*Utajiri* wowote
huanza na wazo .Wazo ni kama *mbegu *ya mahindi abayo baadae huzae mahindi
mengi zaidi .Unapoosikia utajiri Mkubwa wa Bilgate alianza katika wazo .
Kuwa na wazo tu
haitoshi ni lazima ufanyie kazi mawazo unayozalisha.Ni ngumu sana kufanyia kazi
mawazo tunayopata kila siku kwa wakati lakini ni muhimu kuyaandika na kuyapa
vipaumbele(uanze na lipi ).
Kumekuwa na shida
kubwa kwa watu kupata mawazo mazuri na wengine kujiuliza kwa namna gani watu
wengine wanapata mawazo mazuri .Ukweli ni kwamba kila mtu anaweza kuwa na
mawazo mazuri kama akifuata kanuni za kupata mawazo mazuri .
Hizi ni baadhi ya
njia ambazo unaweza kuzitumia kupata mawazo mazuri ,kinyume na hapo utabaki
kusema huna bahati na kuwa watu wengine wanatumia uchawi kumbe mchawi wa kwanza
ni wewe.
1.*Tafuta
marafiki wapya* : Ni muhimu kuhakikisha kuwa unapata marafiki wapya kwa namna
yoyote.Kuna watu kwa mwezi hawatafuti marafiki wapya na wamekuwa ni watu wa
kukaa na watu wale wale ,wenye tabia na mawazo yale yale na wamewafanya wasifikirie
zaidi ya wanavyofikiri.
Ndugu watu
waliofanikiwa na wanaofanikiwa wana tabia ya kutafuta marafiki wapya ,wenye
mawazo mapya ,mitazamo chanya na kiu ya mafanikio.Hakuna namna utapata mawazo
mapya na mazuri kama unakuwa na marafiki wale wale .
2. *Soma vitabu
kila siku*: Ukitaka kupata mawazo mapya hakuna namna utakwepa kusoma vitabu
kila siku na kupata maarifa mapya .Kupitia vitabu unaweza kupata wazo zuri
kupitia maarifa unayopata .Ukweli uko hivi kama hupendi kusoma vitabu hautaweza
kupata mawazo yoyote.
3. *Kuwa mtu wa
kuchunguza vitu* : Hii pia ni njia ambayo inasaidia kupata wazo zuri .unapopata
ziara kwenda mahali fulani ni njia nzuri ya kujifunza na kupata mawazo mapya
,chunguza sana vitu utakavyovikuta huko .Unaweza kupata wazo kokote kule kama
ni mtu unayechunguza vitu .Kuna watu wao wakisafiri njia nzima wanalala tu
,hawa hawapendi kujifunza na kupata mawazo kwao si kitu rahisi na chepesi .
4. *Peruzi Kwenye
mitandao (web surfing) *; Dunia ya leo ya TEHAMA imeturahisishia vingi kwa
makusudi yetu tumeshindwa kutumia mtandao vizuri .Tuna simu nzuri sana ambazo
kupitia hizo tunaweza kujifunza mambo mengi lakini simu zetu zimekuwa za kuchat
tu watsap na kubadilisha profile zao facebook
5. *Penda
kuandika (Keep Journal) * : Kimsingi huwa tunazalisha mawazo mengi sana kwa
siku lakini hatuna utamaduni wa kuandika mawazo yanayokuja akilini mwetu .Kuna
mawazo tuliyapoteza kwa kutokuandika na kuyapuzia na hayo watu wengine
walivyoyapata wamekuwa matajiri .Mawazo yatakuja popote na muda wowote kwa hiyo
ni muhimu kuwa na journal .Simu yako ya mkononi inaweza kukusaidia au Diary
book .Katika mawazo mengi unayozalisha na kuyaandika utapata wazo zuri .
*JYB (0753836463) *