WAAMBIE HAO KUWA HAWAWEZI KUKUELEWA SASA HIVI ~Joas Yunus



Wakati mtu anavyoanza kufanya kitu fulani au kufikiri kuanzisha kitu fulani hupitia changamoto kubwa na hasa changamoto ya kukatishwa tamaaa kutoka kwa watu wanaomzunguka .

Unaweza kukuta mtu amegundua mwenyewe kuwa ana uwezo mkubwa na kipaji cha kuimba lakini watu wanaomzunguka utasikia wakimkatisha tamaa kwa maneno kama haya " hivi wa kuimba atakuwa wewe???" "Wapi familia yenu na kuimba??". Hawa Kaa nao uwaambie kuwa kwa sasa hawewezi kukuelewa maana hawajui unakoenda na wataamini siku nyimbo zako zikirushwa redioni na hapo ndipo watakuja kwako kwa mara ya pili .

Huyu Diamond ambaye kizazi cha dot com kinamshabikia sana alianza naye chini sana na hakueleweka mwanzoni na leo wameanza kumuelewa .Binadamu huwa ana tabia ya kuelewa badae.Wewe ni shahidi wengi darasani mwalimu akitoka ndo huwa wanaelewa .

Mark Zuckeberberg mgunduzi wa facebook mwanzoni wakati anapata wazo la kutengeneza mtandao wa mawasiliano chuoni kwake watu hawakuwa wanamuelewa vizuri na wengi walidhani asingeweza kufika kokote hasa baada ya kufukuzwa chuo watu walijua ndo mwisho wa maisha yake na programu yake ya facebook lakini sasa hao waliodhani hivo sasa wako facebook wanatumia akili ya Zuckeberberg.

Ni kawaida kabisa kutokueleweka mwanzoni na ndio maana hata wewe watu hawakuelewi na wanasema umepotoe njia kumbe wao ndo wamepotea njia .Mtoto anapozaliwa ni ngumu kujua hasa anafanana na nani mpaka akianza kukua  na kuonesha sura yake halisia .Kwanini watu wanakuogopesha wakati hata hawakujui wanabahatisha ??

Najua fika kabisa katika hilo unalolifanya na unalowaza kulifanya kuna watu wengi wamekwambia hutafika kokote na wakakupa mifano ya watu waliokuja na mawazo kama yako .Wamekuonesha changamoto nyingi zilizo mbele yako badala ya kukuonesha fursa zilizopo mbele yako ambazo ndizo zinakusukuma kufanya zaidi .Hawa waeleze wazi kuwa ni vema wakakaa chini maana bado ni mapema kwa wao kuweza kukuelewa wataelewa baadae.

Kuna stori moja kwenye kitabu cha dini kiitwacho BIBLIA ya Nuhu .Nuhu alivyokuwa analanda mbao kwa ajili ya kutengeneza safina kwa gharika iliyokuwa mbele watu hawakumuelewa mpaka yalipowakuta mafuriko na watu wengi wakaangamia.Hawa walielewa baadae mwanzo iliikuwa vigumu kumuelewa Nuhu .

Kuna watu watakuelewa baada ya matokeo au kukuta sehemu fulani .Unajua stori ya Yusufu ??? unakumbuka njinsi ambavyo famikia yake haikumuelewa mwanzoni??? alipokuwa akiwasimulia ndoto ndugu zake nahisi kama walidhani amechanganyikiwa lakini mwisho wa siku walimuelewa baada ya yeye kuwasaidia walivyokutwa na njaa na yeye akiwa ni waziri mkuu wakati huo .

Hey! kwanini unaangalia watu ambao hawakuelewi ???? ,Wewe endelea mbele .Kama unauza genge uza sana na boresha .Kama una mawazo makubwa fanya sana hao wanaokuzunguka wataelewa taratibu kama mwanafunzi anayeelewa baada ya mwalimu kutoka.

0753836463