Ninaitwa aneth gerana isaya nilizaliwa nasikia kama ninyi ndugu zangu lakini kwa bahati mbaya nikaumwa nikapata matatizo ambayo yalinipelekea kupoteza uwezo wangu wa kusikia ndio maana sasa mimi ni kiziwi lakini pamoja na Hali hiyo sikukubali kabisa kupoteza dira na Malengo yangu ya kusoma hadi chuo kikuu.
Kwanza kabisa namshukuru Mungu wa mbinguni maana ni kwa neema yake leo nipo hapa kuwapa ushuhuda huu kwa maana bila yeye nisingekuwa hapa leo nasema asante Mungu wangu wewe ni Ebenezer.
Pili namshukuru admin Joas Yunus kwa kutambua Thamani yangu kwenu akaona heri aniletee huku mnisikie nilipoingia humu nilikuta watu kumi tu nikamwambia kama unataka nisimulie jitahidi ongeza watu wafike 50 kwa maana nataka ushuhuda wangu unoe vichwa vingi na kweli tangu jana anasaka watu kwa juhudi na maarifa hatimaye mmefika 50na zaidi hongera admin kwa juhudi hii group litafika mbali.
Nawashukuru wazazi wangu pamoja na mimi kupata matatizo lakini walinipeleka shule ya viziwi tabora ambapo nilisoma darasa LA kwanza hadi LA saba shule ilikuwa special kwa wanafunzi viziwi hivyo sikupata shida sana na nikafaulu kwa alama nzuri zilizoniwezesha kwenda shule ya sekondari ruvu iliyopo mikoani pwani.
Bahati mbaya si kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga na form five badala yake nikapangiwa chuo cha ualimu sumbawanga.... Dhamira yangu ilikuwa ni kusoma form five halafu niende chuo sikutaka kabisa njia za mkato.... Nikafunga safari hadi wizara ya elimu nikawaambia wanipange shule yoyote ya form five wakasema haiwezekani kwa sababu hamna shule ya form five special kwa viziwi nikamwambia nipeni hivyo hivyo yakinishinda nitanyosha mikono narudi nyumbani.
Nikasoma kwa juhudi sana bila kujali mazingira magumu hivyo nilipomaliza form four pale nikawa kiziw wa kwanza kufaulu kwa alama nzur tangu shule ianze kupokea wanafunzi viziwi

Shule ya sekondari ruvu haikuwa maalum kama ilivyo tabora hivyo mazingira yalikuwa magumu kwangu mana tulichanganyika na wanafunzi wanaosikia mpaka nafika pale hakuna kiziwi aliyewahi kufaulu kwa alama za one two three zaidi ya four ya mwisho na zero hivyo tulikuwa kama wasindikizaji lakini mimi nikajisemea penye nia Pana njia japo mazingira magumu nitapambana mpaka kieleweke.
Basi wakanipa barua ya kwenda iringa girl kusoma form five..... Nakumbuka siku naenda kuripot nilikuwa na shemeji yangu na nilienda nimechelewa na siku nafika ilikuwa jumamosi tukamkuta mwalimu wa zamu alipogundua sisikii hapo hapo akaanza kusema mmh huyo ataweza kusoma kweli???? Shule yenyewe hajawahi kupokea viziwi wala haina walimu maalum bora arudi tu nyumbani hapa anapoteza muda tu... Yaani shemeji aliponiambia huyo mwalimu alichosema nililia kwa uchungu nikamwambia shem basi turudi home akasema wewe baki tu ukishindwa ndo urudi nikakubali
Basi nikawa nimepokelewa na kweli shule nzima nilikuwa kiziwi peke yangu tofauti na ruvu sekondari angalau kulikuwa na viziwi wachache... Pia no special teacher aise siku ya kwanza naingia darasani nilidata si mnajua walimu wa form five wengi wao wanapenda kufundisha huku mnaandika bila kuandika ubaoni hapo ndo nikaanza kukata tamaa siku ya pili sikurudi darasani ikapita wiki nzima siendi darasani maana nikajisemea nilijifanya ngangari sasa nimepatikana si bora ningeenda chuo cha ualimu duuu.
Ndugu zangu mkiona Hali tete hivi mjue neema inakuja nakiri sikutakiwa kukata tamaa hivi lakini it was out of my ability yaani lakini all in all momitress wa darasa akapata habari kuwa siingii darasani akanifuata akaniambia twende kwa mkuu WA shule kutafuta msaada tunaenda mwee mkuu WA shule nikamuona anasema haloooo haloooo hapa iringa girl niongee kumbe anawapigia wizara ya elimu akawambia yule binti kiziwi mliyemleta yamemshinda sasa tufanyeje? Wakamjibu next week Kuna ugeni toka wizarani kuja iringa so wangepita kuniona tukawa tunawait to meet na hao vibosile.

Hakika si watu wote watauunga mkono lakini wapo wengine watakuunga mkono kwahiyo washikilie wale tu Watakuunga mkono na wale wasiokuunga wawe challenge kwako kama sehemu ya kufikia mafanikio kwa sababu siku zote huwezi kupata mafanikio bila kupitia challenges tofauti and challenges always makes u grown strong.
