"Tofali likiwekwa kwenye moto linazidi kuwa imara"




Kuna maeneo ambayo mara nyingi watu hutumiamatofali ya kuchoma kujenge nyumba zao.Nyumba zilizojengwa kwa matofali ya kuchomahuaminika kuwa ni imara kuliko matofali ya udongo wa kawaida.Tofali hupitishwa kwenye tanuru la moto ili kulifanya lizidi kuwa imara .

Watu wengi sana wamekuwa wakilaumu changamoto(wao wanaita matatizo )wanazopitia katika maisha yao na wamejikuta kila wakiamka wakifikiria kuhusu hayo yanayowakabili  kuliko kuangalia Mustakabali wa Maisha yao .

Asubuhi hii nilikuwa namsikiliza Pator Joel Osteen kupitia televisheni ya KTN ya Kenya akawa anasema kuwa unapopita kwenye matatizo na shida jaribu kukumbuka mema Mengi ambayo Mungu amekufanyia na mambo mazuri uliyowahi kufanya na ukifanya hivyo tatizo ulilo nalo halitakusumbua.

Changamoto unayopitia halina chochote cha kufanya juu ya hatma yako lakini ni njia tu ya kukundaa kuwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuhimiri adha na mambo mbalimbali ya Maisha .


Usikubali tatizo liwe sehemu ya maisha yako na kukufanya likurudishe nyuma .Unapaswa kujua kuwa matatizo hayawezi kukumaliza (problems can't finish you up).Kama tatizo haliwezi kukumaliza maana yake haliwezi kupunguza uwezo wa ndani na kusudi ambalo Mungu amekuweka Duniani kukuleta Duniani .


Dad Aneth Isaya Gerena hakuangalia Tatizo la kuwa Kiziwi .Kuwa Kiziwi hakukuzuia yeye kutumia uwezo wake wa ndani kufanya mambo makubwa na hasa ya kugusa jamii. Aneth Gerana katika moja ya simulizi aliyosimulia Kijana Jithamini Watsap Group anasema" Ndugu zangu mmeoona???? Hakika hakuna kisichowezekana chini ya jua ukimtegemea Mungu na kuwa na dhamira yakinifu.... Nawaomba msilie eti hamna ajira,,,,, hamna mtaji,,, hamna pa kuanzia...... Vyote hivyo unavyo wewe mwenyewe hapo ulipo kwa hiyo kuanzia leo amka Anza kuchakarika.... Pika chapati,, kaanga karanga na hata kuuza maji mwaka huu ulete mabadiliko unalipa kijana mwenye nguvu na maji bado yanatiririka mwilini.... Tunataka pose lako mtandaoni liwe for the reason sio unaishia kulike za watu jiulize wa ngapi wanalike zako? Mtu akipita page yako akasema ahaa hapa Kuna jambo mhimu..... At the end of the year utuletee ushuhuda hapa umefanya nini in 2016".

Nick wa Australia aliyezaliwa bila mikono wala miguu hakuangalia tatizo alilokuwa nalo lakini alitafuta kusudi la  yeye kuja Duniani .Nick anasema " nataka watu wasiogope .Siyo vile ulivyo kwa nje lakini vile ulivyoumbwa kuwa ndo kitu cha msingi kwenye maisha .Umetunikiwa ,una kipaji na mambo mengi ambayo yako ndani yako"


Ni marufuku kukaa chini na kulisujudu tatizo 

   JYB 0753836463