Maneno kwa lugha
rahisi ni matamshi au maandiko au sauti au video inayoelezea akili/moyo wa mtu
ulivyo.:Maneno unayoongea,maana yake ndiyo akili yako,na ndiyo yaliyojaa moyoni
mwako.(luka 6;45).
Maneno yako ndio
nia yako uliyo nayo moyoni.Maneno yako ndio maisha ya.Maneno yako,ndivyo ulivyo
ndani na nje.UNACHOONGEA NDICHO
UNACHOWAZA,NA NDICHO UNACHOKIAMINI,NA NDICHO UNACHOKIISHI AU UTAKAACHO KIISHI.
USIPOFUNGUA KINYWA CHAKO UKAONGEA,AU UKAANDIKA,HAKUNA ATAKAEJUA
UNACHOWAZA.Ndio maana
katika interview kuna kuandika na kuzungumza.Hata kama una akili kiasi
gani,lazima uzungumze ili watu wakuelewe na wakujue ulivyo.
Na ndio maana nchi
nyingi wakati wa uchaguzi wagombea wanazunguka kuzungumza na wananchi na kutoa
ya moyoni.wanazungumza na kupewa maksi aidha wanafaa au hawafai kuchaguliwa.
What is
POWER??Nguvu maana yake ni ule uwezo wa kufanya jambo baya au zuri.POWER is
the ability either to push or pull.Kuna nguvu gani katika maneno tunayotamka au
kutamkiwa??
JINSI ULIVYO NI MATOKEO YA MANENO ULIYOJINENEA WEWE MWENYEWE AU
ULIYONENEWA.
KAMA UKO VIZURI NI MATOKEA YA MAMBO MAZURI ULIYONENEWA.NA KINYUME
CHAKE.
Katika makuzi
yako,umepitia mikononi mwa wazazi/walezi/walimu na jamii kwa ujumlaWAMEKUTAMKIA
NINI?????WALIKUAMBIA WEWE NI NANI???MWALIMU WAKO SHULENI ALIKUAMBIA NINI???
Ulivyo sasa,ni
matokeo ya maneno yaliyonenwa juu yako.Tusome neno kidogo tu.Mithali 18:21,Mauti
na uzima,huwa katika uweza wa ULIMI(maneno).
Kama tuko pamoja
nipungieKwa hiyo kufa au kuishi,ni mdomo wako.biashara yako kufa au kustawi,ni
ulimi wako.Mauti sio lazima ufe kabisa kimwili,hata maisha yako)Tusome tena Mithali
6;2.
UMETEGWA NA
KUKAMATWA NA MANENO YA KINYWA CHAKO.na mithali 12:14UTASHIBA MATUNDA YA KINYWA
CHAKO.Tunajadili NGUVU ILIYOKO KATIKA MANENO.Haijalisha unajitamkia au
umetamkiwa au unatamkia wengine.NGUVU NI ILEILE,maadam yametamkwa.
Katika maneno yetu
ya kila siku ziko nguvu kuu mbili.na huwezi kuishi nje ya unachotamka.Kwa
sababu unachotamka hakitoki hapo mdomoni.kimeanzi huko moyoni.na MOYONI ndiko ghala kuu la maneno na matendo.Akili
haifanyi kazi kabla ya moyo kutoa go ahead.
Neno linasema,LINDA
SANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO,MAANA NDIKO ZITOKAZO CHEMCHEM ZA UZIMA.NA
AKASEMA,KIMTOKACHO MTU(MANENO)NDICHO KIUJAZACHO MOYO WAKO.
YAANI KWA MANENO
YAKO,UTAKUFA AU UTAISHI,UTAKUWA TAJIRI AU MASIKINI,UTAAJIRI AU
UTAAJIRIWAUTAOLEWA AU HUTAOLEWA.MANENO YAKO YANA NGUVU KULIKO INAVYOFIKIRI.
