Kama sio wewe basi
ulishawahi kukutana na mtu ana wasi wasi, woga, hajiamini, hana furaha,
hawezi hata kuomba msaada pale anapokuwa na shida ambayo inaweza
kutatulika kwa haraka.
Mara zote katika maisha yetu ya kila siku binadamu huwa anaogopa vitu vifuatavyo;
1.#Kufa. 99% binadamu wote wanaogopa kufa, japokuwa wanajua kuwa kufa ni lazima. Kati ya watu 100, ni mtu mmoja ndio haogopi kufa.
2.Kupoteza #mapenzi(upendo)
kutoka kwa mtu unayempenda au mtu mhimu katika maisha yako. Mfano,
mzazi, ndugu, rafiki, mpenzi au mke na hata boss wako.
3.Kusikia neno #hapana. Tunaogopa sana kukataliwa pale tunapoomba kitu au kutoa mawazo kwa mtu fulani.
4.#Umaskini
Leo hii mtu anaweza akafanya jambo lolote hata kuua ili mradi aondoe
umaskini katika maisha yake. Mtu yuko radhi kufanya kazi yoyote angalau
kupunguza umasikini.
5.#Kuzeeka.
Kila mtu anajua kuwa ni lazima atazeeka lakini bado mtu anaogopa uzee.
Kuna mtu unaweza ukamuamkia akakuambia eti unamzeesha au akaitikia
kivingine. Kumbe anaogopa kuonekana umri mkubwa, anasahau kuwa ukikua
busara ndio zinapoongezeka.
6.#Mtihani
wa darasani. Hakuna kipindi ambacho binadamu anakuwa muoga kama kipindi
cha mtihani. Dictator maarufu duniani kutoka Ujerumani, Bwana Adolf
Lois Hitler, ambaye aliua Waisraeli zaidi ya million 6, alipoulizwa,
kitu gani unakiogopa katika maisha yako? akasema; #mtihani
7.Kuongea mbele za watu #wengi(kuongea
mbele ya hadhara). Kuna mtu ukimsimamisha mbele ya watu 500 au 1000
ukamuambia ongea lolote anaweza akaanza kulia. Mwingine anaweza akaanza
kuongea kilugha cha kwao. Mwingine atatetemeka mwili mzima na mkimuacha
dakika mbili kitakachotokea unajua mwenyewe.
8.#Magonjwa.
Hata kama unapenda wanawake vipi, ukiambiwa yule msichana ana
ngoma(ukimwi) hata salamu unaweza usimpe ukihisi atakuambiza. Huwa
tunaogopa magonjwa sana.
9.#Kukosea.
Tunajuwa kabisa kuwa hakuna binadamu ambaye hakosei lakini tunaogopa
kukosea, tunashindwa kujaribu vitu vipya kwa sababu ya woga wa kukosea.
"Kama hujawahi kukosea, basi wewe hujawahi kujaribu kitu kipya".
10.Kuzungumza na mtu kutoka tabaka la #juu.
Mfano kiongozi, tajiri, boss wako. Ghafla boss wako anakuita ofisini
kwake, huo woga, au rais anasimamisha gari mbele yako kisha anashuka
anakuambia kijana vipi?, utashikwa na kigugumizi ambacho hakijawahi
kutokea katika maisha yako.
NB; "Nothing to be feared, its to be understood".
Woga gani unaouna ni wa kijinga?, we ni kitu gani unakiogopa katika
maisha yako?, unahisi mambo gani mengine ambayo binadamu huwa
amayaogopa?