Ni wapi hisia zinaishia? Akili zinaanzia na wapi zinapokutana?
Hauwezi kuwa na ndoa yenye furaha ikiwa hauwezi kuwa committed kwa mwenzi wako. Unapoamua kuingia katika ndoa siyo suala la hisia tu unapaswa ujue kuwa ni commitments ambazo unaziweka juu ya huyo mwenzi wako.
Kile Kiapo ambacho Mara nyingi tunaapa siku ya ndoa ni maridhiano yetu mbele za watu. Na kwa kuthibitisha hilo ndio maana hata nchi inazo sheria za ndoa na bila kujali ndoa ilifungwa wapi, wale wanaotumika husimama kwa niaba ya sheria za nchi. Na hata Wale ambao hawakupita katika mifumo rasmi, sheria inaeleza kuwa kuishi na mwanamke kiunyumba kwa kipindi cha miezi mitatu itatambulika kuwa ni mme na mke.
Sio hivyo tu!! Biblia inaiona ndoa kama agano baina ya mtu mme na mtu mke. Na ndoa huwa na ushahidi katika ulimwengu wa roho na agano lake ni lile agano la damu. Watalaam wa biolojia wanataja kuwa mishipa ya damu iliyopo katika uke wa mwanamke haina kazi nyingine yoyote na ndio maana hata baada ya damu nyingi kutoka haichukuliwi kama ni tatizo au kama inahitajika tiba, ni kama Mungu alikusudia uwepo wake kuwa ni agano la kiroho ambalo ni lazima likamilishwe na damu (Covenant price).
Ndiyo maana kuna hatari kubwa kiroho na matokeo yake kiakili na kimwili mtu anapoamua kuliarifu agano lake na mke wa ujana wake. Mambo mengi na shida nyingi ambazo watu wanakumbana nazo leo chanzo ni kushindwa kuheshimu agano hilo. Biblia imesisitiza kwa ufupi sana "ndoa iheshimiwe na watu wote" siyo mme au mke ila ni ndoa kwa sababu ya uthamani wake.
Kwa kuwa ndoa ni commitment, tunalazimika kutenda sawia bila Kujali tupo katika hali gani? Hakuna hali nzuri au mbaya inayokupa nafasi ya kufanya vibaya kinyume na kiapo chako. Ujue ni Lazima mwisho wa siku uangalie maamuzi yako kulingana na commitments ambazo uliamua kufanya.
Siyo kwa sababu umefurahi, au umekasirishwa me au mke anapaswa kutendewa sawa na jinsi ambavyo inavyostahili na si vinginevyo.
Lakini hisia ni kitu cha kawaida miongoni mwa wanandoa zipo Nyakati wanakasirishwa, wanafurahishwa lakini hali hizi zote hazibadirishi kile kiapo chako cha ndoa na hata kama Hukuapa unapoingia ni lazima ufahamu kuwa una commitment kwa mwenzi wako.
Watu waoneshe hisia zao, hakuna shida Lakini wasiruhusu hisia zako zikawafanya wakatenda isivyo. Petro anasema ikiwa kutakuwa na manung'uniko hata maombi yatapata vikwazo. Hii ndio nguvu ya commitments. Kukomaa katika mahusianao ni pale unapoweza kuchagua tendo jema pamoja na kuwa unajisikia vibaya. Na unapofikia hapa amani na furaha ya ndoa inabaki kuwa ni jambo la kudumu.
Unapoamua Kuwa katika ndoa jua kuwa ungeweza kuwa na yeyote lakini kwa kumchagua mmoja ujue una commitments.
Nitazungumza zaidi katika mada ijayo nitakapozungumzia Mada ya "wajibu wako, haki yangu" ni kitu gani kianze!!
Nimekuwa na ugumu wa kupata tafsiri nzuri ya kiswahili kwa neno commitments lakini inaweza kuwa ni ahadi yenye nguvu kisheria... Ahadi inayofunga.
Tuonane wakati ujao....
Nduguyo,
Ushindi Elliott
Valentine's gift box '17