Ni jambo linaloweza
kushangaza hapa kwetu Tanzania lakini haya ndiyo maisha ambayo wenzetu
wamefikia .Huku kwetu mtu akianzisha kampuni watu wanashangaa hata kama ana
miaka 60 lakini huko kwa wenzetu watoto wadogo wanaanzisha makampuni na ni
jambo la kawaida na hapa ndipo nakubaliana na msemo wa Bishop John Shusho kuwa
Dunia inakimbia lakini watanzania tunatambaa.
Juzi Rafiki yangu Lazaro
Samweli alituma picha ya mtoto ambaye alisema anamiliki kampuni akiwa na umri
mdogo sana .Nilivyoona hivyo ilinilazimu kufuatilia historia ya huyo mtoto
maana napenda kufuatilia vitu na kupata taarifa za uhakika .Leo nakujulisha na wewe uweze kumfahamu msichana huyu mdogo
ambaye alizaliwa kama wewe lakini yeye akiwa ni mtu wa kudhubutu kuliko wewe
.Mtu mmoja akasema umri ni namba tu na
haufanyi chochote kwenye maisha kumbe hakuna muda wa kusubiri ndivyo
alivyogundua msichana huyu anayefahamika kwa jina la "ASIA NEWSON"
Asia Newson ni
msichana mwenye umri wa miaka 13 kule
marekani ambaye alianzisha Kampuni yake iitwayo Super Business Girl (http://www.superbusinessgirl.com) akiwa
ana miaka mitano (5).Kampuni yake inahusika na utengenezaji wa mishumaa na huwa unawafundisha watoto namna ya kuwa
wajasiriamali maana ndoto yake ni kuona watoto wanakuwa wajasiriamali .
Alianza kujifunza
kutengeneza mishumaa kutoka kwa baba yake na baadae akaanzisha kampuni kutokana
na ujuzi aliopata kutoka kwa baba yake .Uwezo wake wa kujieleza unadhihirisha
kuwa ni mtoto aliyeandaliwa na yeye akakubali kuandaliwa .

Asia atoe funzo kwetu
kuwaandaa watoto wetu kuwa waajiri hasa katika miaka hii ambayo ajira imekuwa
changamoto .Ndiyo inawezekana kuwa na watoto kama Asia Newson kama familia
zitawajengea uwezo watoto wao na kuwaonesha uwezekano wa kufanikiwa kama
watatumia uwezo wa ndani walio nao .
Kwangu mimi Asia amenipa
nguvu mpya ya kukaza uzi na kuamini kuwa hakuna lisilowezekana kama mtu akiamua
.Kumbe unaweza kuwa yeyote na ukapata chochote unachokipata kama utaamua .
Wazazi ni changamoto kwenu
kujiuliza nini utamrithisha mtoto wako ambacho kitamsaidia maisha yake yote .
Joas 0656110906
*Kumbuka kujisajiri kwenye
semina ya mtandaoni kwa ada ya sh 5,000/= tu.Tuma kwa Tigopesa 0656110906 na 0753836463*