✍AMUA KUBADILIKA



Moja ya vitu ambavyo watu wanapata shida ni Kubadilika.Kwa Mfano jana Kijana Jithamini niliwaambia kuwa Sasa tunapaswa kuhama kutoka watsap kwenda Telegram Lakini utashangaa Hawahami . unaweza kujiunga nasi kupitia link hii( http://ow.ly/W02z302FGkv) ambapo Inabeba watu  5000. Hii ni kuweza kuwafikia watu wengi ili waweza kupata maarifa.

Mtu Mmoja alisema kama Huwezi kubadilika hakuna kitu kitakachobadilika na Daima mabadiliko hayakwepeki.Ili ufanikiwe lazima ukubali kubadilika kutoka kwenye mtazamo hasi kwenda mtazamo chanya.

Wakati mwingine inakuwa ngumu kubadilika Hata kama Unapenda kubadilika. Mabadiliko hayaji ghafla Ni mchakato. Anza Kubadilisha Kile ambacho ni rahisi kubadilika huku ukifanya jitihada za Kubadili mambo mengine.

Kimsingi usipokubali kubadilika hakuna kitu kitakachobadilika Lakini mara tu utakapoamua kubadilika kila kitu kwenye maisha yako kitabadilika(if You change everything around  You Will Change but if You  dont nothing Will change ).

Kubadilika Huwa ni gharama na ndio maana wengi wameshindwa kubadilika .Nakumbuka haikuwa rahisi kwangu kubadilika na kuanza Kusoma vitabu na kuachana na baadhi ya vitu vilivyokuwa havina maana kwangu. Lakini ilifika Mahali nikasema Nahitaji kubadilika.

Ndugu, mabadiliko Ni yako binafsi. Usisubiri Yule abadilike ndo wewe ubadilike. Kama Unatumia muda ovyo amua kubadilika, fanya mazoezi ya kubadilika. Kama una marafiki wasiokupeleka kokote, amua kubadilika.


JYB- 0753836463