Nick Vujicic ni Muastralia aliyezaliwa
bila miguu wala mikono lakini kuzaliwa kwake hivo hakujazuia kuishi kusudi
lake. Kwa sasa ana miaka 32 na ni mwanzilishi wa Taasisi ya maisha bila miguu na
ni muhamasishaji, huwapa matumaini wale wenye ulemavu, ameoa na ana mtoto mmoja.
Nick anasema "Naamini kuna sababu
ya kwanini kitu kinatokea. Fanya kila unaloweza bila kukata tamaa huku
ukimwamini Mungu. Nilizaliwa na mtazamo huu namshukuru Mungu kwa kila
nilichonacho. Wazazi wangu hawakunilea tu katika Uzuri lakini pia walikuwa
jasiri kupata watoto wengine "
Anaendelea kusema "Mama yangu
alikuwa Mkunga na hivyo alijua fikra kuhusu maswala ya uzazi. Alijua fikra kuwa
mimba yake ilikuwa na shida wakati niko tumboni. Alipiga utrasound zote. Nilivyozaliwa watu wengi walishtuka kuona sina Miguu wala mikono.
"Asubuhi siku ya kuzaliwa kwangu. Baba alikuwa amekaa pembeni ya mama na aliona kuwa mabega yangu hayakuwa na
mikono. Alitaka kuzimia na kutapika ilibidi Muuguzi ampeleke nje. Ukweli ni
kwamba sikuwa na mikono wala miguu na madaktari walishindwa kueleza chochote
kuhusu tatizo hilo". Alisema Nick
Nilikuwa mlemavu wa kwanza kupelekwa
kwenye mfumo wa shule wa Australia . Nilinyanyaswa na kutengwa sana shuleni kwa
hali niliyokuwa nayo. Wazazi wangu waliniambia kuwapuuza watu walionibeza.
Kila mtu anatafuta kitu cha kumfanya
afurahie maisha. Nilitaka kujua kama mimi si wa kufa tu. Kila mara mtoto
akinicheka au kunitenga hofu ilinijaa na nilikimbia kwenda nyumbani.
Nilipokuwa na miaka 10 nilitaka kujiua. Nilihisi sina thamani na nilifikiri nitaendelea kuwa mzigo kwa wazazi wangu na
kamwe nikadhani sitakuja kuoa. Hii iliendelea mpaka pale nilipoona mvulana
ambaye naye alikuwa hana mikono wala miguu kama mimi. Nikajua kumbe siko peke
yangu.
" Ninaogolea, kuvua samaki na
kufanya mambo mengi kama kuperuzi kwenye mtandao na mengineyo " alisema Nick. Kama Kijana nataka kuwa
huru kadri iwezekanavyo. Wazazi wangu waliniambia "hujui unaloweza kufanya
mpaka pale utakapojaribu "Naweza kupiga mswaki na kuosha nywele zangu. Katika mazingira yoyote nafanya kadri ya uwezo wangu. Maisha siyo kile
ulichonacho lakini ni vile unaweza kukitumia kile ulichonacho. Siogopi kujaribu
na kushindwa.
Nimetembelea nchi 58 na maili milioni 3
(hii siyo kudanganya).Ninamshukuru Mungu nimekuwa nikiongea na viongozi wa
Dunia akini pia yatia na wale wote waliosaulika na kuonekana hawana faida kwa
jamii.
Nilianza kuhamasisha wengine Australia nikiwa
na miaka 19 na kisha nikitambea duniani ndani ya miaka mitano. Nina ndugu
Califonia na wamekuwa wakinitia moyo nisonge mbele. "Nick unaweza kufanya
ndoto zako ziwe za kweli na kuufikia ulimwengu mzima "Nilianza maisha
bila miguu wala mikono.
Nick anajifunza kucheza mchezo wa Gofu.
Anasema " siogopi kujaribu na kushindwa "huu ndiyo mtindo wa maisha
yake. Akiongea na vijana huwa anafurahisha sana. Anatengeneza mwelekeo na
maisha yenye thamani na ushauri kwa vijana. Anasema kuishi kwenye familia maskini
ni mbaya sana kuliko kutokuwa na miguu.
Nick anasema nataka watu wasiogope. Siyo
vile ulivyo kwa nje lakini vile ulivyoumbwa kuwa ndicho kitu cha msingi kwenye
maisha."Umetunikiwa, una kipaji na mambo mengi ambayo yako ndani
yako"
Nilioa. Mke wangu Kanae ni chotara
(Mjapani-mmarekani ) na nilikutana nae kwenye Tax. Ilikuwa ni mara ya kwanza
napenda.Tulimshukuru Mungu kwa kukutana. Tulienda taratibu bila yeye kuacha
masomo aliyokuwa akisoma.
Miezi mitatu baadae mwaka 2011 tukiwa
katika mahusiano nilipata shida binafsi. Nilienda kuanzisha biashara na biashara
hiyo haikuweza kusonga mbele .Niliibiwa pia fedha niliyokuwa nayo. Niliwaomba
wazazi wangu fedha kwa kuwa nilikuwa nimeibiwa na sikuamini kuwa katika umri wa
miaka 28 ningekuwa mzigo tena kwa wazazi wangu. Nililia sana.
Sikuamini kuwa Kanae Angeendelea
Kunipenda na kubaki nami. Alisema " ni sawa tu mume wangu ,siwezi kwenda
kokote .nitatafuta kazi ya uuguzi (nursing) .Hapa ndipo nilipoamini kuwa kweli
Kanae alikuwa mke wangu.
Miezi tisa baadae nilimvisha pete ya
uchumba. Na baada ya mwaka mmoja tulioana na Kiyoshi mtoto wetu akazaliwa. Yeye
ananifika kwenye mabega na huwa tunakumbatiana na kubusiana kila siku.
Nawaambia watu wasikate tamaa. huwa
tunasubiri miujiza kutokea katika maisha yetu lakini muujiza hauji
kamwe. Natamani vitu vingi vingebadilika katika maisha yangu . Nikijua kuwa mimi
naweza kuwa chanzo cha muujiza kwa mwingine naishi maisha yenye tija na yenye
kusudi.
Nick anamaliza kwa kusema "Wote
tuna hofu. Mimi siyo zaidi. Lakini jikubali na fuata kile kilicho cha muhimu na
maana katika maisha yako."