Katika kipindi hiki
kuna matukio mengi mabaya yametokea yakihusisha wafanya kazi wa ndani kama ndio
chanzo cha hayo yote, katika jamii watu hawa wamekuwa wakidharahulika sana na
wakati mwingine wamekuwa wakiitwa majina majina mabaya ya kudharauliwa. Hii
imepelekea kazi hii kuonekana ni kazi ya kawaida sana na haina thamani na kuna
mabosi wengine wamekuwa wakiwadharau sana na kuona ni watu wenye shida, dhiki
na umaskini mwingi. Hali hii imeibua tabaka kubwa kati ya mabosi na wafanya
kazi hawa na imezua migogoro ambayo wengine imeishia pabaya kwa kuacha alama
mbaya.
Aidha kuna familia
nyingine zimeishia pabaya sana pale ambapo mwanandoa mmoja wapo anapojihusisha
moja kwa moja kimapenzi na mfanyakazi wa ndani na wengine wamezaa nao, na kuna
wafanya kazi wa ndani wengine wamevunja ndoa za mabosi wao na wao kukaimu
nafasi hizo. Surah ii imelenga kukueleza namna njema ambayo unaweza kukaa na
wafanyakazi wa ndani.Wafanya kazi wa ndani
ni watu muhimu sana kwa kuwa wanasaidia sana majukumu ya familia kutendeka
kirahisi.
amna njema ya kuishi
na mfanyakazi wa ndani:-
1 1. Mfanye kuwa rafiki yako.
Jambo la msingi ambalo
unaweza kulifanya kwa mjakazi wa ndani kwako ni kumfanya kuwa rafiki. Yohana
15:15, Yesu anasema “siwaiti tena
watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo Bwana wake; lakini ninyi nimewaita
rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu”.
Njia pekee ambayo bosi
anaweza kukamata ukaribu wa mfanyakazi wake ni kumfanya kuwa rafiki, Yesu
anasema tumekuwa marafiki kwa kuwa tunashirikishwa ayatoayo kwa Baba yake.
Urafiki unaimarika pale kunapotokea ushirikishaji. Ukitaka kuukamata kwa
urahisi moyo wa mfanyakazi wako na akaanza kuishi kwa uaminifu kwako na akawa
kama ndugu ni pale unaanza kuishi kwa kumshirikisha mambo mengi uliyonayo na
unayoyapata.
Ukienda kuwanunulia
wanao nguo au zawadi naye pia mchukulie, unapowatoa wanao kwenda kutembea nae
pia mchukue, unapokula na wanao mezani nae pia kuleni nae, mfundishe mambo
mengi kuhusu maisha.Watumishi wengi
wanaangaika kufundisha watu nje ya nyumba zao lakini wale wa nyumbani hawajui
hata kama ni waalimu wazuri.
2. Faida
za wazi zitakazotokea kama kutakuwa na urafiki:-
- Atakuwa wazi kukushirikisha mambo ambayo hata wazazi au marafiki zake hajawahi kuwaambia.
- Atakuwa akifanya kazi zote kwa moyo wa kupenda na uhiyari na wala si ilimradi.
- Atakuwa akijituma kufanya mambo ambayo si kazi zake ila tu ni kwa sababu ajua anamsaidia rafiki yake.
- Kuna ujuzi ambao unao utaanza kuambukizwa ndani yake.
- Maono, tabia, na shauku ulivyonavyo vitaanza kuambukizwa ndani yake na atajiona anawajibu wa moja kwa moja wa kukuunga mkono.
- Atawatumikia watoto wako kwenye ngazi ya uzazi na hata kama haupo watoto wako hawataona kupungukiwa. Ataishi na upendo wa hali ya juu sana kwa watoto wako)
- Atakujali na kujali mambo yako na atafanikiwa kujua nini unapenda na atakutendea hayo ili rafiki yake uzidi kufurahi.
- Ataona anawajibu wa moja kwa moja wa kulinda na kutunza mali zako.
