Kuanguka ni miongoni mwa mambo ambaayo watu wengi
hatuyaelewi sana. Tunaamini ni kitu cha
kukiogopa na kukikwepa kwa nguvu zote na gharama zote. Na mbaya Zaidi kushindwa
huko hakuna mtazamo mzuri mbele za jamii. Fikiria mtu umekopa pesa bank halafu
ukafilisika vibaya na kuipoteza yote.. Umefanya mtihani na ukafeli vibaya au
umeanzisha mradi Fulani umeshindwa kuendelea. Inaumiza sana. Kwa mtu ambaye
hajajulia mchezo huu anaweza kuhisi ana laana. Tunaamini kuwa kushindwa ndio kitu kibaya kuliko vyote. Ni kweli kuwa sio kitu kizuri sana kwa
mtazamo wa kawaida kama kitakukuta. Nakumbuka kuna wakati niliweka pesa nyingi
kwenye biashara Fulani na ikapotea yote. Iliniuma sana lakini nikajua kuwa ili
niimarike katika biashara lazima kuanguka kwanza. Kuna msemo unasema kuwa tunashindwa kwa
sababu hatujajifunza vya kutosha. Kuna
funzo zuri sana lipo katika kushindwa.
Sababu zinazokufanya uanguke
au ushindwe ni kama zifuatazo:::::::;
1.UNAKATA TAMAA MAPEMA SANA.
Ni sababu kubwa sana hii. Watu wengi wanaanguka kwa sababu
wakata tamaa mapema. Pale ambapo mambo hayaendi wao wanahisi ndio mwisho.
Kumbuka kuwa tunaishi katika ulimwengu wwenye milima na mabonde. Misukosuko
ndio mwendo wa ngalawa. Labda hujaona
faida au matokeo mazuri kwa muda wa miezi mitatu, sita au mwaka mzima unahisi
sasa haiwezekani. Mafanikio huchukua muda mrefu sana. Kuanza kuona faida
itakuchukua miaka mingi. Usikate tamaa. Tengeneza misingi mizuri na usikubali
kupoteza zile jitihada zako ulizoziweka tangu awali.
2. UNAOGOPA MNO KUANGUKA.
Kumbuka kuwa hatua yoyote ya mafanikio huwa na maumivu
makubwa sana. Tumia mfano rahisi wa mtoto anayejifunza kutembea huanguka mara
nyingi sana. Lakini yule mtoto mwoga kuanguka huchelewa sana kutembea. Wapo wanashindwa
mapema kwa sababu ya woga wa kuanguka.
Akishaona kuna dalili kama mambo hayaendi anakuwa ameshashindwa. Kama una malengo mazuri hakikisha unapunguza
kuogopa kushindwa. Angalia nini nini utakipata mwishoni.
3. HUJAWAHI KUANGUKA MARA NYINGI.
Jambo mojawapo la kukufanya ushindwe kwenye mipango yako
ni kuwa huna uzoefu na kuanguka. Kuanguka kuna funzo kubbwa sana. Mtu
aliyeanguka mara nyingi huwa imara sana. Anajua wapi huwa panasababisha
akaanguka. Ana ujuzi, maarifa na uzoefu
wa kutosha. Huwa makini sana katika kila hatua. Ni
mwepesi sana wa kulisoma anguko na kulizuia au kulikwepa. Na kijiwekea tahadhari kubwa sana.
4. HAUPO TAYARI KUPATA MAFANIKIO.
Kila kitu kina maandalizi ya namna ya kukipokea. Mafanikio
yanayokuja bila kupangiliwa hupotea
mapema sana. Lazima uwe na mipango sahihi ya kila hatua ya
mafanikio. Lakini pia lazima ujue namna
gani utaweza kuyashikilia mafanikio hayo. Umefika kilele cha mafanikio yako.
Unawezaje kubakia juu hapo. Unawezaje kumudu sifa unazozipata kutoka kwa watu?
unawezaje kubakia na nidhamu ile uliyokuwa nayo wakati uanyatafuta? Watu
haunguka mapema kwa sababu ushindi wa kwanza huwaondolea nidhamu, umakini na
bidii ya kupata mafanikio Zaidi. Hapa ndipo uankuta mtu anaanza kurudi nyuma.
Uanchotakiwa ni kuendelea kuhitaji Zaidi na Zaidi.
Unaweza kutupata Zaidi kwa kutembelea mtandao wetu uitwao
www.mimimjasiriamali.com , pia kumbuka kulike page zetu mimi
mjasiriamali.com na Grow RICH TZ. Karibu
sana.