Huwa kila siku nakutana na vijana wengi
wanajiuliza maswali haya :
- Hivi mimi nitaweza kukutana na Mengi?
- Hivi mimi nitaweza kukutana na Manji?
- Hivi mimi nitaweza kukutana na Bhaharesa??
Ukweli ni kwamba kuna mwanya(gap) kubwa
kati ya tajiri na maskini na hapo ndipo kunatokea ugumu wa maskini kukutana na
tajiri na mwisho watu huishia kuwaona kwenye runinga na kamwe hawewezi kuonana
na matajiri uso kwa uso na kujadili mambo .
Rafiki yangu Kashindi Edson mhitimu wa
Chuo kikuu cha Dar es salaam kwa mwaka huu sehemu ya DUCE jana nilikuwa naongea
nae akasema kuwa daima mstari unaomtenganisha Tajiri na maskini ni
mwembamba sana japo imekuwa vigumu kwa
tajiri na maskini kukutana .Nilivyomuuliza ni wapi sasa maskini na tajiri
watakutana na kwa namna ipi alishindwa kunijibu .
Badae nilipata majibu yangu binafsi na
nikayaamini .Sehemu pekee ambapo tajiri na maskini wanapaswa kukutana ni kwenye
"wazo".Kama una uwezo wa kuzalisha wazo lenye tija hakuna sehemu
ambapo huwezo kufika .Wazo ni ufunguo utakaofungua milango mingi na kukutanisha
na mtu yeyote unayemtaka.Kama huwezi kuzalisha wazo kila siku utakutana na watu
wale wale na hutakutana na watu muhimu wanaoweza kukusaidia.
Kupitia wazo la Adam Ngamange na mtandao
wake wa kijani kibichi ,Adam amekutana na watu mbalimbali ,mawaziri mbali mbali
na imemfungulia fursa mbalimbali .Ni wazo pekee litakalokutoa mahali ulipo
kwenda mahali pengine bila hivyo utabaki kuwa wewe na hakun mtu atakayekutoa.