Tuanze mifano ya
matamshi na matokeo yake.Muasisi wa nchi yetu ,alitamka kuwa Tanzania ni nchi
ya aina gani????Wakati unaendelea kutafakari alichotamka muasisi wetu,kumbuka
ukifuatilia wakati wa uumbaji wa MUNGU ,kila alichokiumba;biblia inasema,ALIONA
NI CHEMA .Maana yake alitamkia mema uumbaji wake.
NI MARA NGAPI UMESIKIA MASIKIONI MWAKO VIONGOZI WENYE
DHAMANA,WAKITAMKA MARA NYINGI SANA KUWA TANZANIA NI NCHI MASIKINI????
Kiongozi alipoingia
madarakani,aliona (moyo)vitu vitatu.UJINGA,MARADHI NA UMASIKINI.Kinywa
kikatamka.na taifa likatangaziwa.LAKINI HAKUONA UZURI WA NCHI YETUKAMA DHAHABU,MITO,MBUGA
ZA WANYAMA.
Unataka kuniambia
nchi ilijaa wajinga,magonjwa na masikini???hapakuwa na kizuri cha kumtukuza
Mungu.Kwa hiyo Mungu kuifanya
Tanzania,work done was zero.kweli????
WAKATI WENZETU
WAMEANDIKA KWENYE KWENYE HELA YAO MANENO YA KUMTUKUZA MUNGU KUWA "IN GOD
WE TRUST"(kwa sababu fedha na dhahabu ni mali ya Bwana.)hayo ndiyo maneno
yao.KWA NINI DOLA ISITAWALE DUNIA,WAKATI WAMEKIRI KWA VINYWA VYAO KUWA THEY
TRUST IN GOD????
WAKATI WAO WANAKIRI
HAYO,NA KUWEKA NYOTA KATIKA BENDERA
YAO,(nyota siku zote inangaa.hata Yesu alipofufuka,waliiona nyota yake
mashariki).SISI TUMEKAZANA KUMSUTA MUNGU KUWA TANZANIA NI MASIKINI,PAMOJA NA
UTAJIRI ALIOTUPA AMBAO HAUPO HATA KWA WENZETU.BENDERA YETU INA MPAKA BLACK
COLOR. Na tulitamkiwa kuwa africa IS A DARK CONTINENT.unategemea nini??
Kwa maneno
aliyotamka kiongozi mkubwa ardhi ikaandika,kwa nini tusivae chupi walizovaa
wenzetu na kujiona ni sawa tu??Kila wakati tunasaidiwa na wenzetu.Marekani wao
nani anawapa missaada.?? .
HAWAHITAJI
MISAADA KWA MAANA UCHUMI WAO WAME UCONNECT NA MWENYE FEDHA NA DHAHABU.Nyinyi
fedha yenu ikoje.???ndio kwanza ina picha za nyoka???.
TURUDI KWENYE
MIFANO YA WATU BINAFSI.kila wakati hapa tunatoa mifano ya watu waliofanikiwa
akiwemo NICK WA AUSTRALIA.Swali,huwa anajitamkia maneno gani?????ulishawahi
kusoma mahali ameandika yeye ni kilema????? .Kijana yeyote aliyewahi kusoma
mahali hao watu waliofanikiwa wakijitamkia kuwa wao ni masikini au
vilema.waseme.
Kama ulishawahi
kumsikia Reginald Mengi akisema yeye ni mfanyabiashara mdogomdogo niambie hapa
leo.HUWA UNAJITAMKIA NINI??MAMA YAKO ALIKUTAMKIA NINI???MWALIMU WAKO
ALIKUAMBIAJE???
KUMBUKA TU.MANENO
YANA NGUVU.Umeshindwa kusonga mbele kwa sababu ya maneno uliyoaminishwa na
unayoendelea kujitamkia.TANZANIA INA WASOMI WA KUTOSHA.TENA MAINJINIA .ni
watanzania wangapi wanapewa tenda za kujenga barabara???Ni watanzania wangapi
wanamiliki migodi???shida sio wao wala serikali.SHIDA WALITAMKIWA KUWA TANZANIA
NI NCHI MASIKINI.
