Una mwaka mmoja kwenye mahusiano
na umeanza kujisikia kuvunja mahusiano yako? Ule upendo wa mwanzo. Uliokuwa nao
unaonekana kuyeyuka?,maneno na lugha tamu za mwanzo ndo zinakufanya uhisi
kuvunja maana unahisi upendo hakuna ?
Daaaah! Mbaya sana kwa kasi
uliyoanza nayo kwa sasa unahisi huwezi kuendelea tena? Au unahisi
ulikurupuka?
Maswali mengi unaweza kujiuliza
na kujiuliza tena mara kadhaa na hata moyo wako kusongwa na hofu na ile hofu
inakupelekea kujisikia hivyo unavyojisikia.
Kuna kipindi nilipitia katika
wakati kama huu,na haikuwa rahisi kwangu kuamua kuendelea mbele na mahusiano
niliyokuwa nayo maana nilikuwa napambana katika ufahamu wangu na kila kukicha
naona warembo wengine tena ni wazuri kuliko niliyenaye hivyo nilipita.Lakini
kwa sasa nimekuwa sawasawa katika mahusiano yangu na nayafurahia kwa sasa.
Mpenzi msomaji wa makala hii
labda niseme tu ,"kadri gari linavyopanda mlima ndivyo hata mlio wa gari
hubadilika na hubadilika kwa sababu safari inakaribia kuwa nyepesi si muda
litafika kwenye njia nzuri na kurudi kwenye mlio wake wa kawaida",
NINI UFANYE UNAPOFIKIA HAPO?
Kuna mambo yanaweza kuchangia
hali hii lakini unapofikia kwenye dilemma kama hii yaani uache au
uendelee?,fanya hayo yafuatayo;
1:Heshimu maamuzi yako
Kwanini nasema kuheshimu maamuzi
yako? Iko hivi watu wengi wamejikuta wakiyasaliti maamuzi yao na pia wakiacha
sintofahamu katika jamii zao,kutoheshimu mawazo wako ni "sabotaging"
yaani unajihuhujumu mwenyewe,hata mfanyabiashara ambaye anataka kufanikiwa ni
lazima awe na uwezo wa kuheshimu maamuzi yake.
Sababu inayoweza kupelekea
maamuzi yako kubadilika ni yale unayoyaona sasa aidha inatamani wengine au
udhaifu wa mwenzio,au ushauri kwa watu wengine.Kama ulichukua tulivu kutaka
kupata mwenza wako kwa ajili ya ndoa nina hakika yalikuwa maamuzi ya
hakika,huwezi ukasikia upendo umekufunika nyakati zote,mahusiano ya kwenye
tamthilia si yako,imekupasa uyaishi ya kwako,uyatengeneze yako ili ukajivunie.
2:Tumia mapungufu unayoyaona kama nafasi ya kuonyesha upendo wako.
Mtu mmoja alisema ,"you will
never find a perfect woman or man" na mimi nasema if you want a perfect
lover,be that lover".
Mpenzi wa kweli anatengenezwa na
mwenzi wake,tell your lover what you him or her to be,otherwise you will be
breaking every courtship you establish and finally you will to be problem to
your life.
3:Mueleze kwanini ulimchagua yeye miongoni mwa wengi.
Achana na kufumbia macho vitu
ambavyo hukumkuta anavyo na ghafla alipokuwa nawe akaanza kuwa navyo,yawezekana
anafanya vile akidhani utavutiwa zaidi kumbe ndo anakupa maswali zaidi kuhusu
yeye kama ni mtu sahihi kwako.
Jizoeze kumwambia kila wakati hii
itakusaidia kukupa amani na faraja na hata yeye atasema laaah!kweli nina mwenza
wa ukweli na sio kila jambo unakuwa unajifanya unalikubali kumbe hata sivyo.
4:Zungumza na mwenzi wako kwa hatua mliyofikia na mnapoelekea.
Kama kuna jambo la msingi katika
mahusiano ni hili kwa sababu huwezesha kujua mmefanikiwa kiasi gani,hii ni
tathmini,huwezi kufika mahali ukafurahia ikiwa hakuna muda wa kutathimini kwa
kiasi mmeweza kufanikiwa hasa katika malengo ya pamoja na yale ya binafsi.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo
ukiyafanya yanaweza yakakuokoa katika hali hiyo ni muhimu sana kuyafurahia
mahusiano yako na palipo na furaha hapakukosa kuparuzwa kwanza.Usikubali
mazingira ya nje yaharibu mahusiano yako maana ni eneo la kutengeneza sura ya
maisha yako ya baadae.
Laban Nzelela
065654760