USIPOJENGA LIBRARY YAKO, UNAJENGA MOCHWARI YAKO ~ Kashindi Edson

Naendelea Kupokea ODA ya kitabu hiki  0656110906


Miongoni mwa makosa makubwa ambayo tunayafanya hasa sisi watanzania na waafrika kwa ujumla ni kutokusoma vitabu vinavyotuongezea ujuzi na ufahamu wa mambo mbalimbali yanayohusu huu ulimwengu tunaoishi ambao una badilika kila iitwapo leo.

Inasemekana kuwa, hayo maarifa uliyonayo leo, baada ya miaka miwili na nusu ijayo yatakuwa hayana kazi tena kwa sababu kutakuwa na maarifa mengine mapya na taarifa zingine tofauti zinazoendana na mahitaji ya wakati huo. Tunaishi katika ulimwengu amabo unabadilika mara kwa mara, tunaishi katika ulimwengu ambao unaenda kasi sana tofauti na zamani ndio maana leo utasikia hapa kasi tu, mwendo kasi, voda fasta, nk. Haya yote yanadhihirisha ni jinsi gani ulimwengu tunaoishi unaenda kasi sana na kumpa nafasi kubwa yule mtu anayesoma alama za nyakati na kuendana na hii kasi ya mabadiliko kuanzia kifikra na kimtazamo.

Tumekuwa watu tunaojua sana tusichokijua. Kuna mtu ukikutana naye, afu ukamuuliza maswali kuhusu uongozi atakujibu, ukimuuliza kuhusu siasa atakujibu, ukimuuliza kuhusu sheria atakujibu, ukimuuliza kuhusu dini atakujibu, karibu kila kitu utakacho muuliza atakujibu. Muulize, ndugu yangu hayo majibu unayonipa uliyatoa wapi au nani alikuambia?. Utasikia, "acha dharau kwani unafikiri mi sijui mambo".

Bwana mmoja kutoka katika taifa la Marekani amewahi kufanya utafiti kwa muda wa miaka 10 akitafiti juu ya vitu wanavyofanywa na watu waliofanikiwa katika maisha yao ya kila siku huku akilinganisha na vile wanavyovifanya watu ambao hawajafanikiwa katika maisha yao ya kila siku na kugundua vitu 300 amabvyo wanavifanya watu waliofanikiwa ambavyo watu amabo hawajafanikwa hawavifanyi.

Ili gundulika kuwa, muda ambao sisi ambao hatujafanikwa tunaoutumia kuangalia tv, kuangalia movies, kuchati na marafiki na wachumba mitandaoni, kushinda kwenye vibanda vya mpira kuangalia Real Madridi Vs Barcelona, muda ambao sisi tunakuwa tunakaa vijiweni kupiga stori na umbeya, muda ambao sisi tunautumia bar kunywa pombe, watu waliofanikiwa huwa wanautumia kujifunza vitu vipya na kujipatia maarifa mapya na ujuzi mpya kupitia seminars, kusoma vitabu, kusikiliza maneno na mafundisho ya watu waliofanikiwa zaidi yao. Watu waliofanikiwa wanasoma vitabu kumshinda mtu yeyote hasa sisi ambao hatuja fanikiwa kama wao.

Nimewahi kufanya tafiti za baadhi ya viongozi wakubwa katika siasa na biashara kuangalia ni tabia zipi ambazo walikuwepo nazo katika kipindi cha maisha yao, tafiti zangu zilinistaajabisha sana, nilikuja kugundua kwamba, Bill Clinton amesoma vitabu zaidi ya 300 kwa kipindi cha muda wa miaka 3 akiwa chuoni, Mwl Nyerere amesoma vitabu zaida ya 7000 katika kipindi cha maisha yake, Nkwameh Nkrumah amesoma vitabu zaida ya 6000 katika kipindi cha maisha yake, Che Guavara amesoma vitabu zaidi ya 2000 katika kipindi cha maisha yake, Zitto Kabwe amesoma vitabu 56 mwaka 2016, 2 PAC amesoma vitabu zaidi ya 1000 katika kipindi cha maisha yake.

Je, mpaka leo, wewe umesoma vitabu vingapi?. Unaweza ukafanikiwa bila kusoma vitabu katika eneo lako lakini sio kwa kiwango kile ambacho ungekuwa unasoma vitabu kwa ajili ya mawazo mapya, ujuzi mpya, kuongeza uwezo wa kufikria, kujikuza kifikra. Utafanikiwa ndio lakini sio kwa kiwango kikubwa kama cha yule anayesoma vitabu na kupata taarifa mpya kila siku na kujiongezea busara na hekima katika kichwa chake.Elimu sio mpaka uende darasani, elimu inapatikana hata kwa kujisomeea vitabu ndio maana tafiti zinaonesha kuwa, asilimia 70 ya matajiri wa Tanzania ni darasa la saba. Wao wana elimu ya maisha na mafaniko ambayo haifundishwi darsani zaidi tu ya kujisomea vitabu na kujifunza kwa waliofanikiwa kupitia semina nk.

Nadhani huu ni muda wa kubadilika na kujifunza vitu vipya, kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu, kuhudhuria semina, kutumia muda wetu vizuri. Cha msingi hakuna faida ya wewe kuishi na mawazo ya yaliyozeeka wakati kuna mawazo mapya ambayo yanaweza kukubadilisha kimtazamo na kimaisha kwa ujumla.
Hii hapa chini ni orodha ya vitabu vikubwa sana ambavyo vinasomwa na viongozi wakubwa wa serikali na wafanya biashara wakubwa duniani na kwa bahati nzuri bei zake hazilingani hata hilo sharti lako au hicho kiatu chako unacho vaa ukienda kwa yule unayempenda.

1.THINK & GROW RICH
By Napolean Hill
Tsh. 20,000
2.RICH DAD POOR DAD
By Robert Kiyosaki
Tsh. 20,000

3.CASH FLOW QUADRANT
By Robert Kiyosaki
Tsh. 20,000
4.THINK BIG
By Ben Carson
Tsh. 20,000

5.WHY WE WANT YOU TO BE RICH
By Robert T Kiyosaki & Donald Drump
6.GIFTED HANDS
By Ben Carson
Tsh 20,000
7.The Art Of Leadership
By John C. Maxwel
Tsh 20,000

8.LIFE IS NOT FAIR BUT GOD IS GOOD
By Robert Schuller
Tsh. 20,000


9.IMPOSSIBLE IS POSSIBLE
John Mason
Tsh.20,000
10.THE POWER OF POSITIVE THINKING
By Norman Vicent Peale
Tsh. 20,000
11.GETTING PREPARED FOR POST UNIVERSITY LIFE
By Kelvin Kitaso
Tsh.10,000
12.FURAHIA MAHUSIANO

By Mussa Kisoma
Tsh. 10,000
13.SABABU 12 KWANINI NDOA NYINGI ZA LEO ZIMEJAA MIGOGORO NA KUVUNJIKA
By Peter Mitimingi
Tsh 10,000

14.MBINU 20 ZA KUFAULU MTIHANI
By Mageth Mushi
Tsh 10,000
15.MBINU 39 ZA KUPATA UTAJIRI
Tsh 10,000

NB; Usipojenga library yako unajenga mochwari yako.
Tupigie kupitia;

0757065702/0655794870