Ndoto ni nini?
Ndoto ambayo tunakwenda kuizungumzia sio ndoto unayoota ukiwa umelala. Ni ndoto ya mchana
ni kile kitu unachotamani kuja kukipata
siku moja kabla hujaondoka duniani.Ndoto inaweza kua katika makundi ya aina
mbalimbali, unaweza kua na ndoto ya kua Rais, Mwimbaji bora, Mchezaji bora,
Mwandishi Bora , Mfanyabiashara maarufu.Vile vile unaweza kua na
ndoto ya kumiliki vitu, nyumba nzuri ya kifahari sana labda ya milioni 300,
Gari la kifahari sana, Unaweza kua na ndoto ya kumiliki utajiri au kua
Bilionea.Zote hizo ni ndoto ambazo kila mmoja alikua nazo huenda ni kipindi
anakua ua hata sasa bado anayo. kwa bahati mbaya sana watu wengi wamekua na
ndoto kubwa sana wakiwa wadogo na kuzipoteza walipoanza kuingia kwenye uhalisia
wa maisha.
VITU VINAVYOWEZA KUIPOTEZA NDOTO YAKO.
1.
UGUMU WA MAISHA.
Maisha yanavyozidi kubadilika na kua magumu
ndipo baadhi ya watu huanza kuasahu vile vitu ambavyo walikua wanatamani waje kua navyo. Maisha yanapokua
magumu sana wengi huona haiwezekani tena wao kufikia ndoto zao hivyo kukata
tamaa kabisa na kuamua kua na maisha ya kawaida.Mtu anaweza kujitazama vile
alivyo na kuona yeye hafananii kabisa kuja kua Rais wa nchi hii labda kutokana
na familia aliyotokea au maisha yanayoendelea sasa hivi.Nakuomba kama unapitia
hali hiyo anza kuikataa kabisa ili usije kupotea.
2.
Marafiki wabaya.
Marafiki na watu unakua nao
mara kwa mara wanaweza kua sababu kubwa sana kukupoteza kabisa na kukufanya
wewe uache kupigania ndoto yako. Ndoto yako ni ya thamani sana ndio maana
inapata upinzani. Ndio maana uutaambiwa haiwezekani. Ndio maana watakucheka ukiwaambia
wewe unataka kua Rais wa nchi hii. Au unataka kua Bilionea. Mara zote watu
wnakuhukumu kutokana na hali uliyonayo sasa hivi. Unaweza kuachwa na Mpenzi
wako umpendaye kwa sababu tu yeye anaangalia maisha uliyonayo sasa hivi na hata
ukimueleza ndoto zako haamini kutokana na hali yako ya maisha uliyonayo sasa.
Ufanyeje?
Kaa nao mbali wale watu
ambao hawana ndoto kama za kwako. Kaa mbali na watu ambao wanafikiri kama kuku.
Yaani wao wamejiona kwamba ni maskini na haiwezekani kua tajiri labda kuiba tu.Inawezekana
ni watu wako wa karibu sana labda kaka, dada, wazazi ufanyeje? usikubali kuwasikiliza weka pamba
sikioni.Mimi kuna mtu aliniambiaga hizo ni ndoto za mchana haziwezi kutokea
kamwe lakini sijakata tamaa naendelea kufanyia kazi ndoto zangu.
UNALINDAJE NDOTO YAKO?
- IANDIKE.
Kama unasema una ndoto
lakini bado ipo kichwani bado hujaelewa maana yake.Katafute Notebook nzuri sana
ya gharama Huwezi kuandika ndoto ya kua Bilionae kwenye note book ya elfu mbili
aisee?? Tafuta notebook ya Gharama hata ya 20,000 ili uweze kuitunza vizuri.
Andika kila kitu
unachokitaka kwenye dunia hii.Hakikisha umeandika kila Kitu na usiache hata
kimoja.Hii ni njia ya kwanza ya kuilinda ndoto
yako. Nikikutana na wewe sehemu Uniambie
au unionyeshe kilipo kitabu chako cha ndoto.Andika ni Jinsi gani unaweza kupata
vile vitu. Ni ujuzi wa namna gani unahitaji ili uweze kufikia ndoto zako. Ni
watu wa namna gani unahitaji kuambatana nao ili ufanikiwe kwenye doto zako.Andika
ni Baada ya Muda gani utakua umefikia Ndoto zako sasa hapa Ni somo jingine
kabisa jinsi ya kuandika malengo. Malengo ya muda mfupi na Muda mrefu.
