Siku moja nikiwa kwenye pitapita
zangu ,nikaingia stationary moja na kumkuta mama mmoja ambaye ndiye mmiliki wa
ile stationary akiwa na mfanyakazi wake.
Kwa kuwa nimezoeana sana na yule
mfanyakazi wa stationary nikamtania kidogo kwa kumwambia,"kwanini hutaki
nikuoe", ghafla yule mama akasema,*mmmmh vijana kama mnaoa oeni tu ila kwa
kijana atakayeoa kwangu lazima ajishike*, nikamuuliza kwanini anasema
hivyo?ndipo akanambia ushuhuda wakati anamuoza binti yake,na ilikua hivi;
Mama:Hivi mwanangu umempendea
nini binti yangu? Maana kwa dini yetu tunaangalia vigezo kadhaa kama
vile;uzuri,tabia na mali?
Kijana: mwanao sijampendea kwa sababu ya elimu yake
bali kwa tabia yake na uzuri pia.
Mama: basi kama ni hivyo mke umepata lakini sikupi
elimu yake wala elimu yake,fahamu kabisa mshahara wake na kazi yake havikuhusu
kabisa. Kama masharti huyawezi basi muache mwanangu.
Duuuuh!!!!!! Maneno yalinichosha
sana nikakumbuka imeandika mtu atawaacha wazazi wake na ataambana na mumewe au
mkewe, nikajiuliza mengi sana je!!hii ndoa itakuwaje huko ndani maana
yawezekana binti atakuwa na mafundisho ambayo ni matango pori,na ndoa itakuwa
kama matangori.
Ikiwa mke au mume atakuwa hana
maamuzi binafsi juu ya ndoa yake au uchumba basi mtu huyo atawaliwa na wazazi
na madhara yatakayo tokea ni;
1:Atawaza kujenga au kuboresha
kwao na kusahau kwamba anapaswa kujenga kwake yaani kwa mke au mume wake maana
hao wameambatana .KUAMBATANA ni
kuunganisha,kuleta na kukusanya pamoja maono na mipango yenu kwa ajili ya ustawi
wenu ,hivyo ikitokea unawaza sana kuhusu kwenu basi ilipaswa ubaki kwenu.
2:Hatokua na siri yoyote kwa
wazazi,kila kitu anachopitia katika ndoa au uchumba vyote atakuwa anamimina kwa
mzazi wake.Ndugu usiombe upate mtu wa namna hiyo .
3: Hatokuwa na maamuzi binafsi
mpaka wazazi wamesema ndio.
Ni aibu kubwa sana kwa binti
akiambiwa na mchumba wake mipango ya maisha au na mumewe hajibu mpaka ameuliza
mzazi wake,halafu la mzazi na linashupaliwa kuliko.Hivi kwani huwezi kujiongeza
?najua ni mzazi wako lakini yeye alishamaliza yake hivyo fanya yako kwa
utaratibu unaokubalika.
Numalizie na hadithi kukikuwa na
mama mmoja ambaye akikuwa anafanya kazi BOT na ikatokea akamuoza binti yake
lakini yule mama alikuwa ni wa kufuatilia kila siku,utasikia mwanangu umekula nini,unashiba
kweli,kama yanakushinda njoo nyumbani haukufukuzwa na mengineyo mengi.
Je !mzazi apaswa kufanya hivi? Je
siku wakifa itakuwaje sasa?
Laban Nzelela
0656574760