KATAA KUFA BILA KUTIMIZA NDOTO YAKO ~Joas Yunus

          

Katika kitu kibaya sana duniani ni kitendo cha mtu kufa na ndoto ambayo haijitimizwa na huku akiwa alikuwa na kila sababu ya Kutimiza ndoto zake .

Thomas Edson angekufa na ndoto yake leo hii tusingeshuhudia umeme ukiwaka na duniani pasingekuwa sehemu nzuri ya kuishi bila kuwa na umeme.Lakini ni Jitihada za mtu mmoja ambaye inasemekana alishindwa mara 1000 lakini hakukata tamaa na mwisho ndoto yake ikatimia .Leo ndoto ya Thomas Edson imeajiri wengi sana na uzalishaji unafanyika kwa kiwango cha juu kupitia ndoto yake .

Huna sababu ya Kufa na ndoto yako kwa sababu ulishawahi sikia historia ya Yusufu nanmna ambavyo alikuwa na ndoto kubwa lakini ndoto yake ikiwa na vipangamizi vingi sana kuanzia kwenye familia yake.Haikuwa rahisi kwake lakini hakukubali mazingira yaue ndoto zake .Tunashuhudia Yusufu anawaokoa ndugu zake ambao walitaka kuua ndoto yake.

Ukifa na ndoto yako maana yake kuna watu  utasababisha wawe na maisha magumu maana walitegemea wewe utimize ndoto yako waweze kuwa na unafuu wa maisha.Ni watu ambao wameandaliwa kufanya kazi chini yako ,utengeneza Maisha hatma ya maisha yao.

Nyuma yako liko kundi kubwa ambalo lina maisha magumu sana .Wanasubiri uanzishe ile kampuni uliyosema unaanzisha lakini hujaanzisha ,wanasubiri ile shule uliyosema unaanzisha lakini mpaka sasa hujaanzisha wanasubiri uanzishe ile supermarket ambayo iko kwenye mpango mkakati wako tokea mwaka juzi lakini bado hujaanzisha.

Nasikitika kukwambia kuw umekuwa chanzo cha ukosefu wa ajira nchini kwa sababu hujatimiza ndoto yako .Angalia ndugu yule anvyohangaika pengine wewe ndiwe mwajiri wake .Machozi yake yako juu yako .Angalia anataka kujiua na achome vyeti vyake kwa sababu yako inauma sana .

Rafiki yangu Michael Mathias Uhahula Mkurugenzi wa Asasi ya Mafanikio  Foundation yenye makao makuu kule mkoani njombe alitambua siri ya kutokufa na Ndoto yake na kupitia ndoto yake ya kuwasaidia watu kuwekeza  katika Mashamba na Misitu ameweza kuajiri vijana miambili(200) wa Kitanzania .Kijana huyu mwenye umri  mdogo wa miaka 27 sasa amefanya mambo makubwa sana na ameokoa maisha ya watanzania wengi sana  kupitia wazo alilokuwa nalo .

Sielewi kwanini hujatimiza ndoto zako wakati hata wewe hapo ulipo unafanyia kazi ndoto ya mtu .Beba mzigo wako ,Jifungue ndoto yako maana iko tayari.Unataka watu wakukumbuke kwa jambo gani uliloliacha Duniani kama hutaki kutimiza ndoto yako ???