Ndoa ni changamoto ambayo tumeamua kwa makusudi kuikubali.
Bila kujali aina ya maisha ambayo kama wanandoa mnaishi kwa sasa ikiwa
ni ya furaha, amani au migogoro na hata kama mnafikiria talaka (Hatua
mbaya zaidi). Unapaswa uelewe jambo moja tu kuwa hakuna aliyebadilika
kati yenu ila mitazamo yenu tu.
Ningependa nitumie lugha ngumu zaidi kwamba ndoa ni tatizo tunaloamua kulichagua kwa makusudi, kwa Bahati mbaya Wengi huingia kwenye ndoa na mtazamo tofauti kabisa na huu na ndio maana baada ya muda huanza kuishiwa pumzi na uwezo wa kusonga mbele.
Tatizo ni tofauti kati ya hali halisi na matarajio / kiwango kwa kulinganisha na matarajio ya mtu binafsi. Tatizo sio kwamba ni zile tofauti zilizopo isipokuwa namna tunavyo tafsiri tofauti hizo na uhusika wetu.
Hizi hapa ni tofauti ambazo zinajitokeza Mara tu baada ya kuingia kwenye ndoa.
1. Kwa ridhaa yetu tunaamua kumpa mwingine uhuru Wetu.
2. Tunaamua kuwajibika kwa mtu mwingine.
3. Tunajitiisha chini ya mamlaka ya mtu mwingine.
4. Tunakubali kugawana yangu ili iwe yetu.
5. Tunakubali kuwaongeza ndugu pamoja na changamoto zao.
6. Tunakubali kuongeza uwajibikaji wa kifedha kwa mtu mwingine.
7. Tunakubali kuanza kuishi maisha ya kufuatiliana, kuulizana, kung'ang'aniana nk.
.
Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanasababishwa na uamuzi wetu wa kuingia kwenye ndoa, kwa bahati mbaya watu huona ng'ambo bila kujua njia ya kupitia kufika huko mbele.
Furaha na amani ya kweli inayodumu katika ndoa sio ile ya kununuliana maua, zawadi na kutoana out (Japo kuwa haya pia ni mambo ya msingi) ni ile inayotokana na jinsi mnavyoweza kuzikabili tofauti zenu na kufikia kwenye ukomavu wa mahusiano.
Hii ndio sababu hasa mahusiano machanga yana hatari na kadhia ya kuingia katika migogoro ya Mara kwa Mara ukilinganisha na yaliyo chukua muda mrefu. Sio tu yaliyo muda ila watu walioamua kuzichukua tofauti zao kwa mtazamo chanya zaidi.
Changamoto zinakomaza na kujenga mahusiano kwa watu walio chanya lakini kwa walio na mtazamo hasi zinawaua na kuwamaliza. Bahati mbaya kichwa cha mada hii ni ndoa ni changamoto.Kama unaweza kubadilisha mtazamo wako kuhusiana na ndoa na kukubali mabadiliko yanayotokana na ndoa upo karibu kabisa na kuanza kuishi maisha ya furaha na Amani katika ndoa.
Lakini kuna swali la kujiuliza Mungu alikusudia ndoa iwe changamoto? La!! Mungu aliikusudia na hata leo haibadiriki kwamba ndoa ni utimilifu wa mahusiano ya ndani (intimacy) kati ya mwanaume na mwanamke. Ni nini sasa kilichobadilika?
Rejea katika kitabu cha mwanzo mara baada ya Hawa kuletwa kwa Adam, Adam alimtambua na kumsifu kwa maneno mwanana hata kabla ya kutambulishwa na Mungu.Baada ya kuwa Adam amekubali kula tunda alilopewa na mkewe, Mungu alipouliza Adam alimshambulia mkewe "si huyu mwanamke uliyenipa"? Adam hakutaka kiwajibika na hii ndio kitu ninakiita mtazamo.
Ufahamu ulibadilika, Mtazamo ukabadilika hali kadharika na mahusiano yetu. Kwa sababu hiyo kuna umhimu wa kujifunza na kujipatia ufahamu mpya kuhusiana na ndoa ili mitazamo yetu ibadilike.
Ndoa ni Kitu chema, Wazo la dhahabu la Mungu... Taasisi kubwa kabisa ambayo Mungu ameifanya.
Nduguyo,
Ushindi Ellioth
Valentine gift box '17