KUTHUBUTHU ILI UPATE MUUJIZA ~ADABERT CHENCHE


Kawaida MTU hupata muujiza akiwa ameandaa mazingira ya kupata. MUNGU hapendi kabisa uvivu, na ikiwa MTU amekaa tu akisubiri muujiza ni ngumu sana.

_Katika watu wawili mmoja aliyebebewa mzigo toka ulipokuwa mpaka unaopoenda, MTU huyu amebebewa wala hajahusika kubeba kabisa ni wazi kuwa:_

  • Hajui uzito Wa ule mzigo hata kidogo kwa hiyo ukiona hathamini ule msaada usishangae.
  • Kwa kuwa hajui uzito hata THAMANI ya ule mzigo inawezekana hajui kabisa.
  • Kiasi cha upendo alichotendewa kubebewa inawezekana akaona cha kawaida tu kwa kuwa hakubeba Bali alibebewa.

SASA TUJE HAPA TAFAKURI NA  FUNDISHO

Ukijitahidi kubeba ule mzigo kutoka eneo moja kwenda la pili na karibu kumaliza halafu ukasaidiwa mpaka kumaliza ni hivi:

  • Ule uzito Wa mzigo wewe unauelewa hivyo utauthamini.
  • Upendo utakua kwani utajua uzito niliobeba na maumivu niliyokuwa nayapata yamebebwa na aliyenisaidia.
  • Ni rahisi sana kumjali aliyekubebea na kukufikishia.

Hivyo hivyo Mwanafunzi aliyeoneshwa majawabu bila kusoma na akafaulu inawezekana asijiamini na kuthamini, ni tofauti na mwanafunzi aliyesoma kwa bidii hatimaye akafaulu huyu atathamini na kujali sana.



*USIKAE KUNGOJA MIUJIZA FANYA ENEO LAKO HALAFU BWANA AMALIZIE.*