CHANGAMOTO
YA MASOKO NA JINSI YA KUJENGA MVUTO WA SOKO
~
Rwihula Daniel. 0657267074
Naitwa Rwihula Daniel
1.Ni
mjasiriamali kwa fikra na vitendo.
2. Ni mkurugenzi wa Kampuni yangu binafsi ya
Kibiashara Ijulikanayo kama Joint Professionals Co. Ltd
3.Ni meneja Mahusihano na Masoko wa Mtandao wa
Kijani Kibichi Tanzania
4. Ni mwanadiplomasia Kijana.
5.Ni mwanaharakati wa Maendeleleo ya Vijana
6.Ni mwalimu wa Ujasiriamali.
Watu wengi wanalalamika kuwa hawana masoko ya bidhaa
zao na hiki kimekuwa kilio cha watu Wengi sana.Changamoto ya Masoko imewafanya
watu wakate tamaa na biashara au ujasiriamali.Soko siyo changamoto kama wengi
wanavyotazama.
Hakuna chakula kisichokuwa na soko au walaji.
Wakulima wa Tanzania wanalima na wanafuga lakini hawana Masoko ati wakati pale
Congo, Comoro, Sudani,Somalia wanahtaji vyakula kwa wingi.
Leo naomba niwambie kinachosababisha changamoto ya
MASOKO NCHINI.
1.UBINAFSI(UMIMI)
2.UKOSEFU
WA NIDHAMU YA KUHUDUMIA SOKO
3.KUTOJIAMINI
4.UKOSEFU
WA TAARIFA SAHIHI
5.UZALISHAJI
HAFIFU
1.UBINAFSI
Hii ni sababu kuu inayopelekea kuwepo kwa changamoto
ya Masoko.
Wajasiriamali wengi wana ubinafsi yaan MTU anajua
soko lakini hana uwezo wa kulihudumia lakini hawezi kumwambia Mwenzie,
Katika tafiti kupiti Kijani Kibichi Tanzania tumegundua
kuna masoko Mengi ambayo yanahtaji supply lakini bahati mbaya Watanzania hawana
uwezo wa Kusuplly soko kutokana na kwamba uwezo wa Uzalishaji ni mdogo kwani
kila mtu anazalisha kivyake na kibinafsi.
Watanzania wajasiriamali wanaogopa kuonyeshana fursa
za Masoko kisa yeye atakosa wateja. Hata kama soko linamzidi uwezo uwezo yeye Hawezi kumshirikisha mwenzie Bali atakaa
anamzungusha mtejaa na baadae mteja anamwona mbabahishaji anamkimbia.
Mfano mtu anapata tenda supermarket wakati labda uwezo bado
haujawa wa kutosha. Atapeleka wiki moja afu anaishiwa mzigo, sasa badala ya kumshilikisha mwenzie mkulima au mfugaji yeye ataanza Udalali na
badae kuchakachua .Na hapo mteja akijua anafuta tenda yako.
Wakati ungepata Tenda ukawashirikisha wenzio
mkajiunga kikundi au umoja wa kuhudumia solo basi mngefika mbali. Ila coz ya
Ubinafsi wenzako watakosa soko na wewe utakosa soko. Ndo maana leo Tunalia na
Masoko.
2.UKOSEFU
WA NIDHAMU YA KUHUDUMIA SOKO.
Katika anga za Kimataifa na anga LA kitaifa watu
wengi hawapendi kufanya biashara na Watanzania cozi wanasema Watanzania ni
wasumbufu kwenye biashara.Yaani MTU anapewa tender, kuwa alete mzigo mda
fulani, kiasi Fulani na kwa ubora Fulani yeye anafanya kinyume. Umemwambia
alete mzigo saaa tatu asubuh atakuletea SAA Tisa na SABABU lukuki au analeta
kesho yake.Hapo
samahan za kutosha.Na mwingine unamwambia lete kiasi fulan mfano trei 1000
anasema sawa naleta akifikisha mzigo anakuonyesha trei 50 na sababu Kibaooo.Unajielewa kweli?? kwa nini hukumwambia hiyo tenda
huiwezi na umwambie uwezo wa oda yako ??.
Huyu ndiye balaa
sasa yeye anajiita Mbongo orijino au mjanja. Anaambiwa alete tani moja yeye
kila gunia anapunguza kilo moja akijua si watashusha na kuweka chini kumbe
jamaa wanapima kila gunia bana. Sasa wanamaliza kupima wanagundua kilo kibao
hazipo kweli unajielewa wewe unachokifanya.
