Jana usiku nilikuwa niko naperuzi kwenye
mtandao wa youtube na nikakutana na somo ambalo ndugu yangu Lameck Hulilo alilowahi kufundisha na
likanigusa sana .Somo hilo ni nguvu ya matendo
unaweza kulipata hapa : https://kijanajithamini1.blogspot.com/2016/07/nguvu-ya-matendo-by-lameck-amos.html
Muigizaji mmoja aliwahi kusema kuwa
maneno huwa yanajenga ghorofa lakini vitendo ni swala lingine .Watu huwa ni
wazuri sana katika kuongea na kuwa na mipango mikubwa lakini siyo watendaji wa
yale wanayoyasema na kuyasikia .Na hii ndio sifa ya watu wa kawaida
(average/poor people).Jack Ma Mwanzilishi wa Alibaba group aliwahi sema " Poor people think like university proffesor and do less than blind people " akimanisha kuwa Maskini wengi wanawaza kama maprofesa lakini utekelezaji wao wanazidiwa na vipofu .
Unapopanga kitu chochote,ni muhimu
kuweka mpango utekelezaji (Action plan) ili kile ulicholipanga kianze kuonekana
.Najua mwaka huu ulikuwa na mipango mingi na uliiandika lakini je , kipi mpaka
sasa umekifanya katika yale yote uliyoandika.
Vitendo huongea zaidi kuliko maneno(Action speak louder than words).Usiwe
ni mtu wa kupanga mdomoni tu kwa maneno lakini ni vema sana ukaangia kwenye
matendo .Kama umepanga kuanzisha biashara mwaka huu ni vizuri mara moja ukaweka
mpango wa kibiashara (business plan ) na
mpango wa kimasoko(marketing plan)
tayari kuingia kwenye utendaji .
Baada ya yule mwanamke aliyekuwa
anatokwa na damu kwa miaka mingi(Rejea
Maandiko ya Biblia kwa wale tunaomini Biblia) alipoamua kwenda kugusa pindo
la Yesu ndipo alipopata uponyaji .Hakuna jipya litakalotokea juu ya maisha yako kama huchukui hatua utabaki
kuwa na mipango mingi iliyoandikwa kwenye makaratasi ambayo hakuna chochote kitakachobadilika
katika maisha yako na thamani yako itabaki kuwa ile ile .
Ukweli ni kwamba makaburini ndiko kwenye utajiri mkubwa maana watu waliokuwa na
mawazo ya kuanzisha makampuni na biashara kubwa walikufa bila kufanyia
kazi .Kwani ufe na kampuni yako kichwani
ambayo ingeajiri vijana wengi wasio na ajira???
Ni kweli umekuwa ukihamasishwa sana
lakini ni kwa namna ipi kuhamasika kwako kumebadilisha mtazamo wako??? .Ni kwa
namna ipi umeanza kuweka yale unayosikia kwenye utekelezaji.
Ukianza mguu mmoja katika kutembea mguu
mwingine hufuata.Mara tu unapoanza kuchukua hatua ya utekelezaji mambo mengi na
mawazo mengi yatakuja lakini ukiendelea kusema nitafanya miaka si rafiki na
unaweza usifanye .Acha tabia ya kuahirisha mambo na kusema nitaanza kesho .
Mbona kuna vitu visivyo na tija umevipa
vipaumbele na huwa huchelewi kuvifanya kuliko kufanyia kazi ndoto zako kwa
mustakabali wa familia yako na maisha yako kwa ujumla???
0753836463