Epuka
kuishi naye kama mtumwa
Watu
wengi wamedhania kuishi kwa namna hiyo na kuwafanya wafanyakazi wao kuwaogopa
na kutetemeka wanapowaona huo ndo ufahari, wao hufurahi wakiona wamegonga
mlango sebuleni kila mtu akakimbilia ndani, na mbaya zaidi kuna familia ambazo
mfanyakazi wa ndani anakula jikoni anapopikia na haruhusiwi kula na watoto wa
bosi wake, hali hii ni mbaya sana, ebu yatazame mambo yanayoweza kutokea hali
kama hii inapotokea:-
- Anaishi kwa uoga, na hata akionyesha nidhamu inakuwa siyo halisi bali ni nidhamu ya uoga.
- Anaishi kwa wasiwasi kama mtu hasiye na makao na wakati wowote anaweza kuondoka.
- Hana raha na maisha anayoishi, anaishi kwa kuvumilia tu.
- Hana uhuru na kitu chochote kisicho miliki yake.
- Anafanya kazi zake kwa uogo ili asije kusemwa.
- Hana uchungu na miliki ya bosi wake kwa kuwa anaona kama haimuhusu.
- Anaweza kuishi nawe kama adui na akawatazama watoto wako kama watoto wa adui zake, na kwa kuwa hawezi kushindana nawe kuna uwezekano mmkubwa sana akajilipizia kisasi kwa watoto wako pale unapokuwa haupo.
- Ni nadra sana kutekeleza mambo katika viwango unavyovitaka kwa kuwa unavihitaji kwa kuwa haupo moyoni mwao.
3 3. Wape uhuru.
Mabosi wengi wanaishi na wafanya kazi wa ndani ila wamewafanya kutokuwa huru kabisa kwao. Na hii imepelekea wafanya kazi hao kutokuwa huru hata kama mambo yanawasumbua. Kila uhuru hakikisha uwe na mipaka ya kufanya na ya kutokufanya, uhuru hapa namaanisha katika mambo ambayo yanasababisha ustawi wa maisha yao katika upande wa kimwili na wa kiroho.
Mabosi wengi wanaishi na wafanya kazi wa ndani ila wamewafanya kutokuwa huru kabisa kwao. Na hii imepelekea wafanya kazi hao kutokuwa huru hata kama mambo yanawasumbua. Kila uhuru hakikisha uwe na mipaka ya kufanya na ya kutokufanya, uhuru hapa namaanisha katika mambo ambayo yanasababisha ustawi wa maisha yao katika upande wa kimwili na wa kiroho.
4. Mjengee maisha bora ya baadae.
Hivi utajisikia raha gani utakapokuja kuona baada ya miaka 10 ya kukaa na huyo mfanyakazi unapata taarifa kuwa ni tajiri sehemu Fulani na anakutaja kwa namna ulivyomsaidia kufikia hapo.
Ni mabosi wachache sana ambao wafanyakazi wao wanawasifia kuwa wamesaidika kufikia maisha bora baada ya kuishi nao, ila mabosi wengi huwa wanaangalia maisha yao tu. Jitahidi uangalie na maisha ya mfanyakazi wako kuwa atakuja kuwa na maisha gani baada ya kuishi nawe, mwazie yaliyo mema na mtendee yaliyomema ilia je kuwa na maisha yaliyo mazuri baadae.
Si vyema unaishi na mfanyakazi miaka hata 3 halafu anatoka hajui huko anapoena anaenda kufanya kitu gani, mfundishe ujuzi mbalimbali, katika kiwango cha mshahara unaompa kiasi kingine kidogo unaweza ukawa unamuwekea akiba hata benki na wakati mwingine unaweza kumfungulia hata biashara ndogo ya usimamizi mdogo ili tu aje kuwa na maisha bora ya baadae.
