MKANDA WA USALAMA ~ Laban Nzelela


Kwa dereva anayezingatia na kuheshimu taaluma yake,vilevile ambaye hataki kutoutendea haki haki muda alioupoteza alipokuwa kwenye mafunzo yake ya udereva ni lazima afunge mkanda wa usalama anapoingia ndani ya gari kwa ajili ya safari.

Nenda kwenye interview yoyote ya makampuni ya usafirisha wa abiria au mizigo nenda  na vyeti vyako pamoja na leseni yako ya daraja la ngapi huko,lakini ukithubutu kuwasha gari na kutia gia kabla hujafunga mkanda itakuwa imekula kwako,si kama hujui kuendesha gari hapana unajua ila kosa lako hufuati kanuni.

Unaweza ukawa dereva mzuri lakini usijue kulitumia vyema gari,hebu fikiria maisha ni yako lakini umewekea traffic police wa kukusaidia kutumia gari lako kwa kufuata kanuni hali kadhalika utumie barabara vizuri.

Unapoingia kwenye mahusiano ya uchumba kanuni ya mkanda wa usalama ni muhimu,ili usilipe faini mbeleni kubali kufunga mkanda,kwani utakapofunga mkanda hautakuwa na uhuru wa kufanya kila kitu kama ilivyo dereva akifunga mkanda si rahisi kuinama na kuokota kitu chini ya uvungu wa kiti.

Vijana wengi tunaingia kwenye mahusiano na kuipuuzia kanuni hii matokeo yake tunapigwa mkono na askari,ndinga tunapaki pembeni then tunalipa faini.
Nani anastahili hukumu kati ya dereva na askari anayesimamia kanuni?,ukijiona umeonewa utakuwa mtu wa kunung'unika tu ili hali wew ndo umevunja kanuni.

Nina maana gani hapa? Kwa taarifa yako hakuna wachumba ambao hubaki na furaha mpaka ndoa isipokuwa wale ambao hawakukutana kimwili,yaani hawakusahau kufunga mkanda wa usalama,kwani wale wote ambao hufunga mkanda hata gari ikiyumba hawezi toka kwenye kiti na kwenye uchumba ni hivyo hivyo si wakati wa kujiachia kwani endapo utajiachia utakwisha tu.

Mahusiano ni kama probabation period yaani wakati wa mtu kuthibitishwa kwamba ndiye au siye,waulize wafanyakazi kama mimi katika kipindi unakuwa mchapa kazi ili mradi uthibitishwe kuwa mwajiriwa,sasa mwenzangu na mie ile kuambiwa nitakuoa au tutaoana tayari mnakuwa wanandoa kabla hata ya harusi.

Halafu unategemea kufika mwisho kirahisi heeeeee!church boy wako radhi kula na kufuta ili usimsumbue mbeleni kwani hatakuwa na furaha sana kwa sababu ya kuangukaz,church girl usilalamike kisa jamaa kapita halafu hana habari na wewe ,si yeye ni nyinyi mlijiachia mkatumia barabara vibaya kanuni ya cause and effect ikapitia hapo na faini yenu yaweza kuwa kutofika mwisho.

Akija anayelia kwa sababu ya mahusiano just muulize ulifunga mkanda wa usalama? Na kama ndio itakuwa kazi rahisi kumshauri kwani utadeal na tatizo la kupotezewa muda na wala si lile la kujuana kimwili.

Hakuna msafiri aliyeamua kushuka kwenye gari na kutembea eti kwa sababu bus linachelewa,na kila mwenye maono husubiri na kama hakuna subira hana anachoona mbele.Mkimuona mnatengenezeana mazingira ya kukutana kimwili ni dhahiri hamna mnachosubiri simple and clear no future ahead.

Team leader

FTF