KANSA /SARATANI Na Dr Amenye


Leo nitazungumzia magonjwa ya Kansa au saratani kwa ujumla
Tumor kwa kiswahili sijui ni jina lipi sahihi Ila linamaanisha kutokea kwa uvimbe au tishu mpya mwilini ambazo sio za kawaida na hazina faida yoyote mwilini.

Tumor zipo za aina mbili ,Benign na malignant tumor.Benign huwa ni vimbe ambazo hukua taratibu sana,hazina uwezo Wa kusambaa mwilini na madhara yake hutegemea sehemu ya mwili ulipotokea huo uvimbe.

Malignant au cancer huu ni uvimbe au tishu zinazokuwa kwa kasi sana,husambaa mwilini na hatari sana kama hazitotibiwa mapema.Seli zote zilizopo mwilini zinauwezo Wa kubadilika na kuwa Kansa, hasa pale zinapozalishwa kwa wingi na mwili kushindwa kuzipunguza.

Mfano  kuna Kansa za tezi, ngozi, figo,INI, ubongo, utumbo, sehemu za siri, viungo vya uzazi, n.k.Kansa karibu zote zinatibika na kupona kabisa iwapo zitagundulika katika hatua za awali kabla ya kusambaa mwili mzima.

Vitu vinavyoweza kusababisha Kansa ni kama vifuatavyo;
  • Uvutaji Wa sigara ambao huchangia zaidi ya 22% ya vifo vya Kansa dunia kote
  • Uzito kupita kiasi
  • Kula mlo usio faa
  • Kutokufanya mazoezi
  • Unywaji Wa pombe kupita kiasi

Kuna baadhi husababishwa na maambukizi ya baadhi ya virus,mfano Kansa ya shingo ya kizazi,Kansa ya INI,Minyoo kama ya kichocho huweza kuleta Kansa ya kibofu cha mkojo.Homoni pia zisipokuwa zimebalance huweza kuleta Kansa kama za matiti, ovari au mfuko Wa kizazi.

Pia kuna kurithi chembe chembe ambazo huweza kuleta Kansa,mfano Kansa ya matiti.Mionzi unapoingia mwilini kwa wingi huweza kuleta Kansa kama Kansa za ngozi.Hivyo ni baadhi ya vitu vinavyoweza kuleta Kansa mwilini.

Dalili za kansa hutegemea na aina na sehemu Kansa ilipo.Baadhi ya dalili ni kama :
  • uvimbe usio uma
  •  kutokea kinyama sehemu ya mwili
  • kutapika dawa kama ni kansa ya tumbo
  • kukohoa dawa kama ni kansa ya mapafu au koo
  • kutopata choo au kujisaidia haja kubwa zenye damu,
  • kukojoa damu,
  • kutokea damu ukeni baada ya kufanya mapenzi kama ni kansa ya shingo za kizazi n.k

Ila hadi MTU anagundua dalili hizo wengi huwa wanakuwa wamechelewa,Inashauriwa kufanya check up ili kubaini kansa hizo zikiwa bado changa,mfano kucheki matiti,kucheki shingo ya kizazi, kwenda hospitsli pale uonapo kitu cha tofauti mwilini.

Kuna baadhi ya kansa ambazo hushangaza watu na wengine kufikiria uchawi,mfano kuna wanawake hupata uvimbe tumboni ambapo ukitolewa hukutwa una meno au nywele Ila ni tumor za kawaida
Tiba zipo nyingi kama upasuaji kutoa uvimbe, Tiba ya mionzi au dawa ( chemotherapy).

Jambo LA msingi kujua na kukumbuka kansa hutibika mapema zikigumgulika,ila zikisambaa huwa ni ngumu sana kuzitibu
Njia za kujizui ni kama chanjo mfano kansa ya INI,kuna chanjo ya hepatitis zinatolewa
  • Kuacha kinywa pombe kupita kiasi
  • Kujizuia na maambukizi za ukimwi
  • Kufanya mazoezi
  • Kutunza mazingira ili yawe salama
  • Kula mlo kamili na vyakula vilivyo salama
  • Kuacha uvutaji Wa sigara n.k

Uvimbe mwingine ambao maarufu ni fibroid ambao hupata wanawake hasa wale ambao hawajawahi kuzaa,hukua kma mimba na mingine huwa mikubwa kama mimba ya kujifungua.

KWA MASOMO YA UJASIRIAMALI NA AFYA JIUUNGE NA GROUP LA KIJANA JITHAMINI TELEGRAMA NA WATSAP 
0753836463 BUREE