Haki au wajibu ni nini kianze.
Mahali palipo na kukwaruzana au machafuko utasikia watu wanagombana na
kudai haki zao,vyombo vya utetezi, jumuiya za kimataifa, kijamii nyingi
zinajengwa ili zidai haki. Haki ni kiini cha migogoro na sintofahamu
katika jamii nyingi sana, inawezekana shida na mtazamo huu umeingia pia
katika ndoa.... Mama anataka haki, kadharika baba.
Ni nani anayedai wajibu wake?? Ni Nani anayeuliza wajibu wake, Ni nani anayetafuta wajibu wake. Wajibu wako ndio haki ya mwingine. Wajibu na haki ni pande mbili za uzani linganifu. Unapouliza haki, fikiria kama umetimiza wajibu wako. Mahusiano yanayozingatia usawa huu ndio yaliyo na nafasi ya kustawi.
Paulo kwa Waefeso kuhusiana na mahusiano ya ndoa anaasa "Na nyinyi waume wapendeni wake zenu Kama Kristo alivyolipenda kanisa, Kwa wanawake anawaagiza kuwatii waume zao. Wakati huo Petrol anawaagiza wanaume kuishi kwa akili, msisitizo kwa wanawake unabaki kuwa ni kuwatii waume zao.
Kila mtu amepewa wajibu katika eneo ambalo ni jaribu kubwa kwake, wakati jaribu kubwa la mwanamke ni mamlaka (utawala), jaribu kubwa kwa wanaume ni tamaa!! Unaposikia madai ya haki sawa, usawa wa kijinsia na wito wa Beijing, Tamwa nk hivi vyote ni taasisi au hatua za kutaka kusawazisha mamlaka na utawala, haaishi kwenye majukwaa tu ya siasa inaingia mpaka katika ndoa.
Wakati watu wengi tunaamini wanawake wana wivu zaidi katika mahusiano, lakini ukweli ni kuwa wanaume tuna wivu uliokithiri. Mwanamke kuwa msaliti katika ndoa hufikiriwa ni jambo baya zaidi kuliko mwanaume kufanya hivyo, na hata inapotokea watu wameachana ni wanaume wanajisikia vibaya zaidi pale wanapomuona yule mwanamke na mwanaume mwingine. Lakini pamoja na haya yote ni wanaume wanaoongoza Kwa tamaa ambayo hudhaniwa kuwa ni upendo.
Japo kuwa ukiwauliza wengi hawakubali, lakini Ayubu anasema nimeweka Agano na macho yangu nitamtazamaje mwanamke kwa kumtamani? Hii inaonesha maamuzi ya makusudi ya Ayubu kushughulika na tatizo sugu la wanaume.
Wanaume wameagizwa kuwapenda wanawake wanaotii, kadharika wanawake kuwatii wanaume wanaowapenda. Kama kanuni hii ikizingatiwa migogoro mingi itakwisha katika ndoa, na kama isipozingatiwa matokeo yake ni dhahiri pia.
Tuonane katika kipindi kijacho, nitakapoeleza lugha za upendo, itakayofuatiwa na ile dhana ya "utii".
Nduguyo Ushindi Ellioth
Valentine's gift box "17