5. Kuwa mwalimu kwake.
Kuna mambo hayafahamu na ukweli ni kuwa amekulia kwenye mazingira tofauti na kuna tabia ambazo amekuwa nazo na kuna vitu ambavyo anaviamini na amekuwa akiviamini vitu hivyo, kama hautakuwa na moyo wa kialimu kwake kila siku utakwaza naye na wakati mwingine utajikuta unamlazimisha kufanya vitu ambavyo yeye haviamini ila atajikuta anafanya tu kwa kuwa wewe umesema.
Usipomfundisha akajua mitazamo na shabaha zako itakuwa ni rahisi na yeye kuendelea na utawala wa mfumo wa maisha yake na akajikuta anawaambukiza mpaka watoto wako tabia yake. Na ndio maana unaweza kukuta wanao walikuwa wanaenda vizuri sana ila tu alipokuja mfanyakazi tabia zao zimeanza kubadilika, hii ni kwa sababu watoto wanapenda kuiga sana na wakati mwingi wanaathririwa na wale waliokaribu nao.
Usidhanie kuwa yupo pale kwa ajili ya kukusaidia kazi tu, kumbuka na upande wa pili kwa ataishi na wanao kwa ukaribu na kwa muda wote ambao wewe haupo, kama hajui wewe ni nani, unaamini nini, na unashabaha gani lazima atajikuta anaingiza tabia yake kwa watoto wako. Wekeza muda wa kutosha katika kumuelimisha na kumvumilia katika hatua zote za kujifunza, ipo siku tu atakuja kufuzu vizuri.
6. Kuwa mlezi kwake.
Jambo jingine unaloweza kulifanya kwake ni kuamua kuishi naye kama mzazi mlezi kwake, ukifanya hivyo utamfanya ajione kuwa yupo nyumbani na atawachukulia wanao kama wadogo zake.
7. Onyesha upendo.
Kitu pia ambacho kitamfanya mfanyakazi wako kuishi vizuri nawe na watoto wako ni namna vile utakavoweza kumuonyesha upendo utakaomfanya ajisikie vizuri kwa ajili yako.
Mipaka ya mfanya kazi wa ndani
Maelezo yangu yatakuwa yamepungua sana kama sitojikita kueleza mipaka ya mfanya kazi wa ndani, familia nyingi zimeingia kwenye majanga makubwa kwa ajili ya kukosa mipaka ndani ya familia, ebu tutzame baadhi ya mipaka ya msingi sana kuwekewa vipaumbele katika ngazi ya familia:-
1. Mipaka katika shughuli za chumbani kwa mke na mume.
Naelewa kuna wengine hawatanielewa zaidi, ila kuna kesi nyingi sana zimeibuka nyakati za leo, unakuta mume analalamika kuwa mke wake kalala na kijana wa kazi au mke kulalamika kuwa mme wake kalala na msichana wa kazi.
Ni busara sana pamoja na hali ya kuwa marafiki kukawa na mipaka ya kuingia na kufanya shughuli za chumbani, shughuli za chumba cha wazazi ziwahusu wazazi wenyewe na si kumuongeza mfanyakazi wa ndani aanze kujishughulisha nazo. Kuna athari kubwa pia kama shughuli za mke zikafanywa na msichana wa kazi, inaweza kuibua dharau na wakati mwingine binti akaanza kujiona yupo sawa tu na bosi wake.
Sarah alipomruhusu Ibrahim azae na Hajiri, Hajiri akaanza kumdharau Sarah na kumuona sawa tu na yeye. Kuna mambo ni lazima muweke mipaka na usipoweka mipaka anaweza akaanza kuzoea zoea kwa ajabu. Si kila kazi unapaswa kumuachia mfanyakazi wa ndani eti kwa sababu unamlipa mshahara, kuna vitu vingine unajiharibia mwenyewe. Kwa mfano mke unataka chakula cha mmeo kiandaliwe na mfanyakazi, akipakue, amtengee na amnawishe huku nawe umekaa tu unasubiri nawe unawishwe kwa kuwa wewe bosi umeajiri. Hii tabia inapoteza taswira ya mumeo kwake na wakati mwingine umuhimu wako kwake unapungua na anagundua kuwa umuhimu wako ni kwenye masuala ya unyumba na tabia ukiikomaza kuna wakati ataona hata unyumba anaweza kuupata kwa msichana wa kazi na hapo ndipo ndoa uingia matatizoni.
