Kama uko kwenye ajira sasa na
unatamani kujiajiri ni vema ukizingatia mambo yafuatayo kabla hujaamua kuacha kazi
:
1. *Tengeneza chanzo/vyanzo
vya pesa nje ya mshahara*. Ni muhimu sana kama uko kwenye ajira na unawaza kuja
kuachana na ajira kuanza leo kufikiri kuanzisha vyanzo vya mapato nje mshahara
wako wa kila mwezi .
Siri ni hii kwamba ukiwa na
chanzo kingine cha fedha kitapunguza hofu ya maisha yako baada ya kuacha kazi
maana utakuwa na uhakika wa kupata mahitaji yako ya msingi hata kama mshahara haupo.
Watu wengi wameshindwa
kuacha kazi japo wanatamani kuacha kazi kwa sababu vipato vyao vinatokana na
chanzo kimoja na hivyo wanaogopa
wakiacha kazi ghafla familia yake itayumba.Fikiria ni biashara gani unaweza
fanya wakati uko kwenye ajira bila kuathiri kazi yako .Angalia ni kwa namna
gani unaweza kuanzisha mradi wowote eneo ulipo na kama una mashamba fikiria
hata kuanzisha kilimo na ufugaji .
2. Tafuta Taarifa sahihi :
Ni muhimu sana kuwa na taarifa sahihi juu ya kile unachofikiri kufanya baada ya
kuacha kazi kinyume na hapo unaweza kuangukia sehemu ambako siko na ukawa
umepoteza muda na rasilimali nyingi
.Unashauriwa kutumia muda mwingi ukitafuta undani wa kile unachotaka
kukifanya.Hii ni pamoja na kujua mtaji unaohitajika ,Masoko ,wataalam n.k
3. Andika Mchanganuo wa
kibiashara : Ni muhimu sana ukiwa bado uko kazini kuanza kufanya mchanganuo wa
mradi unaotaka kufanya .Mchanganuo huu hutoa picha ya mtaji ,masoko ,watu
wanaohitajika ,washindani na mambo mengine kama hayo .Kama huwezi kuandika
waone wataalam wakusaidie .Umuhimu wake ni kwamba taasisi nyingi za fedha na
watu wanaoweza kukusaidia kupata fedha ya mradi wako wanahitaji mchanganuo huo
.
4. *Anza kujifunza
Usimamizi wa biashara: Ni muhimu sana kupata elimu ya kutosha juu ya biashara
na kwa sasa teknolojia ilivyofika mbali ni rahisi kujifunza kwa kutumia mtandao
.Tumia muda mwingi kujifunza kuhusu biashara na usimamizi wake kwa kusoma
vitabu vya biashara na video ambazo zinaelekeza namna ya kufanya biashara .Acha
kabisa uvivu wa kutokupenda kusoma kama kweli unataka kujiajiri .
5. *Acha Uvivu* :Kama
unajua kabisa wewe ni mvivu kwenye kazi Za watu na mambo yako binafsi tafadhali
usiwaze kujiajiri maana kujiajiri wewe ndiye mratibu wa kila kitu kwa hiyo muda
mwingi itakubidi ufanye kazi .Anza kujibidiisha na kuacha uvivu usio na maana
.Jifunze kufanya kazi bila kusukumwa maana ukiwa kwenye mambo yako hakuna
atakayekusukuma .Utafiti wangu usio rasmi umegundua kuwa watanzania wengi
hawapendi kujiajiri kwa sababu ni wavivu na hawawezi kujisimamia