Habari Ndugu
Msomaji wa makala hii!
Twiga ndiye mnyama aliye na shingo ndefu
sana na mwenye uwezo wa kulisha kwenye majani marefu sana kuliko wanyama wengine .Hii inamanisha kuwa twiga
ana uwezo wa kulisha majani ayatakayo yawe ya juu au chini na hii humfanya
ajihakikishie chakula chake hasa kipindi kigumu cha ukosefu wa chakula.
Hata hivyo twiga inasemekana hapo awali
hakuwa na shingo ndefu (As far as organic evolution is concerned) lakini
kilichomfanya awe na shingo ndefu ni namna twiga alivyokuwa akipenda kulisha
majani yaliyoko juu sana na kadri shingo lilivyozidi kutumika kurisha majani ya
juu ndo lilivyoongezeka .
Biolojia inasema katika organic evolution
uliyosoma kuwa kadri kitu kinavyozidi kutumika huwa kinaongezeka na kama kitu
hakitumiki huwa kinapotea .(Law of use and disuse).
Hii inatufundisha kuwa tunaweza kuamua
kuwa vyovyote tunavyotaka kuwa kama tukitumia vile tulivyonavyo(you can be
whoever you wanna be).Shida inayosababisha usiwe vile unavyotaka ni uvivu na
kukata tamaa mapema.
Twiga anatufundisha kuwa watu
wanaofanikiwa ni wale wanaotumia walivyonavyo huku wakizishinda changamoto
ambazo zinazuia kuwa vile wanavyotaka kuwa.
Ukweli ni kwamba kama hutumii ulivyo
navyo vitapotea au kuwa butu kama kisu
kisichotumika .
- Kama hutumii kipaji ,kitapotea
- Kama hutumii akili ulizopewa na Mungu Maisha yako hayatabadilika
- Kama hutumii fursa utakuwa maskini