THAMANI YAKO INAVYOKUFANYA UISHI MAISHA YENYE MAANA

Thamani yako(your values)+Uwezo wako(your core strength)+Kiu yako(Your Passion)+ huduma yako(your service )=Kusudi lako=Maisha yenye maana



1. THAMANI YAKO INAVYOKUFANYA UISHI MAISHA           YENYE MAANA

Tunapozaliwa tunakuwa na thamani sawa .Kadri tunavyokua thamani yetu hupanda au kushuka .

Maisha yetu ni kama bidhaa ambayo huweza kupandishwa thamani au kushushwa.

Binadamu ndo kiumbe pekee chenye uwezo wa kujiongezea thamani au kujishusha thamani .

Ili maisha yako yawe ya thamani unapaswa kujiona wewe kama bidhaa iliyoko sokoni tayari kwa kuuzwa.Bidhaa hufutwa vumbi ,huwekwa vizuri kwenye mifuko mizuri n.k ili uvutie wateja na iweze kununulika kwa haraka sana .

Jiulize mahali ulipo thamani yako ikoje ,je kwenye familia yako usipokuwepo wanajisikiaje au ndo ile wanasema bora kaondoka .

Mshahara unaolipwa pengine ni kwa sababu hujajua thamani yako au umeridhika kwa sababu ukiondoka kampuni itafurahi kuondoka kwako maana hakuna jipya unaloongeza .

Je mtaani kwako/shuleni kwako/chuoni kwako watu wasipokuona wanajisikiaje ???

Thamani yako hupimwa katika baadhi ya maeneo yafuatayo :
·       Unavaa mavazi ya aina gani??
·       Unaongea vitu gani ??
·       Unaishi na watu gani ??
·       Una mawazo ya aina gani?
·       Una wasiliana namna gani??
·       Nidhamu binafsi
·       Uwezo wa kujisimamia mwenyewe
·       Ufanyaji kazi kwa bidii

Kama ilivyo thamani ya bidhaa kuongezeka hata wewe unaweza kujiongezea thamani kwa kufanya yafuatayo kinyume chake utakuwa ukishusha thamani yako kila sekunde .

     · Ongeza thamani kwa Kumuomba Mungu akupe Hekima kutoka kwake
   ·  Ongeza thamani yako kwa kusoma vitabu vizuri na kupata maarifa
      · Ongeza thamani yako kwa kukaa na watu wenye thamani kubwa juu yako na wanaojitambua
     · Ongeza thamani kwa kuangalia TV zinazongeza thamani katika maisha yako .Piga chini TV na vipindi vibovu maana siyo lazima uone kila kinachopita machoni pako
      ·   Jifunze namna ya kuwasiliana
      ·   Jifunze kujisimamia  n.k

FAIDA YA KUWA NA THAMANI ENEO ULIPO

· Utapendwa na watu wengi utachukiwa na wachache maana kuna watu kazi yao ni kuwachukia wengine
·  Utakuwa jasiri kuwashauri na kuwafundisha wengine
·  Hutanyanyaswa kazini kwako na sehemu yoyote
·  Utaheshimika na watu haijalishi una kipato gani au ukoje
·  Uzao wako utaheshimika



HASARA YA KUTOKUWA NA THAMANI ENEO ULIPO
·   Utadharaulika
·   Utaanza kujichukia mwenyewe
·   Utaanza kunungunika na Kumkosea Mungu