NCHI MAANA YAKE NI WATU.NCHI MASIKINI MAANA YAKE NI MKUSANYIKO WA WATU
MASIKINI.NCHI TAJIRI MAANA YAKE NI MKUSANYIKO WA WATU MATAJIRI.NI NGUMU SANA
KUONDOKA KWENYE MANENO YALIYOJENGA MSINGI WA MAISHA YAKO.
Kuna watu
walitakiwa wawe madaktari,lakini wakakutana na walimu wasiojitambua wakawaambia
masomo ya sayansi ni magumu hamuwezi (MANENO)na wakakata tamaa.KUMBUKA
WALIOKUTIA MOYO(waliokutamkia maneno mazuri)na yakakuinua.
Walioko
mahakamani,wanahukumiwa kwa maneno yaliyotungwa(vifungu vya sheria)yawe mabaya
au mazuri.Nchi inaongozwa na katiba(maneno yaliyoandikwa ).Ndio maana kuna
wakati wananchi wanataka katiba ibadilishwe(maneno /matamshi)
Nenda kariakoo.wale
wafanyabiashara wakihojiwa na vyombo vya habari wanasema.Serikali itusaidie
sisi watu wa hali ya chini..Au serikali ituangalie sisi wafanyabiashara
wadogowadogo.Hawatainuka hapo.watauza malimao hata miaka hamsini.kwa sababu
wameshajitamkia hivyo.
Kwa nini watanzania
wengi wanajitamkia hivyo???NI KWA SABABU NDIO ROHO ILIYOWEKA MISINGI YA NCHI.Mtoto
akizaliwa Tanzania,anaenda shule anaambiwa lengo la elimu ya msingi ni
kupambana na maadu watatu.maradhi ,ujinga na umasikini.
Tuende sehemu ya
mwisho ya nini cha kufanya ili tutoke hapo
Vijana wengi
sikiliza salamu zao.wanasalimianaje?????wanaitana majina gani????Vijana
wakikutana utasikia,Niaje mchizi wangu.Mambo niaje,Kijana mwingine anajibu,Mzuka
tuu!Mzuka maana yake nini??Mchizi maana yake nini???
Haya maneno vijana
wanayojitamkia kwa kujidai ni salaam za kisasa,yamewafanya kuwa machizi kweli.Huwezi
kuvaa suruali ukaonyesha chupi yako nusu kama sio chizi(maneno uliyojitamkia)Huwezi
kukaa kijiweni masaa nane ukizungumzia mafanikio ya Lionel mesi na kujua kila
mchezaji wa nje analipwa nini,wakati wewe una miaka 27 unakaa kwa shemeji yako.
MANENO YAKO YAKO
NGUVU.NGUVU MBAYA AU NZURI.NI UAMUZI WAKO
Wakati Tanzania
hata ambao wamepoteza mkono mmoja tu ,wanajiita ombaomba na wanakaa mpaka nje
ya ikulu,Nick aliamua lile neno Disable akalibadilisha kuwa God is able,UNAJITAMKIA
MANENO GANI?UNAMTAMKIA MUMEO/MKEO MANENO GANI??WATOTO WAKO UNAWATAMKIA NINI???
Unawaambia watoto
wako nini kuhusu elimu??uchumi??ndoa???n.k.Watoto watayaishi maneno ya baba na
mama yao.haijalishi ni mabaya au mazuri.Kama wewe na mkeo mnawasema watu mbele
ya watoto,wakikutana nae njiani,watamdharau maana wanakuamini wewe mzazi na
unachosema.
CHUNGA MANENO YA
KINYWA CHAKO.Ni Mara ngapi umesema HUWEZI.bila hata kujaribu hiyo
kazi/biashara??MARA NGAPI UMESEMA SIKU HIZI HAKUNA WANAUME WAAMINIFU.mmeo
akitoka nje ya ndoa unalia nini???.BAADHI YA WALIMU PIA NI KUNDI LINHINE LENYE
MANENO MABAYA NA KUWAVUNJA MOYO WATOTO.
