![]() |
Tafiti zinaonesha kuwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo raia wake
hawana “Furaha” kwa kiasi cha hali ya juu. Mwanzoni sikuwa nikiamini hizi
tafiti hasa baada ya kugundua zimefanywa na watu ambao siyo kutoka Tanzania.
Hata hivyo, kwa zaidi ya mwaka mmoja nimekwa nikifanya uchunguzi wa ukweli
wa hizi taarifa. Ni kweli, “Watanzania wengi hawana furaha”. Unaweza ukapanda
daladala kutoka Mbagala mpaka Makumbusho bila kumuona abiria hata mmoja
akicheka. Hata ukiangalia nyuso zao hazina tabasamu. Pia unawaza ukaingia
kwenye mgahawa ukakuta kuna watu 6, kati ya hao sita, mmoja au wawili ndo wenye furaha, ndo wenye
nyuso zilizo na tabasamu. Wengine wanne waliobaki hawako tayari hata
kuongeleshwa(wamenuna). Nimewahi kuishi kwenye mtaa Fulani, si rahisi kuwakuta
pamoja wakiongea vizuri na kufurahi pamoja, kila mtu ana mambo yake, muda wote
wamekunjiana sura. Ingia hata kwenye Ofisi kubwa, Ofisi ambazo watu wana pokea
mishahara mikubwa na vyeo vikubwa, utashaangaa watu wana misongo ya mawazo
mpaka basi(Extreme Stress).
Wengine hata kuongeleshana hawaongeleshani. Nenda
barabarani, utakutana na watu wakiwa kwa makundi au mmojammoja, utashangaa watu
ni wawili au watu wakionesha kwenda sehemu moja kwa pamoja lakini hata
hawaongei, wala hawafurahii safari yao, wamekaziana sura kama wanaenda vitani.
Hata mtu mmoja, yuko anatembea ukimuangalia kama kaibeba dunia kichwani kwake,
ukimsalimia utafikiri alikuwa usingizini, sura kavu utafikiri siku ya tatu
hajacheka.
Kulingana na tafiti na uchunguzi wa muda mrefu, kuna mamba na vyanzo
ambavyo humpelekea mtu kukosa furaha katika maisha yake ya kila siku. Kama huna
furaha, unawaona watu hawana furaha, sababu kuu 12 zifuatazo ndizo hupelekea
binadamu kuishi bila furaha.
1.Kuogopa vitu ambavyo havijatokea.
Unaishi na mawazo ya kwamba jambo fulani halita fanikiwa, umejuaje?,
Unawaza kwamba nikisalitiwa na mpenzi wangu sijui itakuwaje, je asipokusaliti?,
unawaza kwamba itakuwaje nikifukuzwa kazi?, unajuaje kama utafukuzwa?, Tajiri
anawaza vipi siku akifirisika, hata usingizi hapati, kwani maskini waa sio
binadamu, Kila tukio katika maisha lina wakati wake na maumivu yake. Acha
kuumia kwa tukio ambalo halijatokea. Unajinyima raha tu mwenye. Acha wasi wasi.
2.Kuhifadhi vinyongo moyoni.
Kuishi huku ukimchukia mtu fulani ni sawa na
kunywa sumu huku ukidhani atakufa mtu mwingine. Tuache vinyongo na watu kwani
hatutakuwa na amani mioyoni mwetu, tutaishi bila furaha. Mtu akigombana na
rafiki yake jana, leo kamchukia hata amabaye hakuwepo kwenye ugomvi wao. Hapo
huwezi kuwa na furaha kwa sababu tayari huna wa kumfurahia.
3.Kutokujiamini
Jiamini unaweza kuwa Doctor, Unaweza ukawa kiongozi kama JK Nyerere, Pombe
Maguful, Obama, Zitto Kabwe, unaweza ukawa Mfanya biashara mkubwa kama Eric
Shigongo, Bahresa, Ruge Mtahaba, Unaweza ukawa Mchungaj au Shehe, unaweza ukawa
Mwanamuziki kama Ben Pol, Rose Mhando, Farid Kubanda, Jay Z, Unaweza ukawa
mwanamichezo kama Lionel Mess, Christiano Ronaldo, Fransis Cheka, Flola Mbasha,
Unaweza ukawa Professor, Unaweza ukawa Mwandishi. “Maisha haya, unaweza ukawa
yeyote yule unayetaka kuwa katika hii dunia”. Acha kukosa amani, amani acha
kukosa furaha, jiamini, chukua majukumu, pambana.