- SOMA NDOTO ZAKO KILA SIKU ASUBUHI NA KABLA YA KULALA.
Soma kila siku namaanisha
kila siku asubuhi na jioni.Kwanini usome kila siku ? Unaichora au unaiingiza
picha ya ndoto zako ndani ya ubongo wako hii itakufanya chochote utakachokutana
nacho kama hakiendani na ndoto yako uweze kukiepuka na kama kinaendana basi uweze kukivuta. Unaposoma
inajijenga kwenye akili yako na kutengeneza ukaribu wa wewe kuifikia zaidi. Soma
na tafakari.
- TENGA MUDA PEKE YAKO.
Hakikisha unatenga Muda wa
peke yako angalau kila wiki ukiwa peke yako sehemu ambayo haina usumbufu
wowote.Sehemu hiyo utakua unaipa akili yako nafasi ya kutafakari juu yako wewe.
Jitazame ulivyo sasa halafu jitazame wewe ukiwa umefikia kwenye ile ndoto yako.Kama
ni gari basi anza kujiona jinsi unavyoliendesha lile gari la ndoto yako.Kama ni
Rais embu jione ukiwa Ikulu basi Jione ukiongoza majeshi.Kama ni Bilionea anza
kuona ukiwa Bilionea utakavyokua. Utakavyoweza kubadilisha maisha ya watu wengi
sana Duniani.Ona jinsi dunia inavyofurahia Mungu Kukuumba wewe kwasababu maisha
yao yamebadilika.Nashauri hili ufanye angalau lisaa limoja ukiwa peke yako bila
simu wala kifaa chochote cha mawasiliano.
- SOMA VITABU NA FANYIA KAZI NDOTO YAKO KILA SIKU.
Soma vitabu ambavyo vitakuza
ufahamu wako ili wewe uweze kuifkia ndoto yako.Kama unataka kuwa Rais wa Nchi
lazima ujue kua unakwenda kuongoza watu hivyo
jua ni vitabu gani usome ile ukuze ufahamu wako.Unataka kua Bilionea
hutaweza kua bilionea na ufahamu ulionao sasa hivi mali zote zinatakiwa
ziongozwe na wewe hivyo jijengee tabia ya kujisomea vitu mbalimbali juu ya ile
ndoto yako. Ili ufikie Ubilionea unaanza
na hatua moja anza leo kupiga hatua moja moja hadi ufikie kule unakotaka.
Usikubali kabisa siku ipite ujafanya chochote juu ya Ndoto yako ni kupoteza
fursa.
Kama tunavyojua fursa ya
kwanza ni uhai tulionao leo hivyo usitumie vibaya leo siku zote unakuaga na leo
tu. Ukiweza kuipangilia leo vizuri itakufikisha kwenye ndoto yako.
- JIPONGEZE
Kwenye kila hatua unayopiga
jipongeze ili kujiongezea hamasa na wewe uweze kusonga mbele.Unaweza kujipa
zawadi ndogo ndogo ambazo hua unazipenda kila unapopiga hatua kuelekea kule
unapotaka.Iseme ndoto yako sehemu yeyote unapokua.Kwanini uiseme kwasababu una
Imani na Imani ni kua na hakika juu ya mambo yasiyoonekana.Hata Yusufu alianza
kuwaambia ndugu zake kwamba anaona ndoto anaona akiwaongoza. Walimkemea lakini
hakusita kuendelea kuwaambia. Hii itakusaidia unapokamilisha iwe ushuhuuda
kwamba huyu jamaa alituambiaga anakuja kua Rais, Bilionea, Mtu mkuu sana. Huwezi
kuitwa mchawi au Freemason kama umeanza kusema sasa hivi kwamba utajenga
Ghorofa au utamiliki BMW.Walewale wanaokukatisha Tamaa ndio watu wakuwaambia
ile ndoto yako.Hata wakikusema wewe endelea kuisema.Unapoisema inakupa ujasiri
wa kuendelea mbele bila kukata tamaa.