UKIMWAMBIA MTOTO
HUWEZI,LILE NENO LINAMKAA MAISHANI MWAKE.NDIO MAANA HATA WEWE UNAKUMBUKA MAMBO
MENGI ULIYOAMBIWA UKIWA NA UMRI KUANZIA MIAKA MITATU HADI KUMI NA MBILI AU
KABLA YA BALEHE.
CHUNGA MANENO YAKO.YANAWEKA MSINGI WA WATOTO WAKO.
UKIMWAMBIA MTU,NITAKUPIGA AU NITAKUUA Utafungwa maana
maneno mabaya yanaumiza sana sana.UKIMWAMBIA MTU NAKUPENDA SIPATI USINGIZI
KABISA NIKINYWA MAJI NAKUONA KWENYE GLASI.Haya maneno ni mazuri sana.yanasuuza
moyo.hata kama hakuwa na mpango na wewe atakubali,akija kujuta ni baadae.
MAUTI NA UZIMA,VI
KATIKA UWEZA WA ULIMI.Basi sisi tutumie
ndimi zetu positively.(kunena mema)YAANI HII IANZE NA MTU MMOJA
MMOJA,BAADAE FAMILIA,BAADAE JAMII NA HATIMAE TAIFA.tukiendelea hivyo,baadhi ya
watu wameshaanza maombi ya kufuta haya maneno.
[Halafu tuwe na
nidhamu ya kinywa .Ukiamka asubuhi,sema hivi,ee Mungu,weka mlinzi kinywani
mwangu.(zaburi 141:3)Huyu mlinzi ambae ni Roho mtakatifu.atakuchagulia maneno
ya kuongea.Hutaongea kila neno.Maneno ni sumu Na maneno ni asali pia.
Kuna watu
wamefungwa kwa maneno tu.Kuna watu wamevunja ndoa kwa maneno tu.Kuna watu
wamefukuzwa kazi kwa maneno tu na umbea.Kuna watu wamelaaniwa na wazazi wao kwa
ajili ya maneno yao.Kuna familia zimesambaratika kwa sababu ya maneno.
Unatamka
nini???unanena nini??Maneno yako ndio maisha yako.HATA MWIMBAJI MMOJA AKAIMBA
VILE UNAVYOKIRI ,NDIVYO UTAKAVYOKUWA.Ni maneno matamu tu ulimwambia mkeo
,mwenyewe akalainika akabeba begi akahama kwao akahamia kwako.NGUVU YA MANENO.
NI MANENO YA UONGO
ulimwambia huyo mwanafunzi mpaka akaacha masomo akidhani
utamuoa.hujamuoa.MANENO YA UONGO .(mithali 10:8) mpumbavu mwenye maneno mengi
ataanguka.UNATAMKA MANENO GANI??
maneno yako
yanajenga au yanabomoa, Yanafarakanisha au yanapatanisha.
Yanainua au yanaua
nafsi za wengine, Yote uliyojinenea umeyaona mwenyewe.
PALE ULIPOSEMA
HUWEZI KWELI HUKUWEZAPALE ULIPOSEMA UNAWEZA,UMEWEZA.
Popote
ulipo,unapoona pana kitu kisichofaa,Tamka unachotaka kiwe.Ayubu
22:23..inasema,utakusudia neno,nalo litathibitika.Tamka unataka watoto wako
waweje.Ita watoto wako majina yenye utukufu.Adam alipomtazama Hawa alisema hii
ni nyama katika nyama yangu,mfupa katika mifupa yangu.Wewe unasema,huyu mchaga
sijui nilikutana nae wapi.Ita watoto majina
yao mazuri.
Waite
mainjinia,madaktari,pilot,walimu,wachungaji,wakue wakijua hivyo vitu vipo.
HATA UKIJIITA MASIKINI
JANUARI MPAKA DISEMBA HAIKUSAIDII.UNAJIWEKEA MIHURI BURE.HAIKUONDOI HAPO
ULIPO
JITAHIDI KUONA KITU KIZURI KWA KILA MTU AU KWENYE KITU
UNAVHOKITAZAMA.ITAKUSAIDIA SANA.
Mungu awabariki sana.