"NGUVU YA UWEZEKANO (POWER OF POSSIBILITY " ~Joas Yunus



Ili uweze kufanya kitu chochote katika maisha yako kinacholenga kubadili maisha yako lazima uwe na nguvu ya uwezekano ndani yako ,Nguvu hii ndio itakusukuma kuona yale ambayo watu wanasema hayawezekani kwako utaona kuwa yanawezekana .

Ukiona vitu vikubwa ambavyo vilitokea na vinazidi kutokea ambavyo vimefanywa na wanasayansi wakubwa ,ujue ni kutokana na nguvu ya uwezekano iliyoko ndani yao na kufanya vitu vikubwa ambavyo tunaviona leo .

Pastor David Oyedepo wa makanisa ya Winners Chapel na mmiliki wa Covenant University nchini Nigeria aliwahi kusema akiwa anaongea na mamilioni ya watu kwenye Kanisa lake maneno haya "What was impossible yesterday is possible today" akimanisha kuwa kile ambacho jana hakikuwezekana jana leo kinawezekana .

Ili ufanikiwe katika maisha yako lazima mtazamo wako uwe katika uwezekano na kuamini kuwa hakuna kisichowezekana kama ukiamua kwa dhati kufanya jambo hilo unalofikiri kulifanya .Yawezekana Jana halikuwezekana lakini leo likawezekana .

Wakati nasoma shule ya msingi mara kadhaa nilikuwa nafanya mitihani kwenye kitabu cha hesabu kilichoitwa "Mwandani mwa mwanafunzi" na kitabu kingine kilichoitwa " Jipime katika Hisabati" .Kuna wakati nilikutana na majaribio magumu sana na nikawa nawaza kuliacha jaribio hilo na kwenda jaribio lingine rahisi lakini Niliamini kuwa labda akili ilikuwa imechoka na ndio maana niliona maswali kuwa ni magumu na kesho yake nilivyojaribu kufanya jaribio lile lile nikakuta maswali yanafanyika vizuri.



Maisha yetu ni vile tunavoamini ,Kama tukiamini kuwa jambo linawezekana kila  Jambo litawezekana maana ubongo wetu hupokea kile tunachokiamini .Ukiamini kuwa jambo fulani haliwezekani kweli alitawezekana na ukisema linawezekana litawezakana maana msukumo wa kufanya jambo unaotoka kwenye ubongo hutokana na nini umeingiza kwenye ubongo .Kile unachoingiza kwenye ubongo ni kichochezi (impulse) na kisha ubongo hutoa mwitikio (reaction).

Nafahamu unaweza kuwa ulisikia wale watu waliotaka kujenga mnara wa Baberi ili wafike mbinguni .Kwa akili ya kawaida siyo rahisi kuamini kuwa Mnara ungeweza kujengwa kirahisi namna ile lakini nguvu ya uwezekano ndiyo iliwafanya waamue na waingie katika utendaji .Ukweli ni kwamba mnara ulianza kujengwa  kwa ushirikiano mkubwa na Mungu akastuka ikabidi awachanganye Lugha ili wasielewana na hawakufanikiwa kujenga Mnara maana Mungu aliwazidi akili.

Kama ukiamini katika Uwezekano hakuna kitu kitakachokuzuia na hivyo unaweza kuwa vyovyote unavyotaka kuwa bila kuangalia haijalishi kuna vizuizi vingapi .


0753836463