2. Mipaka katika vitu vya kuangalia na kuvifanya.
Unaweza ukapata binti au mvulana ambaye anapenda kuangalia au kufanya vitu vinavyoharibu tabia njema, wewe kama mzazi na kiongozi muwekee mipaka ili ajue kuwa si kila kitu anapaswa kuangalia na kukifanya, hii itamponya yeye na watoto wako ambao wanashinda pamoja nae.
SIMULIZI
ZA KUKUJENGA KUHUSU WAFANYA KAZI WA NDANI
Nilivyonusurika
kufungwa jera kifungo cha maisha
Nilipomaliza kidato cha
sita nilikuwa na rafiki zangu ambao nilikuwa nikikutana nao kila siku jioni kwa
ajili ya ibada ya pamoja, wakati ule katika ushirika huu tulikuwa tukimuona
Mungu sana. Nilipenda kuwa karibu na watoto na hata kucheza nao kila nilipokuwa
Napata nafasi ya kufanya hivyo. Kuna mtoto ambaye alikuwa akiishi jirani kabisa
na eneo ambalo tulikuwa tukifanyia ibada zetu, nilipokuwa nikimuona nilipenda
kumbeba na kucheza nae. Siku moja nilikuja kupata taarifa za ajabu sana kuwa
nilikuwa nimemchezea Yule mtoto mdogo sana wa kike kwa kuchezea sehemu zake za
siri kwa vidole. Maana mtoto alishikwa na homa kali sana na walipompeleka
hospitalini kumpima wakagundua ugonjwa huo unatokana na kuchezewa sehemu zake
za uzazi kwa vidole.
Yule mama alimuamini
sana msichana wake wa kazi za ndani na alipomuuliza alikataa kabisa na akasema
hajui na wala hausiki kabisa na uharibifu huo, majibu yale yalimpelekea Yule
mama aamini kuwa ni mimi ndiye niliyemfanyia mtoto Yule mchezo ule mchafu na
aliposhauriana na marafiki zake wakahafikiana kuwa ni lazima waende kufungua
kesi ili nikafie jera. Mama Yule aliingiwa na chuki kubwa mno ya kunichukia,
ashukuriwe Mungu wa mbinguni akamsukuma Yule mama aje kuzungumza na mama
mwenzake ambaye ndiye mwenye nyumba katika lile eneo ambalo tulikuwa tukifanyia
ibada, ilikuwa ni taarifa ngumu kuaminika na hata Yule mpewa taarifa aliogopa
naye akaanza kupoteza imani nami kabisa. Ila walichopatana ni kuwa maadamu
tatizo doctor amerimudu kwa tiba ni bora wanihurumie tu kuliko kuniangamiza kwa
kunipeleka jera, waliazimia kwa pamoja kuwa kwa hali ya wazazi wangu kunipeleka
jera wangenipoteza na wangepoteza hatima ya familia yangu pia maana katika
familia nilionekana ni kijana pekee ambaye nimeanza kuchomoza mwanga wa
mafanikio.
Nilipozipata habari
hizi lilikuwa jambo gumu kuliamini na lilinitetemesha sana moyo wangu, na
kunifanya kupoteza ujasiri mbele ya mama Yule aliyeathiriwa mtoto wake.
Bwana
anifadhili katika janga hili
Wakati Fulani asubuhi
katika kipindi cha fuku fuku hili BWANA alishuka na akanitia moyo kuwa
nisiogope maana yeye amekwisha yamaliza yote na wala hakuna baya lolote
litakalo nipata. Nikapata amani kuwa limeisha ila nilikuwa nikitamani sana siku
Mungu afunue yote wazi ili ijulikane kuwa si mimi niliyefanya yale.
