Dunia sasa
inakumbwa Na janga kubwa la ukosefu Wa ajira
.Hali hii imekuwa mbaya zaidi katika nchi zilizopo chini ya jangwa la
sahara ikiwemo Tanzania.Kwa sababu hiyo basi kumekuwa na wimbi kubwa la vijana
wenye elimu na wasio na elimu ambao wako mtaani bila kazi .
Lakini ukweli
unabaki palepale kuwa kama hakutakuwa na uwajibikaji kutoka kwa mtu binafsi
mpaka ngazi ya Taifa tatizo hili litaendelea kuwa vile vile na zaidi
litaendelea kuwa sugu .
Nimeona hivi
karibuni TCU ikifuta baadhi ya vyuo vikuu wakidai kuwa havina sifa lakini mimi
nadhani ni mpango wa serikali wa kupuguza idadi ya wasomi wengi walioko mtaani
.
Uwepo wa wasomi
wengi mimi naona siyo tatizo swala ni kwa jinsi gani wasomi hawa wamejengwa
katika misingi ya uwajibikaji na uwezo kutumia elimu zao kwa vitendo kuliko
kujengwa katika misingi ya kumaliza na kuanza kuzungusha bahasha.
Kama mtu binafsi
atajua wajibu wake na kuachana na mitazamo ya ubaguaji wa kazi tatizo la ajira halitakuwepo .Shida ni kwamba
wasomi wengi hawataki kuwajibika kwa kutumia nguvu zao wenyewe na mawazo yao
wanataka kufuata mawazo ya mtu na kujenga ndoto ya mtu .Msomi yuko radhi kwenda
ofisini ili jamii tu ione kama naye anaamka asubuhi kwenda ofisini akifika huko
yeye kazi yake ni kuchat tu na kusubiri muda wa kurudi nyumbani .Kuna mahali niliwahi fanya kazi na mtu wa jinsi hii ambaye muda mwingi kazini aliutumia kuchat sana huku akisubiri
muda wa kurudi nyumbani na mshahara mwisho wa mwezi tu .
Unaweza kukuta pia
wanafunzi wanamaliza vyuo na kutafuta kazi zaidi ya miaka mitatu bila mafanikio
wakati kwa muda huo wa kusubiri kazi mwanafunzi huyo anakuwa na uwezo wa
kuanzisha hata biashara ndogo na akaweza kuishi na kukuza uchumi wake binafsi
pamoja na pato la taifa kwa ujumla .Vijana Wameshindwa kuelewa kuwa kitu cha
kwanza na cha muhimu katika maisha sasa ni kuwa na wazo zuri na kama mtu ana uwezo mkubwa wa kuona fursa
tatizo la ajira litaisha na vijana hawatailalamikia serikali au mtu
yeyote.Vijana wamekua wavivu wa kufikiri na kusubiri miujiza itokee jambo
ambalo halitakuja kutokea hapa chini ya Jua
Familia kwa upande
mwingine wana wajibu wa kuwajibika katika kuandaa na kuwwajenga watoto wao
katika misingi ya kujiajiri .Utashangaa mtu anamaliza chuo halafu familia
inamuuliza " umeshaanza kuandika barua za kuomba kazi??? " badala ya
kuuliza " una wazo gani tukupe mtaji ?" .Familia zinapaswa kuondokana
na dhana ya ajira na kuamini kuwa hata
mtu akiamini kujiajiri anaweza kufika mbali .Kama wazazi wameajiriwa wasitamani
watoto wao waje waajiriwe .Kama kila familia itaweza kuzalisha ajira tatizo la ajira halitabaki kuwa kama lilivyo.
Asasi za kidini
zina mchango mkubwa katika kuondoa tatizo hili la ajira kwa kuanzisha miradi
mbalimbali ambayo itaajiri waumiini wake .Shida ni kwamba Dini sasa zimekuwa
kama biashara badala ya kubadili maisha ya watu na waumini pia wamekubali
miujiza kuliko uhalisia wa jambo .
Nimalize kwa kusema
kuwa tatizo hili litamalizwa na mimi na wewe kwa kuangalia namna ya kuzalisha
ajira ambazo zitaajiri watu kuliko kuendelea kulaumu serikali wakati sisi
wenyewe ni vyanzo vya ukosefu wa ajira kwa watu maana tumeshindwa hata
kuanzisha genge na kumuweka mtu walau apate elfu moja kwa siku.
Joas (JYB) 0753836463