4.Marafiki. Ukiwa karibu ya watu 5 wezi, wewe utakuwa mwizi wa 6, ukiwa
karibu ya watu 5 matajiri we ni tajiri wa 6, ukiwa karibu ya watu 5 wapuuzi, we
ni mpuuzi wa 6, ukiwa karibu ya watu 5 wanye furaha wewe utakuwa mtu wa 6 kuwa
na furaha. “Ukiwa karibu ya watu 5 wasio na fuaha,
jiandae kuwa mtu wa 6……………….
Angalia watu unaokanao kwa muda mrefu kwa sababu wewe ni matokeo ya wale watu
wanaokuzunguka. Jaribu kuwa karibu na watu walio na furaha, ufurahie maisha
yako. Tafuta hata watu walio katika misingi ya dini. Muishi hata kwa
kufarijiana.
5.Msongo wa mawazo. Kuna watu wanajifanya wanajua kuwaza sana. Yeye ana
waza na kuwazua. Swala sio kuwaza, je unawaza nini? Walishakuwepo watu
wanaowaza kukushinda hata wewe, Yesu, Mohhamed, Soctrates, Plato, Aristotle,
Mahatma Gandhi, Confusius na wengine usio wajua. We leo unawaza nini?, Unawaza
wazo moja, kabla hujalimaliza ushawaza lingine mwishowe unajikuta mawazo
yanadandiana na kurundikana kichwani mpaka unapungua kilo. Tulia, pumua,
fikiria kitu, kitendee kazi, kimalize. Sio unawaza bila kufikiria. Fikiria
namna ya kuwaza tofatuiti na hapo ni “stress” na kujikosesha furaha bure.Ubomgo
wa mwanadamu unawa uwezo wa kufanyia kazi wazo moja kwa wakati mmoja zaidi ya
hapo unajidanganya. Hakuna sababu ya kurundika vingi kichwani
.
6.Mihemko hasi. Hii ni mihemo dhaifu kama vile, chuki, wivu, umbeya, roho
mbaya, hasira. Ukiwa na mihemko hii dhaifu siku zote utakuwa tofauti na wale
walio na mihemko imara kama vile upendo, uwazi, ushirikiano, umoja. Walio na
mihemko dhaifu ndo hao ambao hawana furha hata kidogo. Dakika moja kakuchekea
au kakusema vizuri, kesho kakununia na kukusema vibaya. “Mihemko hasi, ni adui
wa furaha katika maisha ya mwanadamu”.
7.Mahusiano. Utakutana na tajiri au mtu tu mwenye pesa zake, elimu nzuri,
kazi nzuri lakini cha kushangaza hana tabasamu wala bashasha maisha yake yote.
Kumbe haelewani na mke/mme wake, boss wake haelewani nae, mahusiano na majirani
sio mazuri, serikali nayo pia ina wasiwasi nae, kwa harakahaka huyu mtu hawezi
kuwa na furaha. Tujitahidi kujenga mahusiano mazuri na jamii zetu ili tukae kwa
amani na furaha.
