Hebu kama wewe ulisoma shule ya msingi
enzi zile za Nyerere, Mwinyi au Mkapa tujikumbushe hadithi hii ambayo ina funzo
kubwa sina uhakika wa enzi za Kikwete na
sasa Maghufuli kama hadithi hii inasomwa .Hadithi hii ni ile ya *Nani atamfunga
Paka Kengele???* .Twende wote hapa chini na ujifunze kitu .
"Kulikuwa na duka Kubwa la Vyakula
na Vinywaji katika mji. Panya Wengi waliishi katika duka hilo la vyakula na vinywaji. Chakula
kilikuwa ni kingi sana kwa ajili yao. Walikula kila kitu na kuharibu mifuko
yote ya vyakula. Waliharibu pia mikate, biskuti na matunda ya duka.
Mwenye duka alishikwa na wasiwasi kweli.
Hivyo, yeye alipata wazo "mimi lazima ninunue paka na atakaa humu ndani ya
hili duka. Kufanya hivo naweza kuokoa mambo yangu."
Alimnunua Paka mmoja mzuri, mkubwa na
kisha kumwacha pale. Paka alikuwa na wakati mzuri wa kuwinda panya na kuwaua.
Panya hawakuweza kuzunguka kwa uhuru sasa. Waliogopa kwamba wakati wowote paka
ange wakamata na kuwala.
Panya walitaka kufanya kitu fulani.
Wakaitisha mkutano na wote wakasema "Ni lazima kujikwamua na paka. Je,
kuna mtu ana maoni?"
Panya wote wameketi na kuogopa. panya
mmoja mwelevu alisimama na akasema, "paka hutembea kwa upole. Hilo ni
tatizo. Kama tunaweza kumfunga kengele kwenye shingo yake, basi mambo yatakuwa
mazuri. Tunaweza kujua harakati zake
zote ".
"Ndiyo, hilo ni jibu sahihi,"
walisema panya wote. panya wa miaka mingi alisimama polepole na akauliza,
"Ni Nani atakaye Mfunga paka kengele? " Baada ya muda mchache
hakukuwa na yeyote wa kujibu swali hili.:"
Angalia wakati huyu Mwenye duka akiwa na
mawazo ya kutatua tatizo ili aendelee na biashara yake kumbe adui yake mkubwa
naye amejipanga asikamilishe azima yake .
*FUNZO*
_Wakati unapoingiwa na wazo la kufanya
jambo fulani mazingira yanayokuzunguka huja na vipangamizi vya kutofanikisha
mambo yako .Mazingira hayo yanaweza kuwa ni watu wasiotaka uendelee na
kukurudisha nyuma .
Wakati unatafuta kukamilisha ndoto zako
na malengo yako wapo watu watakaa kikao kwa pamoja na kukufanya usifanikishe
ndoto yako .Watatafuta mbinu za kukufunga kengele .Kengele ni maneno
utakayoambiwa kuhusu kile unachowaza kukifanya
na ukiyasikiliza utavunjika moyo sana na hutasonga mbele.
Wakati naendelea kuandika ghafla hapa nakumbuka
hadithi ya Yusufu kwa wale Wakristo akitajwa kuwa moja ya watu na ndoto kubwa za kufanikiwa
lakini ndugu zake nao wakaa kikao kama walivyokaa panya ili Wamwangamize Yusufu
.Nadhani Unakumbuka ilifika hatua akauzwa na hapa ni baada ya pona pona ya
Kuchinjwa na ndugu zake wa Damu.Usingekuwa moyo dhabiti wa Yusufu asingeweza
kufanikisha ndoto zake /
Daima siyo kitu rahisi kufanikisha kile
unachowaza .Unapaswa kujua hata mazingira yamejipanga vizuri kabisa kuhakikisha
kwamba hufanikishi kile ambacho umekipanga .Hivyo ili kukifikia lengo inahitaji
ujenge uwezo mkubwa wa kuzalisha njia mbadala wa kulikabili Tatizo au
Changamoto unayopitia_