Jana
nilikueleza baadhi ya sababu zinazokulazimu kuanzisha biashara yako mwenyewe
kama hukusoma bonyeza hapa kusoma
Leo tutaendelea
kuangalia sababu zingine ambazo zitakufanya uanzishe biashara yako mwaka huu
hata kama uko kazini .
Biashara yako ndiyo usalama wako
Moja ya hofu
ilyotanda makazini (kwenye ajira) ni usalama wa kazi (Job security) .Ukiwa
umeajiriwa ajira yako si salama yapo mengi ambayo yanaweza kutokea na hivyo
unaishi kwa wasiwasi mwingi uwapao kazini na mara nyingi nidhamu ya woga
ndiyo hutawala eneo lako la kazi ili kumfurahisha mwajiri .Jambo hili siyo baya
lakini ukweli linatafuna maisha yako ya baadaye maana maisha ni safari ndefu.
Mwaka huu yamekwisha ni mwaka ambao hutaishi kwa
wasiwasi maana utaanzisha vyako hata kama ni genge litakuwa lako si la mwingine
...hata kama ni kituo cha kutoa ushauri wa kitaalamu ni chako na si cha
mwingine .Ndiyo chako ni chako tu ndivyo
waswahili wanavyosema .
Ni ukweli
usioweza kupingwa kuwa mfumo wa ajira unawafanya watu wajengwe katika
misingi ya hofu na kutojiamini na kama ndiyo hivyo hatma za maisha yetu
yaliyojawa na hofu ni mbaya sana .
Biashara yako(vitu vyako) ndiyo urithi wa watoto wako na vizazi
vyako
Mtoto wako
hautamrithisha kazi yako maana ulipo si pako lakini kama utaanzisha vyako
utakuwa unaandaa mazingira ya mtoto wako .Kuna dhana kuwa elimu ndiyo urithi wa
mtoto lakini ukweli siku hizi elimu bila mwelekeo haileti tija .Ni muda wa
kuangalia baada ya kupata elimu nini mtoto ameandaliwa ?.
Watanzania
wengi wanadhani kazi zao nzuri ndizo za watoto wao hapana mtoto wako fahamu
kabisa wakati akimaliza shule atakuja kukuuliza wewe umpe kazi.Wakati
unaendelea na kazi yako anza kuwaza kuweka misingi na maandalizi ya watoto wako
hata kama unawaona bado wadogo kesho watamaliza shule na kurudi kwako .Andaa
mazingira ukiwa bado una nguvu na rasirimali za kutosha maana siku zilizo mbaya zinakuja ambazo uwezo wa kufikiri ,nguvu na
rasirimali nyingine hautakuwa nazo au zitakuwa zimepungua .
Biashara yako (vitu vyako ) ndivyo vitakuza uelewa/ufahamu wako
Hapa kuna
wengine wanaweza aidha wasinielewe au kunielewa vibaya .Ukiwa kwenye vitu vya
mwingine huna muda mwingi wa kujifunza vitu maana unafuata ratiba na
utaratibu wa mwingine tofauti na ukiwa una mambo yako ambayo yanakufanya
ufikiri kwa kina juu ya nini ufanye ..Unapata muda mwingi wa kutafakari vitu
vyako kwa mapana zaidi na kuongeza maarifa zaidi .
Siri ni hii
kadri unavyoitumia akili yako ndivyo akili yako inavokuwa na kuongezeka na hii
hufuata kanuni ya Baolojia ya law of use and disuse inayosema kuwa "kadri kitu kinavyotumika sana
kinaongezeka na kama hakitumiki kinapotea"
Joas (Jyb)
0656110906
Kesho tutaangalia namna ya kupata wazo la biashara kwa mwaka huu
usikose kabisa mfululizo huu utakaokufanya uanze biashara yako (vitu vyako )
mwaka huu.