Hiyo yote ni Kukosa nidhamu ya Kuhudumia soko. Alafu
tukikosa soko tunalalama MASOKO HAYAPOOO .Toka Lini chakula kikakosa soko au walaji wewe .Nidhamu mbaya ya kuhudumia solo
imewafanya Wakenya, WAARABU NA WAHINDI wachukue SOKO LETU SISI uku tunalia na
soko.Kama unataka soko JENGA NIDHAMU NZURI YA KUHUDUMIA SOKO.
3. KUTOJIAMINI.
Wajasiriamali wengi wa Tanzania hawajiamini.Yaan MTU
bidhaa ni yake lakini hana uwezo wa kuielezea vizuri au kuiuza sokoni afu
anasema SOKO HAKUNA.
Unakuta MTU
anauza kitu cha kawaida sana lakini bwana anavyojieleza na kueleza bidhaa
yake ni kama hajawah nunua akatumia.
Mfano Mimi nafundisha na kuhamasisha ufugaji Mende
kibiashara ila nikikuuzia wazo hili utalinunua tu. Juzi saba saba nimemuuzia
wazo hili Mtanzania mmoja mwenye dola zake yaani ata leo anataka anipe milioni
10 tufanye huu mradi.Wewe una tikiti, tango, nyanya ambazo Wabongo wanakula
alafu unasema Huna SOKOOOO.Mimi MENDE nauza we
nyanya huna soko.Kama huamini niletee Mende kg 1 nikuuzie tena
kwa Mtanzania.
4.BIDHAAA HAFIFU.
Wajasiriamali wengi nchini wana bidha zisizokuwa
na ubora. Wengi wanazalisha bidhaa
pasipo kuwa na hata MAARIFA kidogo ya kuzalisha bidha.Mfano MTU anafuga kuku wa
Nyama walioletwa wakiwa na umri mmoja na kg sawa lakini wakati wa kuuza Mara
huyu ana uzito robo, yule nusu na yule kg 1. Yaani haileweki.Lakini kwa
mjasiriamali anayejielewe utakuta kukua wana umbo sawa, Uzito saws na bei sawa.
Sasa unakuta Mtu anaenda Nakumati kutafuta Soko alafu anaambiwa leta sampo, kwanza anataka sampo yenyewe alipwe.Sampo
hiyo sasa kuku huyu robo yule nusu yule nusu ya robo.halafu eti huyu anatafuta
SOKO .Nani atakupa soko lake??
Wateja wanataka bidhaa zenye ubora na zenye viwango.
Yaan paja LA kuku huyu na huyu vifanane. Ukiambiwa lete kuku wa kg 2 wooote wawe
kilo 2. Weka package nzuri.Maana wengine wanajifanya wachaga sana. Eti anaweka
KIFUNGASHIO cha kawaida ila asipunguze faida kumbe ndo anajifukuza sokoni.
WAPENDWA
MKITAKA MASOKO YAPO MENGI TU SEMA HAMYAONI KWA KUWA MNAPINGANA NA MAHITAJI YA
SOKO
Hii imewafanya Wakenya, Wanyarwanda,
Wamalawi,Wasouth Africa kulifaidi SOKO letu wakati sisi tunalia na Masoko.Ukitaka soko TENGENEZA MVUTO WA SOKO BWANA🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓
JINSI YA KUTENGENESLZA MVUTO WA SOKO.
Mvuto wa soko ndio unamfanya mteja aje kununua kwako
na si kwa mwingine.
Huitaji kuangaika au kulilia SOKO. SOKO LIPO NA LITAENDELEA KUWEPO MILELE.
WEWE hangaika sana kutengeneza Mvuto wa Soko.Na hii
ndo MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANI tunashughulika nacho Kwa wanachama wetu
haswaaa yaani KUWATENGENEZEA MVUTO WA SOKO. ndo maana uku ukiwa na MENDE, soko
unapata FUNZA soko unapata,UYOGA soko unapata,MCHAICHAI soko unapata na ndo maana
tunasema HAPA CHANYA TUUU.HIVYO ukitaka MASOKO WEWE weka nguvu kubwa katika
Kujenga mvuto wa Soko LA bidhaa zako.
JINSI YA KUJENGA MVUTO WA SOKO.
- Jenga NGUVU ya kuhudumia soko kwa Umoja ili kuondoa Ubinafsi.
- JENGA KUJIAMINI
- STAWISHA UBORA WA BIDHAA YAKO AU ONGEZA THAMANI KWA BIDHAA ZAKO.
- JENGA NIDHAMU THABITI YA KUHESHIMU NA KUTHAMINI SOKO.
- Jamani Masoko ni makubwa sana ni sisi kujiweka vyema ili tuingie katika mfumo rasmi wa Biashara au ujasiriamali.
KWA
USHAURI NA MAFUNZO PIGA 0657 267074.
KARIBU SANA KATIKA MTANDAO MPANA WA KIJANI KIBICHI
SULUHISHO LA MASOKO NA UMASIKINI TANZANIA.