SABABU KUMI ZINAZO KUFANYA USISONGE MBELE ~Joas


Wakati tukikuta mambo yetu hayaendi huwa tunadhani kuna mchawi anaiingilia mambo yetu kumbe mchawi wa mambo yetu ni sisi wenyewe  na si vinginevyo .

Zifuatazo ni sababu kumi zinazokufanya usisonge mbele :

1.Huna ndoto : Kama hujui unataka nini katika maisha yako wewe utakuwa ni mtu wa kusubiri Jua lichomoze na kuchwa .Hutakuwa na msukumo wa ndani wa kuhakikisha kuwa siku moja ndoto yako inakuwa kweli .Umekuwa ukifanya vitu kwa mazoea kwa sababu huna ndoto yoyote inayokufanya kuwaza kila siku namna gani utaifikia.

2.Unawasikiliza watu sana kuliko kujisikiliza mwenyewe:Maisha yako ni yako na si ya kaka yako wala mjomba wako au ndugu yeyote na rafiki yeyote uliye naye . Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe(Every body will carry his own burden).Kama unaamini katika unachokifanya na unajua kitakufikisha mahali endelea kufanya kadri unavyoweza .Watu wengi si wazuri na hawajui unakokwenda japo wanaweza kujua ulikotoa .

3.Hutafuti Maarifa : Bila maarifa hutaenda kokote na maisha yako hayatabadilika .Utakuwa kama mtu anayepiga ngumi ukutani ambapo mwisho wa siku huumiza mkono wake mwenyewe .Kama siyo msomaji wa vitabu ,kuperuzi kwenye mtandao kutembelea blog kama www.kijanajithamini1.blogspot.com na www.maishanamafanikio.blospot.com hautaweza kupata maarifa ambayo yatakufanya ufanye mambo yako kwa uwaredi mkubwa na kwa tofauti .Utakuwa ni mtu wa kufanya mambo kimazoea maana huna maarifa na mwisho wa siku hutatoka pale ulipo.

4.Unajihurumia sana : Umekuwa mtu wa kujihurumia sana na kutaka kukaa kwenye comfort zone ,sehemu ambayo unapata vitu kwa urahisi .Hutaki  kuumiza kichwa na kuwaza juu ya maisha yako .Umekuwa mtu wa kutaka vitu ambavyo vimeshafanywa na wenzio maana hutaki kuteseka  na kukutana na changamoto .

5.Unaishi kwa yaliyopita : Maisha siyo jana maisha ni kesho .Kama ukiangalia ulivyoshindwa jana hutafikiria kuhusu kesho .Ukiangalia biashara ya jana ilivyodhurumiwa na kuibiwa hutafanya biashara kesho .Acha kabisa kuishi kwa ya jana hutasonga mbele .Angalia sana kesho yako , Maisha ya watoto wako wa kesho ,mahusiano na familia yako ya kesho na si vinginevyo .

6.Huchukui hatua : Umekuwa mtu wa kusema nitafanya kesho na kesho ikifiika hufanyi .Umekuwa na mipango mingi isiyokuwa na utekelezaji .Kama huchukui hatua utabaki hapo hapo ulipo  hakuna jambo jipya litakalotokea .

7. Unasubiri Matokeo ambayo hujafanyia kazi ; Usitegemee muujiza .Kile apandacho mtu ndicho atakachovuna .Unawezaje kuvuna mahali ambapo hujapanda??? Hey ! Unawezaje kuvuna maharage kwenye shamba la mahindi???? .Newton anasema ili kazi ifanyike lazima kani (force) itumike na umbali(distance ) uwepo .Hakuna matokeo yasiyosababishwa.

8.Huzalishi mawazo : Umekuwa mtu ambaye hutaki kuwaza kwa mtazamo mpya na kuzalisha mawazo mengi kadri iwezekanavyo .Umeishi kwa wazo la mwaka 1999 mpaka leo na hujui kama dunia imebadilika .Hey! Amka anza kuzalisha mawazo .

9.Umeishi kwa tahadhari nyingi :Kila kitu kwako umechukua tahadhari ,unahisi ukianza biashara fedha zako zitapotea ,unahisi ukianzisha kitu hakitasonga mbele .Kwanini umekuwa hivo (too cautious) ????.Kama hutaachana na tabia hii hutatoka mahali ulipo na kamwe usitafute mchawi .

10.Hujifanyii tathimini :Huna tabia ya kupima yale uliyoyafanya kwa siku,wiki,mwezi na mwaka na hivyo unahisi kama unaenda mbele kumbe unarudi nyuma .Ni muhimu ukawa na tathimini yako binafsi katika mabo yako

JYB(0753836463)