AKUONGEZAYE SHUKA ATAKA UZIDI KULALA ~ Joas




Kabla ya kulala nilimuomba *ndugu kuamka mapema* aniamshe majira ya *sa kumi alfajiri*  ili niweze kuamka nikajisomee kwa ajili ya maandalizi ya mtihani maana nilikuwa na utamaduni wa kujisomea asubuhi kujiandaa na mtihani au maandalizi binafsi maana niliamini kusoma kwa bidii ndiko kungenisaidia mimi kufaulu mitihani yangu na kufanya vizuri sana*(sikuamini katika maandalizi ya zima moto)*_

_Licha ya kukubaliani kuwa aniamshe, ndugu huyu *hakuweza kuniamsha* na badala yake alipoamka *alinifunika kwa shuka lake zito alilokuwa amejifunika* .Loo! Kwa baridi ile kali  ya Njombe wakati huo nikiwa Njombe sekondari maarufu kama Njosi sikuweza kuamka maana nilivyoongezewa shuka ndipo usingizi mzito ulinishika maana baridi kali ya siku ile nilishindwa kulala vizuri._

Asubuhi nilipoamka nilaanza kumlalamikia kwanini hakuweza kuniamsha na akawa amenijibu hivi "Niliona kuwa usiku ulihangaika sana kwa kukosa usingizi kwa sababu ya baridi kali ndipo nilipoingiwa na huruma  ikabidi nikuongezee shuka langu wakati nilivyoamka".Alisema

*FUNDISHO* .

Marafiki zetu tunaowapenda wanaweza kutupoteza pamoja na kwamba tunawaamini .Ni muhimu sana kuwa makini .Wakati ukiwa unatafuta mafanikio na mkakubaliana kusaidiana kwa namna fulani yeye anaweza kuamua kufanya vinginevyo na akadhani kuwa anakusaidia kumbe anakupoteza .

Kuwa makini sana na mwajiri wako ,kuna vitu anaweza kufanya kwa ajili yako ili uendelee *kuua ndoto zako* japo yanaonekana kwa macho yanaonekana mazuri lakini *mwenye jicho la tatu* ataona kama ni dalili ya kuua ndoto zake.

Ona, unaposikia mtu *amepanga kuacha kazi* ili afuate *ndoto zake* lakini ghafla *mwajiiri wake akamshawishi achukue mkopo mkubwa* maana yake nini??? .Unaposikia mtu amepanga kuacha kazi mwezi ujao ili afanye yake ghafla *mwajiri akamuongezea mshahara* ambao hapo awali hakuwahi kuongezwa maana yake nini ??? .Hili naliona *halina tofauti* na yule aliyeongezewa shuka akadhani anasaidiwa kumbe ndo anaendelea kulala na mwisho hakuamka kufanya maandilizi ya mtihani .

Kuwa na jicho la tatu na soma alama za nyakati !