Hivi, unajua kwamba kila mwanadamu aliumbwa kwa "sababu" fulani?, Una jua kwamba, Mungu alikuumba uje ufanye "kitu" fulani hapa Duniani?, Na kama unajua kwamba uliumbwa kwa sababu fulani, je, hiyo "sababu" unaijua?, Leo mtu akikuuliza kwanini unaishi, unaweza kumjibu?,
Usiidanganye nafsi yako, unahisi tu, lakini hauna majibu kamili na ya uhakika kwanini ulizaliwa, bado hujui ulikuja hapa duniani kufanya nini, na kama unajua basi acha kusoma haya makala!
Inasemekana kuwa, "mtu mmoja tu, kati ya watu kumi ndo anayejua kwanini anaishi hapa duniani, tisa hawajui". Kwa hiyo ukikutana na kundi la watu10, tambua kabisa, kuna mtu 1 au hakuna kabisa anayejua kwanini Mungu alimuumba. Hiki ndio kinachopelekea, baadhi kufanikiwa, na wengine kukosa hata hata ugali mezani.
Hakuna aliyezaliwa kwa bahati mbaya, kila mtu alikuja kutimiza jambo fulani hapa ulimwenguni.
"Kama hauna jibu la kwanini unaishi, basi wewe hupaswi kuwa hai muda huu. Kutambua sababu ya kuishi ni lazima kwa kila mwanadamu"
Leo nimekuandalia njia rahisi 5, ambazo kila mtu anaweza kuzitumia kutambua "sababu" kwanini alizaliwa, na Mungu alimuumba kwa makusudi gani, pia alikuja kutimiza nini hapa duniani;
1.KUPITIA WATU WA KARIBU.
Hapa nawaongelea marafiki, wazazi, walimu, ndugu na watu unaokutana katika harakati zako za kila siku. Angalia ni kitu gani ukikifanya watu wote wanaokuzunguka wanakusifia, chunguza ni kitu gani unaweza kukifanya vizuri zaidi kuliko marafiki zako wote. Kuna mtu uwanjani anajua mpira kuliko wote anaocheza nao na wote wanamsifia, kuna wale huwa tunaombwa ushauri mara kwa mara na marafiki zetu,:kuna mtu akiongea kila mtu lazima wote mkubaliane na hoja zake, Huyo ni kiongozi, kuna mtu akijaribu kuimba tu, watu wote utasikia we ni msanii, au unaweza ukaambiwa wewe ni mtu fulani na mtu yeyote zingatia hayo maneno, mimi nilishawahi kuambiwa kuwa ntakuja kuwa mwandishi na mwalimu wangu, leo wewe ni shahidi na ninachokifanya muda huu. Zingatia sana ni mambo gani ukiyafanya ndugu, marafiki, walimu na wazazi huwa wanakusifia, hivyo ndio vipaji vyako, hizo ndizo kalama na talanta zako ukizifanyia kazi utapata sababu ya wewe kuishi hapa duniani kwa mafanikio makubwa.
2.KUPITIA MAPENDELEO YAKO.
Jichunguze na kujitathimini kuanzia utotoni mwako mpako leo kitu gani huwa unapenda kukifanya bila kuambiwa na mtu yeyote, chunguza kitu gani ukikifanya huwa unapata furaha moyoni mwako, ukikifanya huwa kama burudani au kiburudisho fulani, hapa tunaongelea vile vitu ambavyo unavipendelea kutoka moyoni mwako, nafsi yako hufarijika unapofanya hicho kitu. Kuna watu stori zao soka, ukileta stori za mpira mnakesha, hao ni wachambuzi wa soka kam Shaffi Dauda au Edo Kumwembe, kuna mtu anapenda siasa mpaka basi huyo ni kiongozi, kuna mtu anapenda kuimba, muda wote anasikiliza muziki huyo ni mwanamuziki, kuna mtu anapenda kuandika huyo ni mwandishi, kuna mtu anapenda kuongea mambo ya dini sana, huyo ni shehe au mchungaji, kuna mtu anapenda shule kiasi kwamba kukosa kipindi j3 mpaka ijumaa, huyo ni msomi kiwango cha doctor au professor, kuna mtu yeye zake ni pesa tu na biashara huyo tajiri wa baadae. Angalia ni kitu gani unakipenda, kisha kifanyie kazi hiyo ndio sababu ya wewe kuishi hapa duniani.
3.KUPITIA NDOTO YAKO.
Hapa hatongelei kuota umempata msichana au mvulana unayemtamani kila siku. Ndoto kile kinachokunyima usingizi, yale malengo yako, yale matamanio yako, ile shauku yako. Ile shauku ya kuwa mfanyabiashara, msomi, mshauri, mchungaji, mwandishi, mchezaji, kiongozi, mtangazi, muigizaji, msanii, mwanajeshi, nk. Mara nyingi ndoto huendana na sababu ya wewe kuishi. Nyerere ndoto yake ilikuwa ilikuwa ni kulikomboa bara la Africa, Malcom X & Dr Martin Luther King Jr, ndoto zao ilikuwa ni kupigania haki ya usawa wa rangi zote Amerika.
