NITAMILIKI BIASHARA YANGU SEHEMU YA KWANZA ~Jyb





Habari yako ndugu msomaji wa makala  .Natumaini umeshaandika malengo yako ya mwaka na kama hujaandika wiki hii isiishe Kabla hujaandika malengo yako.Ninachoweza kukwambia ni kuwa kuweka malengo ni hatua ya kwanza ,kuweka mpango utekelezaji wa lengo ni hatua ya pili lakini kufanyia kazi mpango uliojiwekea ndiyo hatua itakayoleta matokeo makubwa katika maisha yako.

Mwezi huu tutakuwa tukiangalia namna ya kumiliki biashara yako .Sielewi kwanini imeniingia akilini hii lakini naamini kuwa watu wengi wameweka malengo ya kuanzisha biashara  lakini hawajui watafanyaje .Wameweka lengo la kuanzisha biashara lakini akiangalia pesa aliyonayo anakata tamaa.Mwezi huu nitaenda na wewe na kuhakikisha unaanza biashara hata kama watu wanaogopa na watu wengi wanakuogopesha kutokana na hali hii ya uchumi.

Leo nataka nikwambia katika hatua ya kwanza ya kumiliki biashara yako nataka nikueleze kwanini unapaswa kuanzisha biashara yako (vitu vyako ) kwa mwaka 2017 hata kama hukuwahi kuwaza hivyo .Zifuatazo ni sababu ambazo rafiki yako JYB anaona zinafanya wewe uanzishe biashara yako 2017.

1.Kuanzisha biashara ni Mpango wa Mungu
Mpango wa Mungu ni kuwa kila mtu amiliki na afanye vitu vyake.Mantiki ya kutawala ni pamoja na kuanzisha vitu vyetu wenyewe na kutokuwa na Kuingiliwa na mtu yeyote .Hapa haimanishi wewe uache kazi hapana inamanisha hata kama unaendelea kufanya kazi kwa mtu utafute eneo lako la kutawala .Eneo la kujidai .Eneo ambalo hakuna mtu yeyote atakayekuingilia katika eneo lako .Huo ndio mpango wa MUNGU ambao watu wengi wameshindwa kuelewa kwa mapana yake na ndiyo sababu kubwa inayonisukuma nikwambie kuwa lazima  ufikiri kuanzisha biashara yako(vitu vyako) hata kama hukuwaza kufanya hivyo tokea unazaliwa.


2.Hata watu wa Agano la Kale na Jipya walifanya biashara
Najua wewe unaweza kuwa huamini Biblia na pengine huwa hupendi kabisa kusikia lakini leo naomba iwe siku ya kwanza kusikia mifano hii michache ya watu wa agano la kale na jipya ambao nao walifanya biashara .Mistari hii ya Biblia wakati naisoma leo hii imenisukuma nichukue Simu yangu nakuanza kukuandikia wewe ili ufahamu kuwa biashara haijaanzishwa na akina Bilgate wala akina Mengi tu lakini kumbe ilikuwepo toka zamani na watu walihimizwa kufanya biashara.Mistari hii ya Biblia ikupe hamasa kubwa ya kuanza biashara .

A. Mwanzo 34:10 Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo.

B. Isaya 23:18 Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa Bwana, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za Bwana, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.

C.Ezekieli 28:5 kwa hekima yako nyingi, na kwa biashara yako, umeongeza utajiri wako, na moyo wako umeinuka kwa sababu ya utajiri wako

D. Mathayo 22:5 Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake;

Naweza kuwa nimekuboa kwa mistari hiyo lakini nimeona kabisa inatoa hamasa ya wewe kuanzisha biashara hasa mwaka huu ambao JYB anataka kila mtu aanzishe biashara .

3.Biashara yako ndiyo maisha yako .

Wakati tunasoma enzi zile kabla hatujaanza kuzeeka kulikuwa na methali isimayo kuwa "Mtegemea cha nduguye hufa maskini " .Methali hiyo sikuwa naielewa kwa kipindi hicho na sasa baada ya kuwa mtu wa kufuatilia vitu nimeanza kuielewa .Ukweli ni kwamba vitu vyako ndivyo vitakupa utajiri siyo vya mwingine .Hata kama uko wapi na unafanya kazi wapi hili unapaswa kulielewa hili kabisa ...Hakuna mwajiri chini ya jua labda azaliwe mwaka huu anayetaka ufanikiwe kama unavyohitaji wewe...Kuna vitu anaweza kukufanyia ukadhani kuwa anataka ufanikiwe kumbe ndiyo anafisha ndoto yako ...

Kwa leo Niishie hapa ,azimia kuanza vyako ,,,Usikose mwendelezo huu wa kujua kwanini unapaswa kuanza biashara .

@Joas 0656110906