Mhula wa kwanza nakumbuka nilishika Nafasi ya Nane kati ya wanafunzi sitini na Mhula uliofuata nikashika Nafasi ya Tatu! Na yeye alifaulu tulikuja kukutana naye udsm.
It gives me hope to looking forward..... Na nikakazana kadri ya uwezo wangu mpaka nikamaliza shule na division two two yangu mkononi pamoja na cheti cha ubora wa taaluma kwa heshima yangu niliwaomba wizara waanze kuleta viziwi form one kwani shule ilikuwa one hadi six wakakubali mpaka leo inapokea wanafunzi viziwi ikumbukwe kabla sijafika ilikuwa haipokei so am proud I opened a way for them.
Basi nikapata admission ya kwenda kusoma sociology aise baada ya kufika chuo siku ya kwanza naingia darasani si mnawajua maprofesa hawaandiki kabisa ubaoni nikastukia wenzangu wapo busy wanaandika notes huku profesa anafundisha kama vile mchungaji anavyohubir duu nitanyosha mkono nikasema nimadhinda nyuma kwa shida kabla sijakaa sawa nakutana na challenge hii tena aise I was very very disappointed.
Nikaenda hostel nikaanza kutafakari ikumbukwe friend yangu wa iringa girl yeye alijiunga udsm nikiwa second year so hakuwepo in my first year may be she could help me once again nikamkumbuka... I cry alone think what to do
Nikamwambia plz profesa help me akaniambia si nilikuambia hapa huwezi kusoma bora uende marekani nikamwambia kwa hiyo kila kiziwi atakayekuja hapa mtampeleka marekani? Kwanini msisaidie mimi ili kuwafungulia njia wengine? Akauliza sasa tutakusaidiaje? Nikawaambia ajirini mkalimani anisaidie kutafsiri darasani.... Seminar and group discussion akahema kwa nguvu akasema haya nenda tunalijadili
Nikaa mwezi mzima siendi class a new friend of mine akanifuata akaniambia Anne hapa utadiscontinue yaani ndo nilikuwa nasikia about this nikamuuliza kudico ndo nini akanifafanulia kuwa ukifeli hapa Hakuna kuendelea na masomo yewiii nikatoka nduki huyo hadi kwa profesa maboko.
Basi baada ya kama week moja kweli nikaletewa mkalimani.... Kwa mara ya kwanza tangu chuo cha udsm kianzishwe nikawa kiziwi wa kwanza kabisa kusoma pale Tanzania na mkalimani
Tangu hapo nikawa naingia darasani bila matatizo yaani nikadhiriki kikazi life nilipofika second year chuo kikaongeza mkalimani mwingine nikawa nao wawili life at the University ikawa easy nikasoma hadi nitamaliza degree yangu kwa ushujaa.
Mpaka nimemaliza chuo mwaka 2009 baada yangu Kuna viziwi wawili, walinifuata wao walisomea education na walitumia wakaliman niliowaandalia mpaka sasa wapo wengine watatu so am proud again to open the door for them.
Wapendwa nilimaliza chuo 2009 na degree yangu mkononi mie huyo mtaani kusaka kazi... Kama ilivyo kwa magraduate wengi mara mmalizapo chuo mnavyopata shida wakati wa kusaka ajira nami ilinitokea kabisa pengine naweka kusema kwenu watu wa kawaida ni nafuu zaidi yangu kwa sababu waaajir wengi waliogopa kuniajiri kwa sababu sisikii na walijua kabisa ili waniajiri lazima kuajiri na mkalimani pia so walikwepa gharama.
Sitasahau niliona tangazo LA kazi sifa zote zilizotakiwa nilikuwa nazo kabisa ilikuwa ni kampuni binafsi.... Nikaandika barua yangu ya application kwa raha zangu na kuambatisha vyeti vyote vya taaluma basi siku moja nipo home sina hili wala lile gafla nikaona missed call kwa simu yangu nikatimua kumuomba mtu mmoja anisaidie kupokea simu kwa maana nisingeweza kupokea mwenyewe as sisikii yule mtu akasema Kuna sehemu unaitwa interview nikaamua kuongeza vocha kabisa nikamuomba awapigie tena wambie mimi sisikii lakini nitaenda mwee wakauliza aha kumbe husikii JIBU yes wakajibu basi basi usije yewiii niliishiwa nguvu nikasononeka sana.
Nikamuomba sana Mungu anipe ujasiri wa kufanya kitu katika maisha yangu kiwe suluhisho LA kuhangaika huko na kule kusaka kazi bila mafanikio..... Basi nikajikaza sikuwa na hata senti moja tuseme niite mtaji.Hebu na wewe mwenzangu jiulize maswali haya halafu tafakari.
Mwaka 2009 tangu nimalize mwezi wa November ilikuwa mwezi miwili iishe na tukio hilo lilitokea ndani ya hiyo mwezi miwili.Mwaka 2010 January niliendelea kutafuta kazi bila mafanikio nilituma karibu application Mia lakini wapi.... February 2010 nikakaa chini na kutafakari, nikajisemea nguvu ninazo, elimu ninayo, maarifa ninayo, ujuzi ninao sasa kwa nini nihangaike kiasi hiki kutafuta kazi???? Nitatafuta mpaka lini? Na nilipopata nitakalisha matako nyumbani kuwategemea ndugu na wazazi hadi lini??????