4.KUPITIA MASWALI BINAFSI.
Haya ni maswali ambayo unaweza kuiuliza nafsi yako. Hapa unaongea na nafsi yako wewe mwenyewe. Muda wa kuiuliza nafsi maswali ni asubuhi ya saa 11 au kabla kulingana na muda unaoamka kwenda kazini, pia muda wa saa 4 usku ukiwa kitandani kabla ya kusinzia. Hakikisha kuna utulivu, hakuna kelele ya aina yoyote, pia unatakiwa kulala chali bila mikono kushika sehemu yoyote ya mwili wako. Mazingira yakiwa sawa kama nilivyo kuelekeza, jiulize swali moja kati ya haya mawili, (i)Je, ningezaliwa nakuta wazazi wangu wameniwekea billion 10, muda huu ningekuwa nafanya nini? (i), Je mimi nilizaliwa nifanye nini hapa duniani, mimi ni nani?. Weka hisia kwenye haya maswali wakati wa kuihoji nafsi yako, unaweza ukachagua swali la kwanza au la pili, baada ya kuuliza swali kaa kwa utulivu kwa muda wa dakika 20, majibu utakayo pewa ndo sababu kwanini wewe unaishi hapa duniani. Fanya hivyo kwa muda wa wiki 4 (siku 28), nafsi yako itakuelezea nini ungekuwa unafanya kama ungezaliwa unakuta billion 20. Usisikitike sana kwa majibu utakayokuwa unapewa, ikilinganisha maisha uliyonayo kwa sasa, hujachelewa bado, Mtume Mhammadi aligundua sababu ya yeye kuishi hapa duniani kuwa ni kutangaza Uislamu akiwa na umri wa miaka 40, lakini mpaka leo kilamtu anajua kama dini inayoitwa Uislamu.
5.KUPITIA IMANI YA ROHONI.
Hii ndio njia kubwa kuliko zote zilizotangulia hapia juu. Hii njia ambayo mwanadamu humuuliza Muumba wake sababu ya yeye kuumbwa. Njia hii ipo kiimani zaidi, mtu hutumia imani yake kuwasiliana na Mungu wake. Hii hufanyikia maeneo ya ibada kama vile kanisani, msikitini na maeneo toauti na hayo kutegemeana na imani ya mtu kama vile kwenye mito mikubwa, miti mikubwa, mapango ya mawe, nk. Tenga muda wako wa ziada, muda ambao kama ni kanisani, msikitini au Mapangoni hakutakuwa na mtu zaidi yako, kwa maana ya kwamba, unatakiwa kuwa peke yako kwa sababu shida yako ni maalumu!. Kwa wale tuaofumba macho na kupiga magoti, fanya hivyo, kisha, Muulize hivi Mungu wako, Mungu, kwanini uliniumba?, Uliniumba nije kufanya nini hapa duniani?, Mimi ni nani?, baada ya kuuliza hivyo, tulia kwa muda wa dakika 30, fanya hivyo kwa muda wa siku 28, Mungu atakuambia wewe ni nani, na ulizaliwa kwa sababu ipi, hakikisha unakuwa kiroho na kiimani.
NB; Hizi njia mbili za mwishoni (4 & 5), zitumiwe kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu, unaweza ukaongea na mashetani, ukapotoshwa, kama hujiamini kiroho, tumia zile 3 za juu!!
Socrate, Plato, Aristotle, Machiavelli, St. Thomas, St. Augustine, John Lockey, Carl Marx, Shake Speare, Napoleon Hill, Nelson Mandela, Suzan Anthony, Steve Biko, Nkwameh Nkrumah, Dr Martin Luther King Jr, Malcolm X, Robert T Kiyosaki, Jakaya Mrisho Kikwete, Dalai Lama, Henry Ford, Bill Gates, Eric Shigongo, Bahresa, Bob Marley, Mahatma Ghandi, Dubois, Marcus Garvey, Michael Jackson, Jay Z, The Game, African Bambataa, Dj Cool Herc, Bill Clinton, George Bush, Queen Elizabeth, Uhuru Kenyatta, Che Guavara, Fidel Castro, Shaban Robert, Desmond Tutu, Robert Mugabe, Mkapa, Luck Dube..................... Walijua/wanajua kwanini waliumbwa, na sababu yao kuwepi hapa duniani nini, baadhi yao hawako hai kimwili, wapo hai kifikra, ila kama ungebahatika kukutana hata na mmoja wao ukamuuliza kwanini unaishi, angejaza kurasa zaidi ya 10 za maelezo kwanini alizaliwa na kwa nini anaishi!!
"~If you don't find something to live for, find something to die for"~ 2 PAC.
"~To live without a reason to live for, is a biggest sin God will never forgive ~" Kashindi Edson.