Neno la Mungu linasema linda sana moyo wako
...........moyo ni kiungo ambacho ili kiobekane kwa macho ni lazima kiwe nje ya
mwili wataalamu wanasema unakaa upande wa kushoto,hivyo unalazimika kumpasua
mtu ili uuone moyo wake.
Kwa kuwa hatuna uwezo wa kuuona moyo lakini tunao
uwezo wa kuhisi mapigo yake,kila yanapopanda na kushuka hali ya mtu hubadilika
ndo maana wataalamu wakaainisha shinikizo la damu la juu na la chini vyote hivi
vinategemea utendaji kazi wa moyo.
Moyo wako ni wako mwenyewe ,*sasa tunaulindaje moyo
ilihali hatuuoni*, je!biblia inaposema linda moyo wako inamaanisha moyo upi?
Sitazungumzia hayo ya biblia ina maana gani
kutuagiza tulinde moyo bali nataka nizungumze juu ya moyo unapenda mtu,moyo
ambao unasemekana kukabidhiwa kwa mwingine na mwenyenao.
Wengi kwa kushinda kulinda mioyo yao katika eneo la
mahusiano na wenza wao wamejikuta wakiwa na mabadiliko kadhaa wa kadhaa kama
vile;
Ngozi ya mwili kubadilika rangi;walioshindwa eneo
hili hawakushindwa miguuni bali walishindwa kwenye moyo na waliposhindwa
wakaangukia kwenye kubadili rangi za miili yao wakifikiri wataheshimika kumbe
sivyo.
Tabia kubadilika.;wengine baada ya kushindwa kwenye
moyo wakajikuta tabia zao zimebadilika wakawa watu wakujaribu pia mioyo ya watu
kwa kuwadanganya kwa lengo la kuwaumiza kama kulipa kisasi.
Yawezekana hujanielewa ,hebu fikiria kiatu ambacho
kimejaribiwa sana na watu na wewe ambaye unavaa size ileile na ulipojaribu
ukagundua kinapwaya kidogo ilihali ndo size yako ya siku zote,kwanini
kinaonekana kupwaya?
*Kinaonekana kupwaya kwa sababu ya kujaribiwa na
watu wengi*
Vivyo hivyo kwa moyo wako ikiwa unajaribiwa na watu
wengi hauwezi kubaki kama ulivyokuwa ni lazima utabadilika tu kama
nilivyoainisha hapo juu,si hivyo hata usemi wako utabadilika,marafiki
utabadilisha pia *maana moyo ukibadilika mtindo wa maisha hubadilika*
Usikubali kujaribu mahusiano na kutokatoka bila
utaratibu kama ni mcheza basketball tunasema make sure yaani when you start
,start it perfect.Acha kabisa habari za kusema labda hakuwa wangu au najaribu
kama tukifika mwisho basi Mungu ndo amepanga na msipofika Mungu
amepanga.Mweeeeeeeh! Waulize wana wa Israel safari ilikuwa mpango wa Mungu na
hawakufika wale walioanza kwani ulikuwa mpango wa Mungu wasifike.,? mtazame
Adam alipewa na Mungu lakini kupitia huyohuyo akamwacha Mungu ,"loooh
mwenzangu suala si hilo bali ni vile mnavyotembea ndiko kunakoamua mwisho
wenu"
Laban Nzelela
0656574760