Moja ya sababu ya msingi kwa
timu yoyote kuweza kushinda ni mfumo wa uchezaji .Makocha huumiza sana vichwa
sana kujua timu yake kwa kutumia mfumo gani .Utasikia kocha anasema kuwa yeye atachezesha
timu yake kwa kutumia mfumo wa 4:4:2 na mwingine utasikia anachezesha mfumo wa 4:3:3 n.k
Muda mwingine timu
ikishindwa watu huanza kusema kuwa kocha alikosea kupanga mfumo wa kucheza
na utakuta kocha analazimika kubadili
mfumo wa kucheza kwa mechi zijazo ili kupata matokeo makubwa .
Ukisikia wanafunzi wengi
hawaajiriki na hawezi kujiajiri ni kutokana na mfumo wa Elimu butu ambao hautoi
Elimu ambayo inamuandaa mwanafunzi kupambana na mazingira yake na sasa
wanafunzi wengi wako mitaani huku wakiwa na vyeti utadhani na wameanza kuitwa wanafunzi hewa .Kinachopaswa kutafutwa hapa si mchawi wa Elimu yetu na kuingiza siasa
bali ni kwenda moja kwa moja kubadili mfumo wa Elimu tulionao(Salaam Zimfikie
waziri wa Elimu Dr Joyce Ndalichako ).
Kimsingi mfumo/aina ya
maisha tunayoishi yana mchango mkubwa katika maisha yetu na huweza
kusabababisha kufanikiwa kwetu au kutofanikiwa kwetu .Kuna mtu mfumo wa maisha
yake ni Uvivu(uzembe) mtu huyu kamwe hawezi kufanikiwa .Kuna mtu mwingine mfumo
wake wa maisha umejawa hofu na hawezi kufanya chochote ,mtu huyu hawezi
kufanikiwa kama hatabadili mfumo wa maisha yake .
Unapaswa kukaa chini na
kujiuliza ni mfumo gani wa maisha unaoishi kwa sasa .Andika chini na anza
kubadili kile ambacho unaweza kukibadili na bahati nzuri ni kwamba vitu vingi
tunao uwezo wa kuvibadili.
- Kama mfumo wa maisha umejawa na hofu ya usichokijua amua leo kubadili mfumo huu ambao haulengi kupata matokeo chanya.
- Kama mfumo wa maisha yako umejawa na Uvivu kuanzia leo amua kubadilika .
- Kama mfumo wako wa maisha ni kuongelea watu siku nzima ,amua kubadilisha mfumo huu unaokutafuna .
- Kama mfumo wako wa maisha ni kuambatana na watu ambao hawakusaidii chochote huku wakikutafuna amua kubadili mfumo huu mbaya usiokupeleka kwenye hatma yako
- Kama mfumo wako ni kuamini vitu hasi amua kuwa na mfumo chanya
0753836463