Sikuwa na sababu ya kuandika hiki ila umenibidi
baada ya kuona kuna umuhimu wa kuwakumbusha vijana wenzangu wale walioko kwenye
mahusiano na zaidi kwa wale ambao bado hawajaingia kwenye safari hii nzuri
kuelekea ndoa.
Kumekuwa na upotoshaji sana kwa watu wanaoingia
kwenye mahusiano ,sijui wanapata wapi hayo maarifa,yawezekana ni waalimu wao wa
mahusiano ambao wanajali sana ustawi wa mwili kuliko kiroho cha mtu.
Tena wengine wanasema hupaswi kuanzisha mahusiano
mpaka umelijua kusudi la Mungu kwako,hahahahahah! Vipi kuhusu Ibrahim,Daudi na
wengine waliooa kabla.~kwa ufahamu wangu kusudi la Mungu halitafutwi bali
linajifunua lenyewe katika maisha yako~ Usidanganyike kihivyo wengine wapo kwa
ajili ya kuonyesha ufundi kwamba waonekane wanajua kufundisha sana lakini
ukifuatilia katika kuoa kwao nao hawakuoa wakiwa tayari wanajua kama
wanavyokulazimisha wewe leo.
Paulo anawaambia watu ,"ni heri kuoa kuliko
kuwaka tamaa", nikuulize swali paulo hakuwa anaelewa umuhimu wa kufahamu
umuhimu wa kulijua kusudi la Mungu? Mahali pengine pameandikwa *wale aliowajua
tangu asili akawaita..........* sitaki ninukuu kama kilivyoandikwa ila soma
~warumi 8:29-30~
Kwa hiyo kutokana na mafundisho hayo watu wengine
wameogopa kuingia kwenye mahusiano kwa sababu hawalijui kusudi lao,niseme tena
kusudi la Mungu linakuja kwangu kama *divine appointment*mtazame Mussa mpaka
anakutana na kusudi la Mungu kwanza hakuwa anafahamu hivyo ilikuja kama divine
appointment na vilevile alikuwa amekwisha oa tayari so i dont see any useful
point on that.
Sasa kama umeanza mahusiano kwa mtindo huu
ninaokwenda kukwambia ujue kabisa *hukupswa kuanza hivyo* na kama hukuanza hivi
sikwambii uvunje ila usalama wako ni mdogo kuliko maelezo ninayoweza kuyatoa na
kama hujaanza basi ~basi hupaswi kuanza hivi~;
Kuanzisha mahusiano
kimyakimya
Kwanini si vizuri kuanzisha kimyakimya?;
· Waweza
jikuta umeanzisha mahusiano na ndugu yako halafu hamfahamiani halafu mnakaa
mpaka kipindi mlichopangiana kujitambulisha kwa wazazi ghafla mnaambiwa nyinyi
ndugu,hapo mnakuwa mmepotezeana muda na tayari mioyo imeshashibana,kisa kama
hiki kilimkuta dada fulani ambaye ni rafiki yangu.
·Waweza
jikuta unakosa kibali cha wazazi kwani mtoto mwenye busara lazima awe na mzazi
mmoja ambaye anaweza kumwambia chochote na wakashauriana ,kwa kufanya hivi
mzazi anajisikia kuheshimiwa na utakuwa na mtu anayekuombea ili ufikie mwisho
mzuri.
· Unapata
ujasiri na kuamini kwamba hauko single tena hivyo na huwezi kuishi kama hauna
mtu ambaye unampango wa kuwa naye,utajibidiisha kufanya yapasayo kuupendeza
moyo wa mwenza wako na kuboresha future yenu.
*Hasara kubwa ya kuanzisha mahusiano kimyakimya au
kuyafanya yawe siri ni*
- Kukosa kutambulishwa au hata kutajwa mbele ya rafiki zake mpenzio.
- Ni ngumu kufika mwisho,naomba nieleweke ninaposema ngumu si kwamba haiwezekani hapana! Inawezekana kufika mwisho lakini kwa kupambana sana.
Nisiseme mengi lakini kama ni mahusiano ya kweli
kwanini yawe siri ,kwanini hakuna hata mtu wa kwenu anayekushauri au mzazi wa
kiroho anayekushauri na kukuombea rafiki eeeeeeh!,aseeee usifanye hivyo hata
kama anakuomba hebu tafuta kujiridhisha kwa kina kabla hujakubaliana nae.
Laban Nzelela