8.Kutokujua furaha ni nini. Leo hii mtu ukimuuliza furaha ni nini, majibu
atakayokupa lazima utacheka na pia “utafurahi sana”. Watu hawajui furaha nini,
furaha sio amani ya nafsi, furaha sio kupata kile unachohitaji, furaha sio
kupata mke/mme mzuri, furaha sio amani tu ya rohoni, hapana, “Furaha ni
kukubali na kuridhika nafsini, rohoni, akillini na mwilini ”. Furaha nini swala
la wewe kuamua kufurahi au kuto kufurahi. Kuna watu hawana pesa ila bado wana
furaha, kuna yatima wenye furaha kuwashinda watu wenye baba na mama mpaka bibi
na babu. Furaha ni kuridhika. Furaha ni kutosheka. Furaha haipo kwa Tajiri wala
maskini, furaha anayo kila mtu, Furaha ni picha ya akilini, furaha ipo akilini
mwetu na sio sehemu yoyote. Ukiamua kuwa na furaha au usiwe na furaha ni wewe
tu. Furaha ni maamuzi. “Ukitaka kuwa na furaha kuwa, kama hutaki acha, chukia”
9.Fikra Potofu. Kuna watu wanaokunywa pombe, wanaotumia shisha, sigara,
ngono, wakidhani wanapata furaha, kule ni kujiua sio kujifurahisha. Ni sawa ni
kipofu anaevuka barabara. Kuna watu wanaodhani kuwa, kuwa na pesa ndo kuwa na
furaha sio kweli, kuna watu wanaodhani kuwa maskini hana furaha sio kweli,
furaha haina uhusiano wowote na pombe, pesa, sigara, nk. Mtu anakunywa pombe
akishalewa anawatukana watu, hiyo ni furaha au karaha. Tuache dhana potofu za
kwamba tukijihisi hatuna furaha, eti tukimbilie bar,
10.Kukata Tamaa. Kuna watu walisha poteza kila kitu kuhusu matumani ya
kufanikiwa. Ukiwa huna matumaini ni sawa na maiti inayoishi kwenye mwili wa
kuazima. Rudisha matumaini, amini kuwa kila kitu kinawezekana ukijituma, na
kupamba na kujifunza. Hakuna njia ya makto katika mafanikio. Amka, endelea
kupigania ndoto zako. “Mara tu uanapo kata tamaa, ndo hapo hapo unapopoteza
kila kitu”. Ukikata tamaa tayari unaanza kuwazia waliofanikiwa katika jambo
fulani na kujizika kwenye tabia haribifu kama vile wizi, uhuni, ujambazi, na
mwishowe kukosa amani na furaha ya maisha yako.
11.Ubinafsi. Kuna watu kila jambo, kila shida, kila tatizo ni la kwao peke
yao. Hatu swemi kwamba ukanadi shida na matatizo yako, ila jitahidi kutafuta
ushauri, kuongea na wenzio hasa wale unaowaamini kuwa ni sahihi kwako. Acha
kukumbatia shida zako. Tafuta tiba ya shida zako, “Kuficha shida na matatizo
yako ni sawa na kujivalisha sanda wewe mwenye ukiwa bado hai”. Pia wanasema
kuwa, “Mficha maradhi kifo humuumbua”. Kuna watu wanashida nyingi
zinazotatulika lakini wamezikumbatia. Kwa upande mwingine kila kinacho kukuta
wewe hata wenzio kilisha wakuta. Kama kufiwa watu walishafiwa sana, kama kuugua
watu walishaugua, kama kutukanwa au kudharauliwa watu walishadhadharauliwa
sana. Jua hicho kinachokukuta wewe muda huu pia na wenzio kilisha wakuta tangu
zama hizo. Kuwa na amani
12.Kuishi kwa yaliyopita. “Sahau yaliyopita, samehe yaliyopita, chukua
hatua, shika majukumu songa mbele”. Kujuta hakusaidii, acha kuishi na matukio
mabaya ya nyuma kichwani mwako. Kama kama kuna kitu ulisha kosea, hata kama ni
kwa uzembe wako mwenyewe jisamehe songa mbele, ukisha jisamehe wewe wasamee na
walio kukosea ili ufungue mifereji ya amani na furaha katika maisha.
Mbali na hayo, Kutokujua sababu ya maisha, kukosa imani ya rohoni, tama za
kupitiliza, kushinwa mambo mengi maishani, magonjwa, uvivu & uzembe,
kutokujifunza pia vinaweza kukufanya ukaishi bila “furaha”.
“Furaha ni Afya Ya Mwili, Akili, Nafsi & Mwili. Sababu kuu ya kuishi
hapa duniani ni “kufurahi””
Linda
Furaha Yako, Furahia Maisha Yako