Waswahili walisema kinga ni bora
kuliko tiba tena wakaongeza kusema usipoziba ufa utajenga ukuta wakiwa na maana
endapo jambo la kwanza likitiliwa mkazo basi la pili halitatokea na kama la
pili litatokea basi gharama yake ni kubwa na inauma kuilipa.
Kwa dunia yetu tuliyonayo kwa
sasa mambo mengi yamerahisishwa,nakumbuka enzi ninakua kumpata msichana ili ni
ngumu ilikuwa inabidi ujipange tena na kupiga misele karibu na kwao hata mara
tatu kwa siku huku ukiwa na pamba za kuazima.Nakumbuka jeans yangu ya mikasi
maana ilikuwa inanisindikiza na tena nilipoambiwa nisubiri palepale kwa siku
zote mwanaume nilikuwa sibanduki mpaka mtoto amekuja,kwangu mimi naiona ilikuwa
gharama sana tofauti na sasa ukitaka mrembo ni haraka tu unampata,ukiwa na
smartphone ndo kabisa umemaliza maana hakuna haja ya misele.
Mnapokuwa mmekubaliana kuwa
kwenye mahusiano yenye lengo la kuwaunganisha kama wanandoa hapo baadae ni
sawasawa na mwanafunzi anayesubiri mtihani sasa basi ili afaulu kunategemea
sana nini anafanya kwa ajili ya mtihani ulio mbele yako vivyo hivyo katika
mahusiano mnavyoishi leo ndivyo mbele mtakavyokuwa,msitegemee furaha katika
ndoa ikiwa leo mnagombana tena mara kwa mara.
Nia kuishi kwa furaha katika
mahusiano yako leo kwa ndoa yenye furaha,zifuatazo ni kanuni chache zinazoweza
kukufanya ufurahie mahusiano yako;
1Usihangaike kufuatilia nyendo zake.
Kwanini usihangaike? Ni kwa
sababu hakuna mwanaume au mwanamke anayeweza kubadilika kwa kufuatiliwa kwa
lugha pendwa usimchunguze.Utakuta mwingine anamfuatilia mpaka kwenye mitandao
ya kijamii ili aone anakuwa hewani masaa mangapi.Kwa mtindo huu huwezi kumwamini
na kama utamwamini basi ni kwa kuchelewa na ushaumiza akili kumbuka kumfuatilia
hakumfanyi kuwa mwaminifu.
2: Nidhamu ya mawasiliano.
Kuna wengine wakishaingia kwenye
mahusiano basi ni kila sekunde,kila dakika wako wanawasiliana tu,japo si mbaya
ikifanywa kwa nidhamu ila zingine zinazidi.Yawezekana mwenza wako yuko kazini
na kazi zinahitaji utulivu sasa mara griiii griiii kwa wengine sijui ila kwangu
naona ni kero.ikifika hatua ya kuulizwa ulikuwa unaongea nani? Hebu niulize
ulitaka ukipiga ukute niko huru tu au simu nilinunua kuwasiliana na wewe tu?!
Daah! Tulia mpe nafasi ya kufanya mambo ya maisha huku mkifanya mawasiliano
yenye tija.Uzuri wa mahusiano ni kusikia kile ambacho hakijasikiwa sio kila
wakati ni hichohicho tu.
3: Usithubutu kumtaja taja ex wako.
Kwa moyo wangu kiukweli nikisikia
mchumba wangu anamtaja ex wake mara kwa mara siwezi kufurahia tena nitajiona
kiraka yaani nimepachikwa tu,mimi sijapendwa ila anajifariji tu kwa machungu ya
ex wake.loooh!mwenzangu kaa kimya maana huwezi jenga nyumba mpya kwa msingi wa
zamani au ghorofa kwa msingi wa tope.
4:Msile kabla ya kunawa.
Kwa ustaraabu wa kawaida
anayestahili kula chakula kinapokuwa kimetengwa ni yule aliyenawa,kama
umeshahudhuria misiba wanaopewa chakula ni wale walionawa;Ni kosa kutenga
chakula kabla ya maji ya kunawa na endapo utafanya hivyo basi huduma yako
haitafurahiwa.Kula kabla ya kunawa ni kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa.
Rafiki yangu mmoja alinambia
baada ya kudumu kwenye mahusiano kwa miaka kama miwili wakajikuta wamekutana
kimwili,tangu siku hiyo akawa hana furaha na mchumba wake,nikamuuliza kwanini?
Akanambia ni kwa sababu nimemtenda Mungu dhambi hivyo sifurahii tena kuwa na
yeye lakini pili ananitia wasiwasi kwani kila akiniona anataka tufanye sasa
mimi nikiwa mbali na yeye nani anamtimizia? Mwishowe hawa watu waliachana
kabisa.
Kwa hizo chache furahia mahusiano
yako,zingatia ili upunguze uwezekano wa kuumizwa.
Laban Nzelela
0656574760