Baadhi ya Magonjwa yaliyopuuzwa ~DR ADILI AMENYE





Magonjwa yaliyopuuzwa(Neglected Tropical Diseases) haya ni magonjwa ambayo madhara yake hayaonekani sana au watu wachache ndo huyapata hivyo kuonekana kama sio tatizo .Magonjwa hayo huathiri maisha ya watu wengi na wengine kupoteza maisha .


Mfano Wa magonjwa hayo ni kama kichocho, matende, mabusha, trakoma, ugonjwa Wa kulala lala, upofu, dengu,chikungunya( huu wamakonde wanaujua sana) n.k.Naanza na Minyoo

Minyoo ipo ya aina mbali mbali,kama ascaris na hookworm!! Ipo ardhini na huishi kwa muda mrefu sana,wstu hupata kwa kula udongo,mboga za majani,kula kinyesi n.k.

Watu huishi nayo wengine bila shida yoyote,ila wanaweza kupata usumbufu kama kuwasha makalio,anus,tumbo kujaa sana,kula sana  Ila wakati mwingi minyoo huziba utumbo na kusababisha madhara makubwa na operation hufanyika kuondoa hiyo minyoo. Wengine hutoka puani au kwenye choo.

Wamama wajawazito wengi hukutwa nayo kipindi wanafanya cliniki,na hupewa dawa kama tiba au kinga, wengine hupata maybe kukitokea chanjo za kitaifa za magonjwa haya Ni vizur kuchukua walau Mara mbili kwa mwaka.

Ugonjwa mwingine unsitwa RIVER BLINDNESS usababisha upofu na magonjwa ya ngozi, hasa kwa watu wanaoishi jirani na mito inayokwenda kasi!! Kyela na tukuyu ni moja ya maendo yenye ugonjwa huu sana!! Nigeria ugonjwa huu uliamisha kijiji baada ya wakazi wengi kupsta upofu hadi pale walipofanya fumigation kuua mbuu waliokuwa wanaenez ugonjwa huu.

Ugonjwa mwingine ni dengue na chikungunya.Haya yapo kundi moja na Ebola Sema kuua ni Mara chache, chikungunya uligundulika Tanzania na ni jina LA kimskonde, kujikunja sababu ya maumivu.

Ugonjwa mwingine ni mabusha na matende .Waweza pata minyoo ya magonjwa haya na ukaishi nayo miaka kibao bila kuugua,ila yanatibika kirahisi sana na kupona kma yatagundulika mapema.

Ugonjwa Wa kichocho, unathiri mfumo Wa chskula na mkojo, usipotibiwa unaharifu figo,maini na kuleta Kansa ya kibofu cha mkojo.

Trachoma unaambukizwa na nzi na tanzania upo sana Dodoma,usababisha upofu ingawa kinga kubwa ni usafi Wa macho na ukiwa Tiba unatibika na kupona

Ugonjwa mwingine ni ukoma,huu unaathiri ngozi,mishipa ya fahamu na viungo, ukigundulika mapema unatibika bila kuharibu viungo,ila ukichelewa unaaharibu viungo,ngozi na mishipa ya fahamu sanaaa
African sleeping sickness kwa kiswahili sijui wanahuitaje,dalili zake  ni kama za malaria sema kingine ni kulalalala sana na huu unaua,Ndorobo ndo wanaoeneza,kwa hiyo wanaoishi karibu na hifadhi za wanyama wapo hatarini kuupata.

Shirika LA afya duniani (WHO) limepanga kuyatokomeza kabisa magonjwa haya kwa kinga na chanjo!!Zinapotolewa wengine hawatumii wakiamini zinaua mbegu za kiume au kufanya uume usisime .

Kwa wale wanaoishi karibu na mito epukeni kushinda mitoni jioni na kuepuka mbu wanaouma maeneo ya mitoni.

Wale wanaoishi pwani ns ukanda wote chanjo za matende,mabusha na kichocho sio za kukosa.