UWEKEZAJI WA MUDA MREFU ~ Joas




Maana ya uwekezaji :
Uwekezaji ni kitendo cha kuingiza fedha kwenye mradi fulani kwa ajili ya kujipatia faida ama ya muda mfupi au muda mrefu

Hakuna mwekezaji anayewekeza kwa ajili ya kupata hasara kama yupo itabidi tumpeleke Milembe akipimwe akili

KWANINI UWEKEZE ????

·  Ajira yako  si salama ,unaweza kuipoteza muda wowote na maisha yakawa magumu sana.Kama ukiachishwa kazi leo na hujawekeza kuna uwezekano ukawa na msongo mkubwa wa mawazo na mara nyingi watu hufa mapema

·        Faida ya vizazi vyako
Unaweza usifaidi sana uwekezaji wako kwa sasa lakini kizazi chako kikaishi maisha ya furaha kwa sababu uliwekeza vizuri
Miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na kasi na ongezeko la watu wengi wanaotaka kuwekeza .Hata hivyo watu wengi hupenda kuwekeza katika vitu ambavyo pay back period yake ni ndogo yaani wanapenda kuwekeza na kupata faida haraka sana .Watu wamewekeza kwenye maduka ,supermarkets n,k ambavyo wana uhakika wa kupata hela kwa muda mrefu

Hata hivyo uwekezaji wenye faida kubwa ni uwekezaji wa muda mrefu .katika uwekezaji huu mtu huweza kusubiri kwa zaidi ya miaka mitano ili kuona matunda .Hata hivyo watu wengi kwa sababu ya kutokuwa wavumilivu wanashindwa kufanya uwekezaji huu .
  

BAADHI YA UWEKEZAJI WA MUDA MREFU NI KAMA UFUATAO :

  •      UWEKEZAJI KATIKA MUNGU

Kuwekeza katika Mungu ndicho kitu cha msingi kabisa katika uwekezaji wa aina yoyote .Pasipo Mungu hatuwezi chochote na tukiwa na Mungu tunayaweza mambo yote katika yeye atutiaye Nguvu hivyo tunapaswa kuwekeza muda na pesa zetu kwa Mungu sambamba na vipawa na karama tulizopewa .

  •  UWEKEZAJI KATIKA MAARIFA 

Najua unaweza usinielewe lakini ukweli ni kwamba huu ndio uwekezaji ambao utakulipa sana kama utaamua kuwekeza kwayo.Wekeza sana katika maarifa kwa gharama yoyote maana bila maarifa hata hiyo miradi unayowekeza itakushinda kuendesha maana utakuwa na maarifa duni .

  •  UWEKEZAJI KATIKA WATU

Watu wengi hawajui kuwa watu ni mali na watu ni fedha pia .Sikia bila watu hakuna fedha na fedha huletwa na watu .Sasa kama fedha ziko kwa watu ,kwanini usiwekeze kwa watu .
Siri hii wanaijua watu wachache sana wenye maarifa na wale wanaoijua ndio wanaofaidi matunda .

Uwekezaji kwa watu unahitaji kujitoa sana kwa ajili ya wengine lakini in long run watu hao hao watakulipa maradufu kama utajua namna ya kuwatumia na kubuni huduma zako ambazo kama umewekeza kwao lazima wafuate huduma yako kokote ulipo .

  • UWEKEZAJI KATIKA ARDHI NA MASHAMBA

Huu pia ni uwekezaji wa muda mrefu ambao hulipa sana japo kwa muda mrefu .Yapo mashamba mikoani yanapatikana kwa bei rahisi ni vizuri kuyakimbilia na kuanza kuwekeza katika ardhi .Faida ya uwekezaji katika ardhi ni kuwa unaweza kuanza mradi kama kilimo na ufugaji au kilimo cha miti na ukajipatia pesa .Shida watu hawataki kutoka mjini kwenda mikoa ya nje ambayo ardhi hupatikana kwa bei rahisi na huko unaweza kufanya mambo mengi kwa kutumia kiasi kidogo tofauti na mji wa dar es salaam ambapo kwa sasa ardhi imekuwa gharama sana .

_Rafiki yangu Michael UHAHULA yeye baada ya kumaliza Chuo kikuu cha Dar es saalam alipata wazo la kuwekeza kwao Njombe baada ya kuona kuna mashamba mengi ambayo hayana kitu na yana rutuba nzuri _

_Wakati huo akiwa amemaliza mwaka 2014 ,Michael hakuwa na fedha kama inavyokuwa pale mtu anavyokuwa amaemaliza chuo lakini kwa kuwa alikuwa na wazo alihaha kutafuta mtaji huku akiwa anawashirikisha watu wazo lake lakini wengi walimbeza_

_Michael hatimaye alikutana na wazungu na mara baada ya kuwasimulia ardhi iliyoko mkoani Njombe kuwa haina watu na ni nzuri kwa mambo mbalimbali ,wazungu hao walimsaidia kiasi kikubwa cha fedha ambacho Michael alisajiri asasi yake iitwayo Mafanikio Foundation na sasa akiwa ameajiri vijana 200 wanaofanya kazi za mashamba_

_Asasi hii ya ndugu Michael inajihusisha na kumuuzia shamba mtu yeyote ,na kumtafutia hati miliki pamoja na kumpandia mtu huyo mnunuzi wa shamba miti ya mbao na nguzo kwa bei ndogo sana na shamba hilo linasimamiwa mpaka uvunaji_

Hii ni fursa kwako kama ulikuwa hujaisikia na tayari Michael anapata kiasi kikubwa cha fedha kupitia wazo lake la uwekezaji kwenye Mashamba