Katika
vitu ambavyo humtofautisha tajiri na maskini ni namna wanavyofanya uwekezaji
.Mfano Maskini hununua ardhi na kuiacha miaka kumi bila kuiendeleza huku tajiri
akinunua ardhi hufanya mwendelezo wa ardhi hiyo kwa kujenga kiwanda,kulima n.k.
Watu
wengi wanapenda kuwekeza lakini hawana ujuzi wa wapi wanapaswa kuwekeza na
mwisho wa siku maisha yameendelea kuwa kama yalivyo kwa muda mrefu .
Sababu
kubwa ya watu kuwekeza na kubaki kuwa kama walivyo ni kuwa hawakufuata kanuni
za uwekezaji .Yafuatayo ni maeneo muhimu ya kufanya uwekezaji wenye tija kwa
faida ya vizazi vyako .
1. *Uwekezaji katika Maarifa* :
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa
Maarifa~Biblia
Eneo hili la maarifa ndio msingi mkubwa wa mwekezaji awaye yeyote .Ni
kama vile mjenzi wa nyumba asivyoweza kujenga nyumba yeyote bila msingi .Ni
muhimu sana kuyatafauta maarifa kwa gharama yoyote maana maarifa ndiyo funguo
ya vitu vyote hapa Duniani .Bila maarifa utanunua eneo kubwa na hutaweza
kuliendeleza ,bila maarifa hutapata mawazo ya nini ufanye kama biashara yako
haiendi .Bila maarifa utabaki ukiamini kuwa kuna watu wana bahati na wewe huna
bahati
Tajiri
huchukua miaka mingi sana akitafuta maarifa ya kile anachodhani anaweza kufanya
wakati maskini hana muda wa kutafuta maarifa na ndiyo maana mambo yake hayaendi
.Unapaswa kusoma vitabu sana ,unapaswa kuhudhuria semina mbalimbali ,unapaswa
kusikiliza vit vya kukuongezea maarifa .
Shida
na hii kwamba usipoyatafuta maarifa kuna vitu vingi hutaweza kuvifanya .Kwa
mfano una wazo la kuanzisha biashara ya mtandaoni (online business) wakati huo
hutafuti maarifa ya kuijua vizuri biashara hiyo ujue huwezi kufika unakotaka
kufika .
2.*Uwekezaji katika Muda*: Vijana wengi
sasa wanatamani maisha yaende haraka haraka sana .Wanatamani mafanikio haraka
sana huku wakisahau kuwa hata kuzaliwa kwa binadamu ni mchakato wa muda mrefu .
Ukitaka
kuwa na mafanikio makubwa lazima UJUE
kuwa kuna vitu haviwezi kuleta matokeo haraka kama unavyoweza kufikiri ,vinahitaji
subira ili vianze kutoa matokeo .Ndiyo maana imekuchukua miaka 17 Na zaidi
mpaka unaitwa mtu mwenye shahada ya kwanza .
Ni
muhimu sana kujua kuwa muda ni mali na hivyo kadri unavyowekeza kwenye muda
ndivyo unavyopata matokeo makubwa .
3. *Uwekezaji katika watu*: Hii ni sehemu
ya uwekezaji ambayo watu wengi wamejisahau na mwisho wa siku wameshindwa
kufanikiwa .
Watu
pekee ndio wanaoweza kukufanya ufanikiwe kwa haraka zaidi .Tengeneza mtandao wa
watu wenye tija na fikra chanya ambao kila iitwapo leo watakufanya kuiona ndoto
yako kuwa inawezekana .
Kuwekeza
katika watu pengine utatumia muda na vitu vingine lakini wewe usijali ,jua kuwa
huo ni uwekezaji unaodumu miaka na miaka .Tumia muda kuwasaidia watu na
kutengeneza mtandao wa watu .
Matajiri wengi Duniani walijua nguvu iliyoko
kwenye mtandao wa watu(Power of Network) na kupitia mtandao walipata mafanikio
waliyoyataka .