THAMANI ya kitu ipo ndani ya kitu chenyewe, yaani
kwa mfano THAMANI ya fedha ipo KATIKA fedha yenyewe.SASA basi, unapoyaendea maono yako ni wazi umeona THAMANI iliyondani ya maono hayo japo
inawezekana wengine hawawezi kujua.
Kumbuka maono yanakuwa ndani yako kwa hiyo usimshangae
anayekupinga au anaona unapoteza muda.
1. Hajui asili ya maono yako kabisa.
2. THAMANI ya maono uliyo nayo si rahisi kila mtu
kuyajua.
3. Mwanzo na mwisho Wa maono mwingine haujui kabisa hivyo
kupingwa ni jambo la kawaida kwa mtu aliyebeba maono.
MUHIMU: Hapa ninaongea na kila mmoja wetu kwa
maana ninajua mtu humu ana maono ambayo ndio kusudi lake kuwepo hapa
duniani.Sasa kwa kuwa watu hawajui asili ya maono yako ujue ni wazi utapata CHANGAMOTO kubwa sana.
Siku moja
nikiwa mtoto niliwahi hisi katika gari wenye raha ni abiria tu na si Dereva.
Mbona Dereva anahangaika hangaika tu wala hapumziki anabadilisha badilisha tu
gia kila wakati, kwa kweli niliona hana raha kabisa.Nilikuwa ninaona kila hatua
anayoiendea anabadili gia tena akifika katika miinuko miinuko ndio anabadili
mara kwa mara.
Nilipokua mkubwa nikagundua yafuatayo.
Safari ya Dereva inaendana na maono. Sisi kama abiria
tunaweza kulala kwa kuwa tuko na mbeba maono, lakini Dereva kwa kuwa ndiye
mbeba maono hawezi kulala hata kidogo na ukiona ameanza kusinzia sinzia ujue
ajali inakaribia.Sasa tega sikio kama mbeba maono kwa kuwa umekwisha kuona
mwisho wa maono yako unaanza kukutana na upinzani.Kuna upinzani wa nje na upinzani wa ndani.
1. Upinzani wa ndani ni ile hali ya NAFSI yako mwenyewe hasa kwa kuona
ni kama unataka kushindwa au kukata tamaa vile.
2. Upinzani
wa nje huambatana na mazingira na watu wanaokuzunguka wewe. Wengine wanaweza
kuwa na mtazamo hasi na unachokifanya Lakini kwa kuwa unaasili ya maono ndani
yako kuna NGUVU akupazo MUNGU aliyeweka maono ndani yako kiasi cha kutoka
kwenye hali ya raha na kuanza kukabili CHANGAMOTO, na wakati mwingine utaona
hata watu wa karibu wanakushambulia. Pia unashindwa kuelewa kabisa. Msukumo wa
ndani ya nafsi yako unaweza ukawa pengine chini na watu wa nje wakiongeza
unaweza ukaona kama hutofika katika maono yako.
Lakini kwa kuwa unaasili ya maono ndani yako kuna NGUVU
akupazo MUNGU aliyeweka maono ndani yako kiasi cha kutoka kwenye hali ya raha
na kuanza kukabili CHANGAMOTO, na wakati mwingine utaona hata watu Wa karibu
wanakushambulia pia na hata unashindwa kuelewa kabisa.
Kwa kuwa wewe tu ndio unayajua adui wa aina yoyote ile,
ataanza na wewe kwanza na si mwingine, lakini ile hamu ya kuyatimiza na kufika
mwisho itakupa nguvu za ajabu kuelekea ushindi mkubwa wa maono yako.
Maeneo
matatu unayopatia NGUVU
Ni MUNGU mwenyewe kwa
kuwa ameianzisha kazi na anataka uitimize katika mapenzi yake.Msukumo chanya
uliopo ndani yako unaolenga wewe kufanikiwa juu ya maono hayo. Watu uliopewa
kukusaidia katika maono yako watatumika kukuinua.KUMBUKA: SHUJAA BILA VITA SI SHUJAA
Na unapopitia CHANGAMOTO ili kunolewa vizuri kuelekea
mafanikio yaliyo mbele yako MUNGU atakupa tumaini na Amani mpaka ufike mwisho
Wa maono yako.
Kwa hypo
hayo ni maeneo muhimu sana ambayo hukupa nguvu sana kuelekea maono yako.
1. Jenga uhusiano mzuri na MUNGU akupaye maono.
2. Uwe na Uwezo Wa kugeuza hasi kuwa chanya nyakati zote,
haijalishi mazingira yakoje.
3. Tunza urafiki na watu wote na zaidi wale uliopewa
mtimize maono pamoja.
Kwa hiyo hayo ni maeneo muhimu sana ambayo hukupa NGUVU
KUELEKEA maono yako.
Ahsanteni
sana,
Adabert
Chenche
0712
957528