Ulipita muda kidogo
Yule msichana wa kazi alikuwa akipenda sana uasherati, na kuna mambo ambayo
alikuwa akiangalia ambayo yalikuwa yakimuinulia hisia ila alikosa sehemu ya
kwenda kutuliza hisia zake, ikamlazimu kufanya mchezo wa kumchezea mtoto Yule
ili kujiridhisha kihisia na alipenda kumfanyia mara kwa mara. Isingekuwa rahisi
kabisa kwa mzazi kujua jambo lile kwa kuwa akirudi kazini yeye alichokuwa
anauliza ni mtoto ameoga au amekula.
Isingekuwa rahisi
kumkagua mwanae kwa kuwa vitu alivyokuwa anavitaka alikuta vimefanyika vyote
kwa ustadi mkubwa. Ila daktari pekee aliona bora amchunguze mwili mzima ndipo
alipokuta tatizo hilo.
Nguvu
za Mungu za funua tatizo
Siku moja walikuta
binti ameanza kupagawa na mapepo na yalimzidi katika kiwango cha kugeuka na
kuwa kama chizi, walimpeleka sehemu mbalimbali kwa maombi, na alipokuja
kufunguliwa tu binti alianza kutamka siri za ajabu na akazungumza kwa wazi kuwa
yeye ndiye aliyekuwa anamchezea mtoto Yule. Hapa kweli BWANA alinitetea na
kuwadhihirishia kuwa sikutenda yale. Na alizungumza kuwa hata wakati wa mchana
huwa analeta wanaume mule ndani ili kufanya uzinzi nao.
Katika simulizi hii
waweza kujifunza kuwa kuna umuhimu wa wazazi kuwa karibu na watoto wao zaidi ya
vile wafanyakazi wa ndani walivyo karibu nao.
Mfanyakazi
wa ndani wakala wa shetani.
Rafiki usomaye kitabu
hiki, sijakusudia kuandika kitabu hiki ili nikutishe au nikufanye uwaone
wafanyakazi wa ndani ni watu wabaya.
Nikiwa kwenye huduma
mkoa Fulani katika nchi yangu Tanzania, nilipata simulizi kutoka kwa mwenyeji
wangu ilinibidi nitafakari kwa kina sana. Kama ibilisi anakutafuta na kutafuta
uzao wako jua kuwa anaweza kutuma hata wakala wake aje kuajiriwa kwako kama
mfanyakazi wa ndani, na akija aweza tumika kama wakala wa kuharibu ndoa,
kuharibu watoto wako, kuharibu uchumi wako na kila chema.
Rafiki yangu akanieleza
kwa kuna mama aliyeokoka alichukua mfanyakazi wa ndani na alipomchukua alikuwa
akimsaidia kufanya kila kitu kwa ufanisi na uharaka wa hali ya juu sana. Binti
Yule alipenda sana kufanya kazi na kila alilokuwa akilifanya lilikuwa likiisha
kwa uharaka na ufanisi mzuri, na binti Yule alipenda sana ibada, na alikuwa
anawasisitiza wanafamilia wale wawe wanaomba kila siku kabla hawajaenda kulala.
Jambo lile lilifanya
wanafamilia wampende sana na waone kuwa Mungu amewapendelea na kuwapatia
mtumishi wake mzuri aje kuwafanyia kazi za ndani, na walipokuwa kanisani Yule
msichana alipendelea kuimba pamoja na waongoza sifa. Loooh! Kumbe binti Yule
hakuwa na chembe chembe za Uungu ndani yake hata kidogo bali alitumwa na adui
kuja kuiangamiza ile familia na kuipoteza kabisa katika mstari wa ki-Mungu, na
kiukweli japo walifanya ibada na kila kitu kilionekana kinaenda vizuri ila hali
ya ulimwengu wa Roho ilikuwa ikiwabadilikia na kuna mambo walikuwa wakianza kuyashindwa
taratibu.