Nikamuomba sana Mungu anipe ujasiri wa kufanya kitu katika maisha yangu kiwe suluhisho LA kuhangaika huko na kule kusaka kazi bila mafanikio..... Basi nikajikaza sikuwa na hata senti moja tuseme niite mtaji .Hebu na wewe mwenzangu jiulize maswali haya halafu tafakari
Yaani hatukuwa na ofisi na hela yoyote ya kufanya process za kuandaa katiba na nyaraka kwa ajili ya kusajili ili tufanye kazi kisheria si mnajua donor wengi ili wakupe msaada lazima usajili na uwe na ofisi maalum

Nikaamua kuwakusanya wanawake viziwi wenzangu ambao hawakuwa na elimu wala ajira kabisa mwenye Elim nikiwa mimi pekee yangu... NikawAmbia mimi mwenzenu nimemaliza chuo lakini sijabahatika kupata kazi Lakin nina kitu nataka kuwafanyia ili kuwakomboa pamoja na kujikomboa mwenyewe.... Huo ndo ukawa mwanzo wa asasi ya furaha ya wanawake wajasirialiali kwa viziwi Tanzania, FUWAVITA I am the founder and director of that ngo mnataka kujua nilianzisha vipi bila kuwa na senti mfukoni????
Mwanzo nikaandaa katiba nikiwa home na nembo halafu nikawaita wenzangu tunajadili wakaongeza nyongeza nikaadd... Baadae nitatafuta wadau nikawaambia azima yangu ya kufungua kampuni si haba wengi walivutiwa na idea wakachanga tukapata hela ya kufanya process za katiba pia tukachangachanga kidogo kila mtu alichokuwa nacho tukakamilisha usajili.... Nitaenda kule kwa afisa kama mtaa wa sigara kule ipo sehemu za machimbo kama mnapajua kwa sababu kipindi hicho nilikuwa naishi mitaa hiyo nikamuomba atuunge mkono atakubali akatupa kaofisi kidogo na kiti na meza hapo ndipo tulipoanzia.
Yaani hatukuwa na ofisi na hela yoyote ya kufanya process za kuandaa katiba na nyaraka kwa ajiliya kusajili ili tufanye kazi kisheria si mnajua donor wengi ili wakupe msaada lazima usajili na uwe na ofisi maalum.Pia tukahama toka mtaa wa sigara tukaenda sinza afrikasanaa tukanunua meza viti laptop.... Na kulipia kodi ofisi yetu mpya.
Kifupi asasi ya fuwavita na juhudi zangu imeniwezesha kufahamiana na kufahamika kwa watu mbalimbali na hivyo inakuwa easy kupata sapoti baadhi ya matukio. Yote haya nisingeshiriki ni kupitia fuwavita.Yote haya ni kupitia fuwavita
Ndugu zangu mmeoona???? Hakika hakuna kisichowezekana chini ya jua ukimtegemea Mungu na kuwa na dhamira yakinifu.... Nawaomba msilie eti hamna ajira,,,,, hamna mtaji,,, hamna pa kuanzia...... Vyote hivyo unavyo wewe mwenyewe hapo ulipo kwa hiyo kuanzia leo amka Anza kuchakarika.... Pika chapati,, kaanga karanga na hata kuuza maji mwaka huu ulete mabadiliko unalipa kijana mwenye nguvu na maji bado yanatiririka mwilini.... Tunataka pose lako mtandaoni liwe for the reason sio unaishia kulike za watu jiulize wa ngapi wanalike zako? Mtu akipita page yako akasema ahaa hapa Kuna jambo mhimu..... At the end of the year utuletee ushuhuda hapa umefanya nini in 2016.
Yaani niliendelea na fuwavita.... Juhudi zangu na exposure,,, experience I got fuwavita zilisababisha nipate ajira yangu ya kwanza kabisa bila kutafuta sana katika kampuni ya Tayoa ipo mikocheni kama data management and on line counselor.... Mkurugenz wa Tayoa alivutiwa na juhudi zangu akaniajiri lakini sikuiacha fuwavita niliendelea kuwa nao bega kwa bega huku niko Tayoa.
Nimefanya kazi Tayoa miaka mitatu kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2013.Hapa nilikuwa Tayoa. Nikiwa Tayoa I got married to Mr bill in 2011.Blessed two babies Baraka and Betty.
Mwaka 213 July nikapata ajira mpya serikalini kama afisa maendeleo ya jamii.....
Nilianzia sengerema mwanza nikafunga safari hadi sengerema... Nimekaa mwaka mmoja na nusu halafu nikahamia ilala municipal . mwaka 2014 July nikahamia ilala municipal to the same post of CDO. Then mwaka huu January nimehamia wizara ya jinsia na watoto ambapo nipo hadi leo nahuku naendelea na fuwavita iliyonitoa mbali.