Mfano;kuna kipindi inaibuka vijana wengi
sana walisomea hotel management.yaani
kila kona wanasoma hiyo course.ikafika mahali ikaisha.Ikatokea wengi sana
wakasomea public relations.nayo ikapita.Ikatokea hapa juzi wakaibuka matabibu
wengi sana wa tiba mbadala.kila kituo cha tv ukifungua ni tiba mbadala.nayo
imepoa.Ikaja ufugaji wa kware.wengi sana walifuga.sasa imepoa.Kwenye biashara
nako hivyo hivyo.utakuta huyu kafungua saloon.basi mtaa mzima ni saloon.
Nimetoa mifano michache.Je??unafikiri nini sababu
ya fursa kuibuka na kupotea??
1. Kutokumtegemea
Mungu na kufikiria peke yako unaweza.
2. Kutokuwa na imani kuwa utaishi.yaani kuna
mpaka watumishi ukienda msibani utasikia wakisema ,sisi ni marehemu
watarajiwa.sasa marehemu mtarajiwa anaweza kuwa na miradi endelevu??wenzetu
wana mipango binafsi hadi ya miaka tisini na tano.wewe mpango wako mrefu
umeweka miaka mingapi???kama sio miwili
3.Uvivu wa kufikiri.yaani mtu anaanzisha mradi au
biashara.hakai kusoma,au kupeleleza au kutafuta taarifa nyingi kuhusu
anachokifanya.anafungua biashara,anafanya usafi anakaa nje ya duka au ofisini
bila hata kufanya vhochote kuongeza ujuzi.kwa hiyo miaka nenda rudi unakuwa
huna jipya.mwishowe biashara inakufa.
4. Kutokuheshimu mitaji.Mtu unachuka mkopo
kuanzisha biashara .na hutengi faida na mtaji.kwa hiyo unakula zote😃😃mwisho
wa siku unabaki unarejesha tu huongezi bidhaa
5 Kukosa maarifa.(sio kukosa elimu) Elimu unayo
lakini huna maarifa ya unachokifanya.kwa hiyo unakuwa unafanya alimradi.
6.Unakuwa huna mipango inayosubiri hela.kwa hiyo
ukipata pesa ghafla,unafungua biashara au mradi ghafla unauendesha ghafla ,nao
unakufa ghafla.huna mipango endelevu
7.Kuiga kitu cha mtu ambacho hujui alivyoanza na
njia anayoipita.
8.Kupata taarifa potofu.Kuna watu huwa hawasemi
kweli kuhusu miradi au biashara zao.mtu anakudanganya alianza na mtaji wa laki
tano kumbe milioni tano.wewe unaingia kichwa kichwa.Au mtu anastawi magari
manyumba anakuambia ni kazi hihii ya kufuga kuku.kumbe ana yake.
9.Hatuna maono kutoka ndani yetu.hatujui
tunachotaka.tunabaki kusema nataka niwe kama diamond.
10.mfumo wa elimu ya nchi yetu.fikiria tanzania
nzima shule za serikali na binafsi wanasoma vitu vinavyo fanana kwa asilimia
kubwa.kwa hiyo kuna kuwa hakuna upenyo wa kuwaza tofauti.na mwanafunzi ukiwa
sio msomaji binafsi umekwenda na maji.
11.kutokuwa na mpango wa kupata kipato
endelevu.yaani kutaka hela kuendana na matumizi yaliyopo.Mtu unataka uajiriwe
ili upate hela ya kuoa.Hakuna mpango wa kuwa na fedha ya kutosha.Kwa hiyo
unaibukia tu fursa yoyote.(hand to mouth income))
12.Kuwazoea wateja na kukosa nidhamu ya kazi yako
Wengi wameibukia hizi fursa na hata wengine
kuchukua mikopo matokeo yake wamejikuta wanazalisha kitu kilekile na kutegemea
wateja wale wale.mwisho wa siku wakajikuta hawawezi kuendelea.Ninashauri
tufanye yafuatayo ili tudumu ktk ujasiriamali au ktk biashara kwa muda mrefu na
kutawala soko.
1.Kabla ya kufanya chochote,pata muda wa
kumuuliza Mungu.zaburi;32:8
3.Toka nje ya wewe.kile unachokiona ndani yako
,kitoe nje halafu kisimamie.huo ndio upekee wake.tuonyeshe uwezo wako .Fanya
kama vile uko peke yako duniani.na kumbuka huna kopy,hakuna anaefanana na
wewe.kwa hiyo hata siku moja usitafute kufanya kitu kinachofanana na wengine.
4.ISHI ukijua kuwa dunia
inahitaji ulicho nacho ambacho hatukijui bado.Hakuna mtu aliyeujua umeme mpaka yule aliyeuvumbua alipouvumbua.angekaa
kimya ingekuwa hasara kubwa.Na mwingine akaja akagundua umeme wa upepo bila
kujali wa maji upo.Na mwingine kagundua umeme wa betri bila kujali.Sasa wewe
mbona hutaki kutoa hicho kipaji chako????badala yake unataka kufanya ambavyo
tayari vimefanyika.TUPE NEW BRAND,KUFANYIA EDITING VYA WENGINE IMETOSHA.
5.Weka mipango yenye muda maalumu.fursa za msimu
pia ufanye,lakini usizitegemee.weka mipango ya kukaa sokoni pengine miaka hata
50 .Na kama hukusomea na unakipenda na unakiweza,ok.tafuta taarifa sahihi then
go for it!!!kweli kabisa ukibobea ni raha hata ugonjwa fulani unaweza
kuuchambua adi msikilizaji atasema una phd ya udaktari
Hivi unajua kuna watu hata bidhaa zikipanda bei
huwa hawajui.??yaani hawafeeel the pinch.kwa nini???kwa sababu wana kipato cha
kudumu na cha kutosha.Lakini ngoja soda ipande bei.wanalalamika mpa ulimi
unatoka.anatamani apimiwe hapo ya mia.🙈
Tunataka vitu vya tofauti.Tanzania inakutegemea
wewe kijana uje na mawazo ya tofauti ili tusonge mbele.Mungu alikusudia tuwe
tofauti ndio maana katuba tofauti jamani.cha ajabu badala ya kuvaa kama wewe,kuongea
kama wewe,kubuni kitu chako,kufanya biashara ya kwako,umebakia kuiga tu.kila
mtu anataka kuvaa kama p square.
Kila mtu anataka kusuka kama rihhana.
Obama ameibuka na yes we can.
Basi kila mtu utamsikia yes we can.
Ukimuuliza we can nini,anangaa mimacho.
BE YOU.REMAIN YOU!!!Hebu usiku wa leo jichunguze
upya maana kuna vitu Mungu amekuwekea bado hujavitoa ulimwenguni.Anza sasa
kutuambia wewe ni nani na una nini.