Siku rafiki yangu
anatembelea familia ile, Mungu alianza kumsemesha kuwa mtoto Yule ni wakala wa
shetani na hata vyakula vyake ni mauchafu tu japo kinauzuri na ustadi, na
wakati mtumishi yupo sebuleni mama mwenyeji kwa upendo akamtuma binti akaandae
chakula jikoni ambapo hata moto ulikuwa haujawashwa, alipoenda ndani ya muda
mfupi sana akawa amekoleza na kupiga chakula kizuri na kukiweka mezani, Yule
mtumishi Mungu akazidi kumsisitiza kuwa si chakula cha kawaida kile, ilibidi
iitishwe ibada ya familia muda huo.
Ilipoitishwa ibada
mtumishi akamwambia aombe, kwa kawaida hakukuwa na mtu anayeomba vizuri na
kunena kwa lugha kama Yule binti katika ile familia, alipoambiwa aombe
akawaambia wote wafumbe macho ili aombe. Wote wakafunika isipokuwa Yule rafiki
yangu, Yule binti akamsihi afunike macho ili aombe ila mtumishi akakataa
akamwambia aombe hivyo hivyo, kwa kujilazimisha akaanza kuomba ila alishindwa
kutamka maneno akawa anazungumza zungumza tu yasiyoeleweka na mwishoni akaanza
kumpigia kelele mtumishi kuwa anamtesa amuache, hapo ndipo mapepo yaliporipuka
na kuanza kujieleza yametumwa kuangamiza familia na familia yenyewe haikuwa na
habari na hilo, ilifurahi kupata rafiki.
Simulizi hii
itakufundisha kuwa katika uchaguzi wa wafanya kazi wa ndani ni busara ukamwomba
Mungu sana ili apate kukupatia kijakazi wa kusudi lake kwako. Na pia familia
isiyo na nguvu za Mungu ni kambi ya shetani.
Msichana
mchawi nyumbani kwa mama yangu.
Mama yangu ni mkarimu
sana haswa katika kukirimu wageni, tangu nakuwa nilikuwa nikiona wageni
mbalimbali wakiletwa nyumbani kwetu na mama huwapokea na humshawishi baba pia
kuwapokea na kukaa nao kwa kitambo.
Siku moja nikiwa
nyumbani kimapumziko nikitokea Dar es Salaam ambapo nimekuwa nikifanya kazi
zangu, wakati Fulani mama alinishirikisha kuwa kuna msichana amempokea na
anahitaji kazi na msichana huyu alikuwa hatokei mbali na nyumbani na pale
alipokuwa akiishi walimuondoa kwa kuwa waliogopa kuwa alikuwa mchawi na
walilalamika kuwa toka aanze kuwa katika familia hiyo mambo yao yamekuwa
yakiharibika, kwa tiketi ya wokovu wake mama akampokea na akaongea nae na
mwisho akamsihi ampokee Yesu Kristo na Yule binti alikubali kuipokea sara ya
toba, nafikiri ukiri wake ulitokana na hitaji lake la kupata mahali pa
kujihifadhi. Niliporudi jioni mama alinieleza kwa furaha kuwa binti Yule
ameokoka sasa na anatarajia kumtuma aende Dar es Salaam akawe mfanyakazi wa
ndani kwa Dada yangu (mtoto wa mama mkubwa).
Nilijikuta nakosa amani
na suala lile na ikanilazimu kumuita Yule dada nje nikae nae kumuhoji,
nilimuhoji sana na nikagundua kuwa alikuwa akitumika kichawi tangu akiwa mdogo
kwa kufundishwa na bibi na baba yake. Mwisho nikamuomba nimuombee ila alikataa
akasema akipombewa huwa anachoka sana na mwili unakosa nguvu, nguvu ya Mungu
ilipozidi kutanda katika lile eneo nikamwambia anyooshe mkono wake unishike
alikataa kabisa, ilinibidi kumuinua na kumpeleka ndani ambapo nilipofika tu na
kumshika alijikuta ameanguka na pepo zikianza kupiga kelele. Nikukumbushe kuwa
kama hakuna nguvu za Mungu utaajiri hata wachawi na utaona shida yake katika
utendaji kazi wao na ni lazima wafanye uharibifu.