MAMBO YA KUFANYA TAREHE YA MWISHO WA MWAKA.



Yakiwa yamebaki takribani chini ya masaa 36 kufikia mwaka 2017 mwaka ambao JYB anaamini utakuwa mwaka wa mabadiliko nimeona nikuandikie mambo muhimu ya kufanya siku hiyo  ya  mwisho .

Hapa naomba ieleweke kuwa sitaki kubadilisha mambo yako uliyoyapanga kufanya kesho Lahasha lakini nataka nikueleze mambo ambayo ukiyafanya kesho yanaweza kufanya maisha yako yabadilike kabisa mwaka 2017 .

Najua unaweza kuwa ulishawahi kuyasikia mambo haya lakini kesho ukiyafanya kwa upya kabla ya sasa sita usiku yanaweza yakaandika historia mpya na ukarudi kunisimulia mwakani 2017 .Mambo haya ni ya msingi sana na nimelazimika kukufahamisha wewe ili uyafahamu .

1.Tafuta sehemu tulivu na anza kutafakari
Kesho ni siku ya kutafuta sehemu iliyotulia kabisa ,sehemu isiyo na kelele nyingi yaweza hata isiwe beach lakini hata chumba chako kinatosha kabisa kuwa sehemu nzuri .Anza kutafakari juu ya mwaka unaoisha ,mwaka 2016 .Tafakari ni wangapi wamekufa lakini wewe uko hai na una sababu gani za kuwa hai leo ???.Kaa chini tafakari uzima ulio nao na ulinzi ambao Mungu amekupa kisha mshukuru Mungu na Muahidi Mungu kulitafuta kusudi la kuwa hai leo na kuliishi mwaka 2017.

2.Jipongeze kwa yale uliyoyafanya .
Nikisema kujipongeza kuna mwingine hapa anawaza kujistarehesha kwa mambo mbalimbali Lahasha !.Hapa ni kuipongeza nafsi yako kwa maneno mazuri sana ..Jipongeze kwa yale uliyoyafanya 2016 hata kama ni madogo na hayajafikia lengo.Najua malengo yako mengi sana hayajitimia lakini  pata muda wa kujipongeza kwa yale uliyoyafanya .Iambie nafsi yako kuwa ee nafsi yangu umefanya yote haya kumbe hata haya mengine unaweza kuyafanya ukiamua .

3.Azimia kuachana na tabia zinazokurudisha nyuma (Weka kiapo)
Ni lazima upate muda wa kuangalia tabia ambazo zimesababisha kutokupiga hatua kwa mwaka 2016 na kuamua kuziacha 2017 kwa udi na uvumba .Ndiyo kama ulikuwa na tabia za uvivu azimia kuwa hutakuwa mvivu 2017.Kama ulikuwa na tabia za kutosoma vitabu azimia kuachana na tabia hiyo .Katika hili ni lazima ujiwekee mkakati kambambe na uiandike .Mifano hii inaweza kukuongoza .
-Mwaka 2017 nitahakikisha nasoma vitabu 10
-Mwaka 2017 nitahakikisha naamka saa kumi na moja alfajiri  kila siku .

4.Andaa taarifa yako ya mwaka na iweke kwenye faili lako .
 Hili pengine unaweza kuliona gumu lakini kumbe ndilo lanaweza kufanya mwaka 2017 kuwa mwaka wa KUINUKA.Taarifa ya maendeleo yako binafsi ni muhimu .Unaweza ukawaa hujawahi kufanya hili lakini anza kesho kufanya hivyo .Taarifa yako iwe na mambo yafuatayo

  • Malengo yako uliyokuwa umeweka 2016
  • Malengo yaliyofikika 2016
  • Malengo ambayo hayakufika 2016
  • Changamoto ulizokutana nazo 2016
  • .Malengo yako kwa mwaka 2017
  • Mikakati ya kufikia malengo yako 2017


Joas Yunus 0656110906