano & saikolojia.
Miongoni mwa vijana hao ni;
Joas Yunus
John Bosco
Adabert Chenche
Magret Mush
Ana Boniface
Laita N. Mwashiba
Kelvin Kitaso
nk, wote ni kutoka Tanzania!
Kati ya hivi vitabu vyote, hakuna hata kimoja kinachofikia bei ya kile kiatu unacho vaa kwa ukienda kwa "mpendwa" wako.
"~Soma vitabu, Ongoza Wenzako ~"
Tuwasiliane kupitia
0757065702